Spika Ndugai: Nampa onyo kali Jenerali Ulimwengu kuchunga ulimi wake, haipendezi mtu wa umri wake kuwa anaongea ovyo ovyo

Mkuu kwani anaimiliki kihalali?

Tatizo lake ni lipi haswaa hadi aishi na hiyo mashine?
Huenda hujui unachokiuliza, wewe unaweza kumiliki mashine ya MRI nyumbani kwako peke yako kwa matumizi binafsi?

Kusafisha damu kwa mgonjwa wa figo ni mara mbili mpaka 3 kila wiki.
 
Muhimili wa Bunge unapaswa uheshimiwe, na ambaye anajaribu kuuvunjia heshima atachukuliwa hatua za kisheria.

kama anabisha arudie tena kutumia lugha za kashfa na kebehi kwa viongozi na mhimili alafu ataona tabu atakayo ipata.
huo ndi uzuzu wenu mkiambiwa ukweli unalalama, pumbafu
 
Huenda hujui unachokiuliza, wewe unaweza kumiliki mashine ya MRI nyumbani kwako peke yako kwa matumizi binafsi?

Kusafisha damu kwa mgonjwa wa figo ni mara mbili mpaka 3 kila wiki.
Wewe ni nani hadi ututajie magonjwa ya mtu?
 
Kwa wale tunaomfahamu Ulimwengu kama mfuasi na mwanafunzi mahili wa itikadi za Mwl. Julius Nyerere, Samora Machel na wanamapinduzi wa Cuba, Amerika kusini n.k. tunaamini hawezi kutishwa na yeyote anapo timiza haki yake ya kutoa maoni na kuelimisha umma. Anapokejeli dhana ya "waheshimiwa" hili neno lilishafutika ktk vocabularly na badala yake tukaitana "ndugu". Mengi anayozungumza na kuandika ndugu yetu Ulimwengu pengine yapo mbele ya wengi wetu kwa upeo na wakati. Badala ya kumtolea "onyo kali" ningeshauri bunge wamkaribishe Twaha Jenerali Ulimwengu kwa mjadala ambao naamini utaleta manufaa makubwa.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Tumia sheria ya uhamiaji kwa kurekebisha kakipengele kwenye uraia wa kuandikishwa
 
Ndugai wewe kwa Generally utasubiri sana sana, we unachojua ni kwamba Yesu alikuwa ni m-Yerusalemu na alimwoa Maria.
 
Mbona ndugai kamshukia jenerali kama mwewe baada ya jenerali kupiga kunako? au alikuwa na mpango wa kumlazimisha hangaya, atake asitake......
 
Hoja no. 4 unaweza kuitumia kufungua kesi ya kikatiba aisee. Mkuu points zako ni fikirishi sana
 
Wana JF, siku mbili hizi kumezuka mtifuano unaotishia amani kati ya Spika wa Bunge na Mwandishi mkongwe na mwanasiasa nguli tokea enzi za ukombozi wa Afrika pia Wakili wa mahakama kuu Jenerali Ulimwengu.
Hii ni baada ya kauli ya kitisho ya Spika Ndugai.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…