Spika Ndugai haya uliyosema kuhusu Wabunge wa CHADEMA waliofukuzwa mbona mwaka 2017 hukuyasema wabunge wa CUF walipotimuliwa?

Sasa kama watu walishafukuzwa Chadema, na chama chao kikakuandikia barua kuwa walishafukuzwa wewe kwa nini hutaki kuamini kuwa walishafukuzwa? Ok kama huamini kwa nini usiombe uthibitisho kuwa walifukuzwa na vikao halali?

Umesema vyema. Lakini mimi niko kwenye kipengere hiki...

Unasema angeomba uthibitisho wa "kufukuzwa kwao". Uthibitisho gani wakati anayo barua mkononi mwake?

Chama kinatoa taarifa kwa Spika, na si vinginevyo kama anavyonwabwaja kuwa sijui walete hiki na kile nk nk..

Uthibitisho hutolewa mahakamani. Na wenye uhalali wa kuomba uthibitisho (uhalali wa mchakato wa kufukuzwa kwao ni hawa wabunge 19, siyo Spika) kupitia mahakama kama wakitaka...

What Mr Speaker is doing is stupidity with ignorance in it...!
 
Sasa kama watu walishafukuzwa Chadema, na chama chao kikakuandikia barua kuwa walishafukuzwa wewe kwa nini hutaki kuamini kuwa walishafukuzwa? Ok kama huamini kwa nini usiombe uthibitisho kuwa walifukuzwa na vikao halali?
jamaa alitaka siku ya kikao angekuwepo ili ahakikishe akidi kama imetimia na maamuzi yapi yamefikiwa - huyu ndiyo kiongozi wa chombo kikubwa kabisa cha kutunga sheria na kuisimamia Serikali nchini kwetu.

Pole Tanzania hawa ndiyo wanaukuzika ukiwa mzima.
 
Ndugai kaa fikiria, suala la katiba halina uzoefu we fuata tu, hata kama unakinga ya kuto shitakiwa, uoni aibu? Waliofukuzwa wanajijuwa hawana chama wewe na naibu wako mnapishana mara hakuna taarifa mara kwa karatasi hii sio ya kuichukulia hatua, kumbuka ulie kuwa unashauriana ujinga huo hayupo tena, huko peke yako ukiendeza ujinga, acha!
 
Hayo si ndio ameyaomba? au hiyo taarifa yake hujaipata?
 
Kuna wakati unajiuliza kwanini mungu alimtoa Mahiga ama Ndulu katika hùu ulimwengu na kumuacha mtu wa hovyo kama huyu Ndugai. Kuna binadamu kama akina Kijazi walitakiwa wawepo sio huyu.
Mkuu maneno huumba na ndicho kilichotokea kwa mwendazake. Tena yeye mwenyewe alivyo spana mkononi!
 
Akipewa muhtasari atataka picha za kikao.
 
Amekiri kupokea barua ya CHADEMA lakini alipuuza hakuijibu. Angewajibu kwa barua rasmi CHADEMA kwamba barua yao ilikuwa 'kipeperushi'. Badala yake amejibu kwa ngonjera za bungeni! Kwani yeye halazimiki kufuata utaratibu rasmi wa mawasiliano kati ya ofisi yake na CHADEMA?
Kwa kitendo hiki yeye Ndugai hajawadhalilisha bungeni na mbele ya jamii wanawake anaojigamba anawalinda hata kwa kudharau maamuzi na barua ya CHADEMA kuhusu masuala yao binafsi na chama chao?
Anaposema "wanalindwa" anamaanisha bunge zima limeamua wazi kupingana na CHADEMA juu ya masuala ya ndani ya chama hicho?
Spika anatakiwa kuwa neutral katika BUNGE vinginevyo litakuwa kama kamati ya CCM.
 
Lakini hii sio mara ya kwanza bunge kuwa na watu wa aina hiyo, hata akina Zitto waliwahi kusurvive bungeni kwa njia hiyo. Chadema walisusa inawabidi wakae kimya hawawezi kulalamika kwa niaba ya wapiga kura wote, kwani akina Halima hawakuikosea chadema bali katiba na walipa kodi wote. Nia ya cdm lazima waiweke wazi. Je, wanataka kuyatambua matokeo na kupeleka watu wao bungeni, je, wana uchungu na hela za walipakodi wanazolipwa akina Halima, je, nini hasa?
 
Hoja ya cdm kwenye malalamiko yao ni nini? Je, wanataka kuyatambua matokeo na kupeleka watu wao bungeni? Je, wanataka kuokoa hela zetu wananazolipwa akina Halima kimakosa? je, wanalalamikia Spika kuvunja katiba ya nchi kuruhusu wabunge waliofukuzwa kwenye chama kilevi, Je, wanalalamikia mchakato wa kuwapata akina Halima? au nini?

Nadhani hoja yao kama cdm iliishia pale walipoyakataa matokeo na walipowafukuza uwanachama akina Halima, full stop!
 
Kwani alitumia sheria gani kuwabakiza akina Zitto kwenye ubunge hadi mwisho wa uhai wa bunge? Mbona wakati ule wa akina zito Bawacha hawakuimba mapambio kama wakati huu. Njaa kitu kibaya sana.
 
Sikatai hilo hata mimi, lakini hoja kama hiyo sio ya chadema tena, wao walishayakana matokeo hadi sasa na wamesema wamewafukuza uwanachama akina Halima, shida ya cdm ni nini hapo? Waache watu wengine walalamike lakini sio chadema.
 
Sikatai hilo hata mimi, lakini hoja kama hiyo sio ya chadema tena, wao walishayakana matokeo hadi sasa na wamesema wamewafukuza uwanachama akina Halima, shida ya cdm ni nini hapo? Waache watu wengine walalamike lakini sio chadema.


Spika anasema hao kina Halima ni Wanachama wa Cdm na ndiyo maana ya wao kuendelea kuwa wabunge kwa tiketi ya cdm, Cdm inasema hao sio tena wanachama wao na imepeleka barua kwa spika kumjulisha jambo hilo.

Ni hivi, kama spika angesema hao kina Halima sio wanachama wa chama chochote hivi sasa basi hapo cdm isingekuwa na haki ya kulalamika isipokuwa kesi ingebaki kwa spika kuvunja katiba kwa kuwaruhusu Watu wawe wabunge bila kupitia chama cha siasa lakini hivi sasa cdm inayo haki ya kulalamika kwasababu chama chao kinatumika kuhalalisha ubunge wa kina Halima kinyume na katiba ya nchi na kinyume na maamuzi ya chama chao kwani hao kina Halima wamefukuzwa chamani.

Ndugai ni spika wa ajabu sana, historia itamuandika hivyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…