Spika Ndugai: Kutoka 'kuua' upinzani Bungeni hadi kuwa 'mpinzani' Bungeni

Ndugai anayo msemo wake mmoja hivi akirefers wimbo ule ya kua ukishachafuka uwezi kushafishika Tena.
Kama anaamini hivyo anasubiri Nini, mvua inyesha au jua kuchwea.
 
Hahahahahaaa nineupenda huu uchambuzi.

Kwenye biblia imeandikwa "watu wangu msipoimba basi mawe yatageuka na yataimba na kumsifu Allah"

Sasa naona yanatimia kwa Ndugai,alishiriki kuua upinzani bungeni usisikike leo ameanza kusikika yeye akiimba wimbo wa upinzani akiwa peke yake/ usicheze na reality hahahajaahaa
Maisha hayatabiriki. Maisha yana mambo mengi ya ajabu na yenye kutoa majibu. Maisha yanakwenda kasi sana. Job Yustino Ndugai, Mbunge wa Kongwa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yamemfika. Yamemkuta na amefikishwa kwenye ukuta. 'Ameropoka'; akajitetea, akaomba radhi lakini hakukubaliwa. Rais 'kumjibu' kwa 'kumtaja' hadharani inamaanisha kuwa msamaha haukutolewa. Lazima jambo liwe.

Ndugai na historia ya kuukandamiza upinzani Bungeni. Tangu mwanzoni mwa utawala wa Mwendazake na baada ya Ndugai kupokea maelekezo ya kuwashughulikia wapinzani ndani ya Bunge na nje kuachwa Mwendazake mwenyewe, Ndugai alikuwa mahiri bila ubahili katika kusimamia maagizo kutoka juu katika kuwashughulikia wapinzani. Aliwafukuza kutoka Ukumbi wa Bunge Wabunge wa upinzani; aliwaburuza Kamati ya Maadili; aliwasimamisha kwa tambo wahusika na hata kuwatisha. Kilele cha yote ni pale alipomvua kikatili Ubunge Tundu Lissu.

Ndugai aliona ameyapatia. Aliona amefika. Alikuwa akicheka kwa mateso ya wenzake na kukasirika kwa mafanikio ya wapinzani Bungeni. Upinzani ukafika tamati Bungeni mwaka 2020 baada ya 'uchafuzi mkuu' wa mwaka huo. Upinzani ukafutwa Bungeni. Ndugai akafurahi sirini na hadharani. Akakiona kiti cha Spika rahisi na chepesi kuliko nyasi katika kukiongoza bila kuunguza. Akaendelea kuwakera wapinzani kwa kuwaapisha na kuwakumbatia Wabunge haramu 'wa CHADEMA' wakiongozwa na Halima Mdee.

Leo, karma imemrudi Ndugai. Haaminiki. Hatakiwi. Hapendwi. Hathaminiki. Haeleleweki. Hapokelewi simu zake wala kujibiwa jumbe zake. Hapewi ushirikiano na wale alioamini walikuwa wakimfurahia. Amekwama. Anahema. Anazama. Amekuwa mpinzani wao Bungeni. Amekuwa mpingaji wao chamani. Amekuwa mpinzani wao sirini na hadharani. Upinzani umefufuka Bungeni kupitia yeye. Hakika, karma is real!

Spika Ndugai asithubutu kuongoza kikao chochote cha Bunge. Akifanya hivyo, hataupenda mwisho wake utakaorushwa mubashara runingani.

What goes around, comes around!

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Dodoma)
 
Kwanza alikosea namba ya kuomba radhi,piki kaishajiuzulu

Sent from my SM-N960F using JamiiForums mobile app
 
Mzee Tupa tupa, haujaandika point ya msingi inayomhusu Ndugai, siamini kama kweli umesahau au umeamua kumpumzusha yule mgogo.

Ndugai anakuwa spika WA Bunge WA Kwanza aliyejitungia Sheria ya kutoshitakiwa .

Alijiona untouchable.

Sasa karma imemrudia.

Hakuna anayemtetea hata mmoja.
 
Alikuwa katuliaaa ndugai anakula AC ya mjengo pale dodoma maskini akaenda kuita wale wagogo wenzake dakika 5 tu alichosema maisha yake anayaona machungu mnoo., shenztyp
 
Watu wanatumia fursa, kosa moja goli 100
 
Maisha hayatabiriki. Maisha yana mambo mengi ya ajabu na yenye kutoa majibu. Maisha yanakwenda kasi sana. Job Yustino Ndugai, Mbunge wa Kongwa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yamemfika. Yamemkuta na amefikishwa kwenye ukuta. 'Ameropoka'; akajitetea, akaomba radhi lakini hakukubaliwa. Rais 'kumjibu' kwa 'kumtaja' hadharani inamaanisha kuwa msamaha haukutolewa. Lazima jambo liwe.

Ndugai na historia ya kuukandamiza upinzani Bungeni. Tangu mwanzoni mwa utawala wa Mwendazake na baada ya Ndugai kupokea maelekezo ya kuwashughulikia wapinzani ndani ya Bunge na nje kuachwa Mwendazake mwenyewe, Ndugai alikuwa mahiri bila ubahili katika kusimamia maagizo kutoka juu katika kuwashughulikia wapinzani. Aliwafukuza kutoka Ukumbi wa Bunge Wabunge wa upinzani; aliwaburuza Kamati ya Maadili; aliwasimamisha kwa tambo wahusika na hata kuwatisha. Kilele cha yote ni pale alipomvua kikatili Ubunge Tundu Lissu.

Ndugai aliona ameyapatia. Aliona amefika. Alikuwa akicheka kwa mateso ya wenzake na kukasirika kwa mafanikio ya wapinzani Bungeni. Upinzani ukafika tamati Bungeni mwaka 2020 baada ya 'uchafuzi mkuu' wa mwaka huo. Upinzani ukafutwa Bungeni. Ndugai akafurahi sirini na hadharani. Akakiona kiti cha Spika rahisi na chepesi kuliko nyasi katika kukiongoza bila kuunguza. Akaendelea kuwakera wapinzani kwa kuwaapisha na kuwakumbatia Wabunge haramu 'wa CHADEMA' wakiongozwa na Halima Mdee.

Leo, karma imemrudi Ndugai. Haaminiki. Hatakiwi. Hapendwi. Hathaminiki. Haeleleweki. Hapokelewi simu zake wala kujibiwa jumbe zake. Hapewi ushirikiano na wale alioamini walikuwa wakimfurahia. Amekwama. Anahema. Anazama. Amekuwa mpinzani wao Bungeni. Amekuwa mpingaji wao chamani. Amekuwa mpinzani wao sirini na hadharani. Upinzani umefufuka Bungeni kupitia yeye. Hakika, karma is real!

Spika Ndugai asithubutu kuongoza kikao chochote cha Bunge. Akifanya hivyo, hataupenda mwisho wake utakaorushwa mubashara runingani.

What goes around, comes around!

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Dodoma)
 
Kidume cha Bungeni - chaliiiii, CCM vana laaah.

1647849971870.png
 
Bado mmoja karma inamchelewesha huyu anajiona bado raisi wa jamhuri.
 
Back
Top Bottom