Spika Ndugai: Nampa onyo kali Jenerali Ulimwengu kuchunga ulimi wake, haipendezi mtu wa umri wake kuwa anaongea ovyo ovyo

Spika Ndugai: Nampa onyo kali Jenerali Ulimwengu kuchunga ulimi wake, haipendezi mtu wa umri wake kuwa anaongea ovyo ovyo

Kuna faida gani kuwa na raia asiyekuwa na kitu kichwani kama Ndugai, si akheri huyo asiyekuwa raia lakini mchango wake kwa jamii unaonekana?
Ndugai ni mzigo mzito sana kwa taifa hili.. Hata sielewi ni sifa zipi zilizofanya bunge limpe uspika!
yule ni takataka tupu
 
Kwa hiyo Bwana Ndugai anatuona sote ni wabunge wa kuweza kutupangia nini cha kuzungumza dhidi bunge linaloketi Dodoma kwa kodi zetu? Mamlaka yake yanaishia kwa Wabunge tu. Kama bunge ni dhaifu litabaki kuwa hivyo; na katu ukali wake kwa wakosoaji wake hakulifanyi kuwa na nguvu.
Wabunge wenyewe akina Babu Tale!!!!!
 
Hii ni observation muhimu. Kitendo cha Ndugai kuhamaki maneno ya Jenerali mitandoni, basi ni ushahidi tosha kuwa wanashinda mitandaoni, wanasoma.

Kwahiyo tuandike sana, kumbe wanasoma, wanapata ujumbe kutoka kwa wananchi.

TUANDIKE SANA
 
Mkuu watu kama hawa ni wa kusamehewa tu. Kawaza tu lake kichwani kua Jenerali c mtanzania, akaliandika. Hajui historia ya jamaa na pengine hajui hata Jenerali Ulimwengu ni nani
Ulimwengu ni Mzalendo. Huyo hapo kulia kwenye harakati za ukombozi wa Africa akiwa na Hayati Samora Machel.
JamiiForums-1682061689.jpg
 
Kitendo cha bunge kulaumiwa na kila mmoja maana yake lina kiongozi dhaifu anayeshindwa kutekeleza majukumu yake ipasavyo, lakini badala yake ili kuficha udhaifu wake, kiongozi huyo huamua kutumia sheria zinazomlinda kwenye hiyo nafasi yake kuwashughulikia wanaomuonesha udhaifu wake, kwa namnaa hii tutegemee kuwa na bunge kibogoyo zaidi siku za mbeleni.
 
Ndugai amesikika wiki iliyopita akilalamika kuhusu serikali kepeleka miswada Tata ya Sheria àmbayo hajui Bunge linapitishaje? Yaani wewe mwenye nyumba unayeshika funguo hujui Nani kaingiza bangi chumbani kwako halafu ukielezwa wewe ni dhaifu ndo maana unachezewa na serikali unatishia watu?
 
Back
Top Bottom