Chadema walisusa matokeo ya uchaguzi 2020, walikaza hata walioshinda wasiende kuapishwa na kushiriki bunge, sasa kinachowauma chadema kutaka akina Halima wasishiriki vikao vya bunge ni nini?
Akina Halima mmeshawafukuza kwenye chama chenu tayari hivyo wametumia mbinu zao binafsi na akina Ndugai kuendelea kuhudhuria bunge pamoja na kufukuzwa kwenye chama chao. Sasa hoja ya Chadema na Bawacha kutaka Ndugai awafukuze bungeni akina Halima ni nini?. Nini kinawawasha akina Halima kubaki bungeni wakati wao wameyasusa matokeo wenyewe?
Au wanataka sasa kuyakubali matokeo ya uchaguzi ule ili wachague watu wao badala ya akina Halima kwenda bungeni?
Kwani hela wanazokipwa akina Mdee kwa kwenda bungeni ni za chadema?
Nijuavyo mimi akina Halima waliona ni upuizi kuachia nafasi 19 zote ziende bure kama vionhozi wa chadema walivyotaka iwe. Kwa njia zao na mipango yao wenyewe nje ya chama wakazitumia hizo nafasi badala ya zingebaki tupu au kuchukuliwa na CCM.
Je, kama Ndugai angeamua kuwapa CCM hizo nafasi 19 za ubunge zilizosuswa na chadema viongozi wa chadema wangesema nini? Bado wangedai?
Chadema mlishasusa kupeleka majina 18 ya wabunge wa viti maalumu kwenda kula kiapo, pia mlitaka hata yule mbunge mmoja aliyechaguliwa jimboni asiende bungeni, hivyo wenyewe kwa njia zao wako bungeni na nyie mmeshawafukuza kwenye chama, hivyo mwacheni Spika Ndugai ahangaike nao yeye mwenyewe kwa kutumia njia zake nyie endeleeni kutoyatambua matokeo hivyohivyo.
Au mnataka kuwapeleka wake zetu bungeni badala ya akina Halima? Kama ni hivyo anzeni kwanza kwa kuyakubali matokeo ya uchaguzi kabla ya kudai akina Halima watoke bungeni.
Nafikiri wakati mwingine tunatakiwa kuwa wakweli pale ambapo kila kitu kiko wazi. Tusingoje kuabishwa. Pamoja na mimi kutopenda kususia uachaguzi, lakini hiyo ni hiari ya chama cha siasa. Kususia uchaguzi kunakuja na faida au hasara zote za kususia. Tokeo kubwa la kususia ni kupoteza nafasi zote ambazo zingipatikana na huo uchaguzi. Kwa maana hiyo unaposusia huwezi susia nusu nusu. Kwa kifupiwaliposusia walipoteza haki ya ubunge wa vitu maalum.
Hata kama CHADEMA wangeamuwa kususia nusu nusu, ni lazima taratibu za kujaza hizo nafasi zifuatwe. Mimi nasikitika chombe kikubwa kama bunge kwa ushauri mbovu wa Ndugai wanaweza kukubali wabunge toka CHADEMA, ambao CHADEMA ilisema haikuwateua. Kama hawakuteuliwa, hiyo inatosha kuwaondoa buneni, kwa sababu hawana kigezo chochote cha kuwaruhusu kuwa wabunge, kwa sababu sponsor wao CHADEMA amewakana.
Tatizo lingine, ni pale mwanachama anapokuwa amefukuzwa chama. Ukifukuzwa kwenye chama, huwezi kuendelea kuwa mbunge unaotegemea uteuzi wa chama husika. Hawa tayari si wanachama, kwa hiyo hawawezi kuendelea kuwa wabunge kwa sababu tayari wamekosa sifa baada ya kufukuzwa.
Mimi mara nyingi namuona Ndugai anaendesha chombo muhimu kihuni. Bunge siyo sehemu tunayotegemea kutakuwa na uvunjaji wa katiba. Bunge linatakiwa kuilinda katiba. Kuilinda katiba ni pamoja na kuhakikisha wabune wote walioapishwa au watakaoapishwa wako bungeni kisheria kwa kuwa na sifa zote za kuwa wabunge. Kama ndugai hana hakika ni juu yake kutafuta ushauri wa kisheria kuhusu hilo.
Mwisho, namuomba Ndugai aheshimu bunge na kiti chake. Aache uzandika na matani ambayo hayana tija. Matani na uzandiki na ishara tosha kuwa huyu Bwana kiti cha Uspika kimempwaya, ndiyo maana anafanya maamuzi ya ovyo na inaonekana hana msimamo. Ndugai alikuwa ni kati ya wabunge ambao walikuwa wanampigia Magufuli, lakini leo hii utamuona anajaribu na yeye kujionyesha ana mawazo yake, ndiyo maana akachomekea ishu ya bandari ya Bagamoyo, huku huko nyuma alikuwa nyuma ya ishu. Nafikiri huyu ni mtu wa kujipendekeza, na hakuna mtu wa hatari kama mtu wa kujipendekeza.