Chadema walisusa matokeo ya uchaguzi 2025, walikaza hata walioshinda wasiende kuapishwa na kushiriki bunge, sasa kinachowauma chadema kutaka akina Halima wasishiriki vikao vya bunge ni nini?
Akina Halima mmeshawafukuza kwenye chama chenu tayari hivyo wametumia mbinu zao binafsi na akina Ndugai kuendelea kuhudhuria bunge pamoja na kufukuzwa kwenye chama chao. Sasa hoja ya Chadema na Bawacha kutaka Ndugai awafukuze bungeni akina Halima ni nini?. Nini kinawawasha akina Halima kubaki bungeni wakati wao wameyasusa matokeo wenyewe?
Au wanataka sasa kuyakubali matokeo ya uchaguzi ule ili wachague watu wao badala ya akina Halima kwenda bungeni?
Kwani hela wanazokipwa akina Mdee kwa kwenda bungeni ni za chadema?
Nijuavyo mimi akina Halima waliona ni upuizi kuachia nafasi 19 zote ziende bure kama vionhozi wa chadema walivyotaka iwe. Kwa njia zao na mipango yao wenyewe nje ya chama wakazitumia hizo nafasi badala ya zingebaki tupu au kuchukuliwa na CCM.
Je, kama Ndugai angeamua kuwapa CCM hizo nafasi 19 za ubunge zilizosuswa na chadema viongozi wa chadema wangesema nini? Bado wangedai?
Chadema mlishasusa kupeleka majina 18 ya wabunge wa viti maalumu kwenda kula kiapo, pia mlitaka hata yule mbunge mmoja aliyechaguliwa jimboni asiende bungeni, hivyo wenyewe kwa njia zao wako bungeni na nyie mmeshawafukuza kwwnye chama, hivyo mwacheni Spika Ndugai ahangaike nao yeye mwenyewe kwa kutumia njia zake nyie endeleeni kutoyatambua matokeo hivyohivyo.
Au mnataka kuwapeleka wake zetu bungeni badala ya akina halima? Kama ni hivyo anzeni kwanza kwa kuyakubali matokeo ya uchaguzi kabla ya kudai akina Halima watoke bungeni.