Spika Ndugai: Nampa onyo kali Jenerali Ulimwengu kuchunga ulimi wake, haipendezi mtu wa umri wake kuwa anaongea ovyo ovyo

Spika Ndugai: Nampa onyo kali Jenerali Ulimwengu kuchunga ulimi wake, haipendezi mtu wa umri wake kuwa anaongea ovyo ovyo

Basi baada ya kaulu hizo Ndugai ndipo alipo toa matishio yake ya hapo juu akiwa bungeni.
Lakini mwanaharakati mashuhuri Fatma Karume akaingilia kati na kumuonya Ndugai asilete za kuleta kwa kuandika yafuatayo:

Screenshot_20211112-080056_Instagram.jpg
 
Naye mbunge wa wananchi wa Tarime aliyeporwa ubunge wake katika uchafuzi wa 2020 John Heche akamkumbusha Ndugai juu ya aliyowahi kumwambia Bungeni kuhusu heshima ya bunge na watu wanavyoliona katika ukurasa wake wa Instagram

 
Wana JF, siku mbili hizi kumezuka mtifuano unaotishia amani kati ya Spika wa Bunge na Mwandishi mkongwe na mwanasiasa nguli tokea enzi za ukombozi wa Afrika pia Wakili wa mahakama kuu Jenerali Ulimwengu.
Hii ni baada ya kauli ya kitisho ya Spika Ndugai.View attachment 2007704
Unataka kulinganisha Mlima na kichuguu. Kichuguu tunakijua na Mlima ni upi.
 
Sisi wananchi tunashangazwa sana na ubabe wa kishamba unaofanywa kupitia mhimili wa Bunge letu. Ikumbukwe hili Bunge la sasa liliundwa kwa kukiuka taratibu nyingi sana kupitia kitu kinachofananishwa na Uchaguzi mkuu 2020

Tumemsikia Spika akitoa onyo kali dhidi ya Jenerali Ulimwengu kuwa wameishiwa uvumilivu.

1.
Spika anakiuka ibara ya 18 ya Katiba ya sasa

2.
Tangu uhuru mpaka leo, Bunge halijawahi kutunga sheria bali linapitisha miswada ya sheria zinazotungwa na Excutives. Ndo maana unasikia wabunge wanasema SERIKALI ILETE SHERIA BUNGENI ili waipitishe.

3.
Ndugai atupatie ushahidi lini Bunge liliwahi kuiwajibisha serikali kupitia ripoti ya CAG

4.
Je, kanuni za kudumu.za Bunge zilifuata utaratibu katika kutungwa na kupitishwa kwake? Kwa nini zinatumika kama sheria wakati hazijakidhi vigezo vya kuwa sheria?

5.
Bunge linatoa wapi mamlaka ya kutishia wananchi?

Bwana Ndugai, wananchi kwa sasa hawafuatilii sessions za Bunge. Haya ni matokeo ya kunajisi sheria za Uchaguzi na ukiukwaji wa maadili ya uongozi.

CCM tuna wakati mgumu sana 2025

Nipinge kwa hoja
Ndugai anajichulia kifo. Siku zake zinakaribia. Ngoma ikilia sana.
 
Back
Top Bottom