Spika Ndugai: Nampa onyo kali Jenerali Ulimwengu kuchunga ulimi wake, haipendezi mtu wa umri wake kuwa anaongea ovyo ovyo

Jenerali ni mtu mwelevu, na si aina ya watu wa kutishwa na hoja dhaifu.
Kama kuna sheria kavunja kwanini asichukuliwe hatua za kisheria?
Huu muhimili ni kiini macho tu, kuanzia MPs wengi walivyopatikana ni vigumu ukaheshimika.
 
Nimemsikiliza Twaha Halfan Ulimwengu hakuna baya. Sema Job anataka kuvalisha huu udhaifu wake kwa bunge zima kitu ambacho ni kosa.
 
Mbona waliosema Wabunge wanademka hakuwashugulikia?
Subfoofer ana ubaguzi wamatamko.
Aliwahi mwamri Mnyika akajifunze kwa Bashiru
 
Kwanini hupendwi kuguswa Ndugai. Wewe Mungu! Jana tu umetoa kauli ya kufoka kwa akina dada wakipewa madaraka, na wewe je ni Mdada?
 
Job Ndugai bado anaumwa
 
Ndugai ajitafakari na kujitathmini kwamba kwanini ktk kipindi chake ndiyo Bunge limezodolewa na watu wengi wenye akili kwamba ni dhaifu?

Badala ya Ndugai kutumia nguvu nyingi sana kupambana na wanaolizodoa bunge lake ni vema angerekebisha makosa yake na akasafisha taswira ya bunge.

Kila mfuatiliaji wa duru za Siasa na kazi za Bunge hapa nchini bunge limegeuka toilet paper ya serikali.

Baadhi ya waliowahi kukumbana na rungu la Ndugai kwa kulizodoa bunge ni pamoja na Prof. Assad na Pascal Mayalla . Na Sasa ameahidi kumshushia rungu Jenerali Ulimwengu.

Ndugai ashauriwe na akubali kuwa amelewa ili aache kuendelea kunywa pombe ya madaraka. Ni kweli bunge lake ni dhaifu.
 
Kwa kweli analiabisha Taasisi anayongoza, anajiabisha yeye mwenyewe, na wajumbe wengine wa Taasisi hiyo na wabongo wote kwa Jumla yetu, hata kwa Kiongozi wa Jamuhuri yetu. Kwa mojawapo ya Taasisi Nyeti kuwa kama Kiongozi wa taaluma yake
 
Umeskika ukitoa tambo za vitisho hapo bungeni leo dhidi ya mwana huyu wa Tanzania . Mzalendo asiyeimbwa. Kosa lake ni lipi tuambieni ili tumwambie.
Kosa lake ninini?
Bunge ni taasisi ya watu.
Wewe ni kibaraka wa wawatawala.
Utawatisha wangapi?
 
Bàada ya kumaliza mjadala wenu huko space na kina shangazi Maria mmekuja kumnanga spika wetu
 
Na sijui Israili anakwama wapi kwani kwa huyu amesharahisishiwa kazi yeye ni kufanya finishing tu.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] ila nyie watu jaman
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…