Spika Ndugai: Kama bunge halitaibana na kuihoji serikali nani atafanya jukumu hilo?

Hehehe 🤣🤣🤣
 
 
Ukitamka Speaker, akili yangu inawakumbuka Msekwa na Sitta.

Sioni kama ntakuja kukumbuka eti Ndungai aliwahi kuwa Speaker.
 
Rubish spika huyu yeye na jiwe ndo chanzo cha haya
 
Watanzania tunakokotwa na wahuni walioingia ktk siasa na kujitwalia madaraka makubwa ya kutuamulia. Tunafanywa wajinga sana tena bila aibu wala chembe ya woga. Ipo siku hawa wajinga na waoga watasema hapana
 
Ndugai itakuwa ni malaria imepanda kichwani labda.Unaanzaje na unaanzia wapi kumuuliza swali mtu ambae ndiye kakupa ubunge?!
 
Ndiyo analijua leo hili? Wakati Bunge lilipokuwa na Wabunge wa upinzani yeye ndiye alikuwa anawa shutdown wapinzani wasiibane Serikali na wakati mwingine akiwapa wabunge vilaza wa CCM airtime waijibie Serikali kwa njia ya kuwakejeli wapinzani. Ndungai huyu ndiye ameshusha hadhi ya Bunge hadi lionekane kama kijiwe cha wahuni tu.
 
Ukiona Mkeo na nyumba ndogo yako wamekuwa mashosti basi kaa chonjo unaumizwa !! na kwenye ngazi ya Taifa ukiona Bunge na Serikali ni kitu kimoja basi mwananchi kaa chonjo unaumizwa!!
 
Ishukuriwe Corona
 
Ndugai ndo chanzo Cha bunge kuwa butu, pale bungeni ameingiza wabunge hawana vyama, nape aliwahi hoji akaishia kutishiwa na spika ndugai.Ndugai ajiuzulu uspika
 
Swali ikihojiwa kuhusu hao wabunge COVID 19 wanaokula hela bure anaiweka kapuni ,mengine anajifanya mfuatiliaji kama nesi wa zamu
Hao wabunge wanatimiza wajibu wao kitaifa,tatizo ni chadema kukosa usingizi
 
Akili ya Ndugai inajua mbunge lazima awe CCM
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…