Hivi ni huko Ikungi tu spika ameona tatizo la maji? Kwake Kongwa kila kijiji kina maji? Je huko kwetu Isimani Ndugai anakujua pamoja na shida yake ya maji? Na huko ni kwa Lissu?
Halafu ivi mbunge anahela za kupeleka maji kwenye jimbo lake, kama sio seriksli ndiyo yenye jukumu hilo? Spika amejiridhisha kuwa Lisu hakuwahi kupigia kelele shida ya maji jimboni kwake na nchi nzima?
Nachoona Ndugai anahukumiwa kwa dhambi aliyoshiriki kuwatendea CDM, na hususani Lisu na Mbowe maana majina yao hayamkauki kinywani mwake pengine kuliko jina la mamsapu wake! Dawa kwake ni kuweka wazi dhambi hizo ili afunguliwe vifungo vya hukumu ambayo itamuandama maisha yake yote.