Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 128,308
- 245,426
Ametoa onyo hilo leo Mjini Dodoma na amemtaka Ulimwengu kuacha mara moja kutoa lugha za dharau dhidi ya Mhimili wa Bunge. Bali hakusema ni hatua gani atachukua ikiwa Jenerali Ulimwengu atakaidi onyo hilo, ila anasema watapambana naye ndani na nje.
----+
Akizungumza katikati ya mjadala wa Marekebisho ya Sheria mbalimbali uliowasilishwa Bungeni, Spika Ndugai amesema Ulimwengu ambaye ni Mwandishi wa Habari Nguli amekuwa akilikashfu Bunge na Spika apendavyo.
"Jenerali amekuwa akilivunjia heshima Bunge na Spika pia, napenda kumpa onyo kali kuchunga ulimi wake, haipendezi Mtu wa umri wake kuwa anaongea ovyoovyo, akiendelea na sisi tutaacha ukimya itabidi Watu washughulike naye ndani na nje yaani Mahakamani, habari imfikie uvumilivu wetu umefika mwisho, sisi sio kama anavyodhani" Spika Ndugai
“Huyu mzee hivi karibuni amekuwa akiropoka ropoka sana...” - Spika wa Bunge la Tanzania Job Ndugai, akitoa onyo aliloliita la mwisho kwa mwanahabari nguli Jenerali Ulimwengu na kumtaka kuacha tabia ya kukashfu watu na kuzivunjia heshima taasisi mbalimbali na kulidharau Bunge.
Pia soma: Uzee dawa: Msikilize Jenerali Ulimwengu