Spika Ndugai: Lissu kwa miaka 10 ya Ubunge hakuna 'legacy' yoyote aliyoacha Jimboni kwake

Spika Ndugai: Lissu kwa miaka 10 ya Ubunge hakuna 'legacy' yoyote aliyoacha Jimboni kwake

Etwege

JF-Expert Member
Joined
Jul 4, 2018
Posts
7,207
Reaction score
17,674
Leo kwenye mjadala wa kupitisha bajeti ya wizara ya maji, spika Ndugai amesema kwa masikitiko makubwa kuwa licha ya Tundu Lissu kuwa mbunge wa Ikungi kwa miaka 10 lakini hakuna alichofanya cha kukumbukwa na wananchi!

Ndugai amesema hata kijiji anachotoka Lisu hakuweza kuwapelekea maji kwa miaka kumi!

20210507_145623.jpg

My take
Nguvu aliyoitumia Lissu mzee wa MIGA kutetea Acacia angeielekeza kutetea wananchi wa jimbo lake wangefika mbali sana kwa miaka 10.

Inasikitisha sana wananchi hawana maji alafu yeye anatetea wezi wa madini !!!
 
Kuna kitu kikubwa sana hakiko sawa kwa Ndugai.

Hajui kabisa majukumu ya Spika. Spika na mipasho kwa wabunge wa upinzani wapi na wapi hivi? Sijui Lisu alimfanyaga nini Ndugai aisee. Anashindwa kabisa kuacha kumuongelea.
 
Jibu hoja yake, aliacha nini jimboni?
 
Hivi ni huko Ikungi tu spika ameona tatizo la maji? Kwake Kongwa kila kijiji kina maji? Je huko kwetu Isimani Ndugai anakujua pamoja na shida yake ya maji? Na huko ni kwa Lissu?

Halafu ivi mbunge anahela za kupeleka maji kwenye jimbo lake, kama sio seriksli ndiyo yenye jukumu hilo? Spika amejiridhisha kuwa Lisu hakuwahi kupigia kelele shida ya maji jimboni kwake na nchi nzima?

Nachoona Ndugai anahukumiwa kwa dhambi aliyoshiriki kuwatendea CDM, na hususani Lisu na Mbowe maana majina yao hayamkauki kinywani mwake pengine kuliko jina la mamsapu wake! Dawa kwake ni kuweka wazi dhambi hizo ili afunguliwe vifungo vya hukumu ambayo itamuandama maisha yake yote.
 
Back
Top Bottom