Spika Ndugai: Kama bunge halitaibana na kuihoji serikali nani atafanya jukumu hilo?

Spika Ndugai: Kama bunge halitaibana na kuihoji serikali nani atafanya jukumu hilo?

Spika Ndugai amewataka wabunge kutimiza wajibu wao wa kikatiba kama mhimili wa kuibana, kuihoji na kusimamia serikali wakati wote tena bila kuchoka.

Spika Ndugai amehoji kama wabunge wanashindwa kufanya kazi hiyo wanataka nani mwingine aifanye?

Source: ITV habari
Hehehe 🤣🤣🤣
 
Hao ni wabunge wa NDIOOO kila kitu, kama mlivyohitaji. Hata Covid 19 waliingizwa humo kwa kukubali masharti hayohayo.

20210524_173034.jpg
 
Ukitamka Speaker, akili yangu inawakumbuka Msekwa na Sitta.

Sioni kama ntakuja kukumbuka eti Ndungai aliwahi kuwa Speaker.
 
Spika Ndugai amewataka wabunge kutimiza wajibu wao wa kikatiba kama mhimili wa kuibana, kuihoji na kusimamia serikali wakati wote tena bila kuchoka.

Spika Ndugai amehoji kama wabunge wanashindwa kufanya kazi hiyo wanataka nani mwingine aifanye?

Source: ITV habari
Watanzania tunakokotwa na wahuni walioingia ktk siasa na kujitwalia madaraka makubwa ya kutuamulia. Tunafanywa wajinga sana tena bila aibu wala chembe ya woga. Ipo siku hawa wajinga na waoga watasema hapana
 
Ndugai itakuwa ni malaria imepanda kichwani labda.Unaanzaje na unaanzia wapi kumuuliza swali mtu ambae ndiye kakupa ubunge?!
 
Spika Ndugai amewataka wabunge kutimiza wajibu wao wa kikatiba kama mhimili wa kuibana, kuihoji na kusimamia serikali wakati wote tena bila kuchoka.

Spika Ndugai amehoji kama wabunge wanashindwa kufanya kazi hiyo wanataka nani mwingine aifanye?

Source: ITV habari
Ndiyo analijua leo hili? Wakati Bunge lilipokuwa na Wabunge wa upinzani yeye ndiye alikuwa anawa shutdown wapinzani wasiibane Serikali na wakati mwingine akiwapa wabunge vilaza wa CCM airtime waijibie Serikali kwa njia ya kuwakejeli wapinzani. Ndungai huyu ndiye ameshusha hadhi ya Bunge hadi lionekane kama kijiwe cha wahuni tu.
 
Ukiona Mkeo na nyumba ndogo yako wamekuwa mashosti basi kaa chonjo unaumizwa !! na kwenye ngazi ya Taifa ukiona Bunge na Serikali ni kitu kimoja basi mwananchi kaa chonjo unaumizwa!!
 
Ndugai na Mwendazake mpango wao ulikuwa wawe na bunge dhaifu nabutu ambalo lisingekuwa na Uwezo wa kuisimamia serikali ili mambo yao likiwemo la kumuongezea muda Jiwe yangekuwa rahisi kuyapitisha!
Mpango wao haukutimia na ndiyo maana nchi imeambulia bunge butu ; Ndugai analolihimiza kuisimamia serikali kazi inayowashinda!!
Ishukuriwe Corona
 
Ndugai ndo chanzo Cha bunge kuwa butu, pale bungeni ameingiza wabunge hawana vyama, nape aliwahi hoji akaishia kutishiwa na spika ndugai.Ndugai ajiuzulu uspika
 
Swali ikihojiwa kuhusu hao wabunge COVID 19 wanaokula hela bure anaiweka kapuni ,mengine anajifanya mfuatiliaji kama nesi wa zamu
Hao wabunge wanatimiza wajibu wao kitaifa,tatizo ni chadema kukosa usingizi
 
Ndugai ni MNAFIKI tena akiwa ni mtu mzima mwenye umri wa miaka zaidi ya 60, bunge lililopita hakukuwa na wabunge waliouliza kuhusu watu wasiojulikana? Manunuzi ya ndege bila kuidhinishwa na bunge haikuulizwa? Na mengine mengi? Je, akiwa kiongozi mkuu wa bunge Ndugai alihakikisha bunge analoongoza linaibana serikali? Ndugai yupo sawa sawa kweli?
Akili ya Ndugai inajua mbunge lazima awe CCM
 
Back
Top Bottom