Spika Ndugai: Baadhi ya watu wananiandika vibaya kwasababu mimi Mgogo

Spika Ndugai: Baadhi ya watu wananiandika vibaya kwasababu mimi Mgogo

Kamanda Asiyechoka

JF-Expert Member
Joined
Sep 13, 2020
Posts
3,315
Reaction score
5,058
SPIKA NDUGAI: KUTOKANA NA MAZOEA YA WAGOGO KUDHARAULIKA NDIO KINACHOSABABISHA MIMI KUSHAMBULIWA MITANDAONI

"Mengi mnayoyasikia wakati mwingine sio kweli kihivyo, nchi yetu ina upotoshaji mkubwa sana wa mambo mengi, na sisi viongozi siwezi kusimama leo nifafanue hili, kesho nifafanue lile, keshokutwa nifafanue lile.

Niseme ukweli, kuna baadhi wananiandika vibaya kila kukicha sio kwasababu nina pungufu lolote, kwasababu mimi mgogo, dharau ile, muwe mnaelewa vitu vingine, kabisa ninawaambieni.

Huyu ataongea kitu gani! Wana akili hawa! Yaani umeshaharauliwa hata kabla haujapanda ile ngazi, wako wenye attitude za namna hiyo, sasa baadhi ya vijana wetu nao wanapiga madongo kumbe haelewi kinachosumbua hapa ni nini! Ni attitude tu.

Na wakati mwingine mnakuwa hamjapata ufafanuzi wa jambo lenyewe likoje na sababu zake ni zipi"

Spika wa Bunge
Job Ndugai

 
Sio kweli, asitake kutuletea ukabila ambao watanzania hatuna habari nao. Matendo na maneno yake bungeni ndio chanzo cha yeye kusemwa vibaya, ameishusha hadhi ya taasisi ya bunge.

Mfano issue ya kina Mdee na wenzake, ilishawahi kufanyiwa kazi na bunge siku za nyuma na uamuzi kuchukuliwa kwa wabunge wa CUF, kwanini leo Ndugai aendelee kuwalea wale huku wakipoteza pesa za walipa kodi kinyume cha sheria?

Hapa hakuna ukabila, Ndugai afuate sheria na taratibu zilizopo hakuna mtu atakaye msema vibaya, tena atapata uungwaji mkono asioutegemea.
 
SPIKA NDUGAI: KUTOKANA NA MAZOEA YA WAGOGO KUDHARAULIKA NDIO KINACHOSABABISHA MIMI KUSHAMBULIWA MITANDAONI
"Kuna baadhi wananiandika vibaya kila kukicha, sio kwa sababu nina pungufu lolote, ni kwa sababu mimi ni Mgogo, dharau hii!" Job Ndugai, Spika wa Bunge
#MkutanoMkuuwaWagogo https://t.co/JmhLQzphKhView attachment 2061332
Malechela, Le Mutuzi, Ben Pal, Job Ndugai, Mavunde, Juma Nkamia, Matonya hawa ni baadhi tu ya Wagogo ambao ni Icons.... Ukijua tabia zao utaelewa kwa nini tunasema WAKOMA wana akili za hovyo.
 
Mh.Spika
Zigo lako libebe mwenyewe,wagogo hatudharauliwi kabisa na usitake kupata sympathy kutoka kwetu kwa maovu yako.
Time and again tumekuwa tukikuambia dhuluma haidumu na ikidumu huangamiza,sasa ona jinsi Mwenyezimungu anavyofanya mambo yake na tunamuomba akushushe uwe mtu wa kawaida kama sisi....ona kwa:
Paul Makonda
Sabaya
Bashiru
Polepole
na wengi wengine.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Haaa mitandaoni hawajui hata kabila au ugogo wako, people are keen to what you said na character yako ikoje, je unachosema unamaanisha au ww ni mnafiki, hutabiriki, huaminiki, huna au unayo public trust etc. Na hii yote inatokana na who you are thru your previous records, records zipo hazifutiki, ukiwa wa hovyo hovyo, public inakuchukuliwa hovyo hovyo.

Period. 😅🐧
 
Back
Top Bottom