Dickson Edwin Mgaya
JF-Expert Member
- Apr 2, 2020
- 513
- 1,422
Mbeleko imekatoboka mzee, kuna watu watalimia meno round hii!! Hakuna undugu, ukabila, utani wala ukanda hapa
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hao watakuwa MaCCM wenzake.Manake upinzani walishajikatia tamaa na Jiwe kupata zuri lolote kutoka kwake.Ndio maana wenye mioyo miepesi walianza kuunga mkono juhudi! 🤣Kauli ya Spika wa Job Ndugui hii leo inaonesha haamini utawala wa sasa.
Amesema " Wanaofurahia kifo cha Mkulima wa mahindi wamesahau mwakani hawana pakula?
Tumemla kibogaWametafuna nini?
Siasa mpaka kwenye misiba!Hii kauli ya Spika wa bunge mh Ndugai inafikirisha sana...
Hata wewe zamu yako iko karibuNaye zamu yake itafika ni muda tu!
Hata km mkulima angekuwepo wasingekula mahindi hayo!Hii kauli ya Spika wa bunge mh Ndugai inafikirisha sana...
Sisi Nyani na wenzetu wa jamii kama zetu Tumbili, Sokwe, Kima, Gendaheka tunamuombea Bw. Subwoofer nae Mungu ampende zaidi haraka iwezekanavyo ili somo lieleweke vizuri.Hii kauli ya Spika wa bunge mh Ndugai inafikirisha sana...
Tena basi umenikumbusha uongozi wa waislamu wote na wasabato hatukomagi sana no misukosuko mingi!! Wakristo wenzangu tupate fundisho hapa.Waislam wengi ni watu waungwana sana (though mimi sio Muslim). Kwenye hotuba ya Speaker wa baraza la wawakilishi na yule mbunge (mwislam) aliyeenda kusoma dua wamemeombea Hayati Magufuli msamaha kwa kuwa wanatambua kuwa Magufuli alikuwa binadamu hivyo kuna watu aliwakosea. Hawa wa kwetu wameanza kuita wenzao manyani. Inasikitisha sana.
Khaaaa nimecheka hatari... Wewe mtu wa kamnyonge na majita makojo umeandika nn? Hiyo fibrillation hiyo sasaTena basi umenikumbusha uongozi wa waislamu wote na wasabato hatukomagi sana.no misukosuko mingi!! Wakristo wenzangu tupate fundisho hapa...
Mtu akitoa naomi tofauti na yako anaitwa nyaniNyani wapo wengi, kuwataja wachache
1. Tundu lissu
2. Fatma karume
3. Binti wa sarungi
4. Zitto kabwe
5. Na genge lao lote na bavicha maji...
Kama ajajenga au alichukua mkopo Mkubwa ndo imekula kwake hata alie kilio cha mbwa mbuzi.Gambo na Hapi angalau walianza kurudi nyuma.Duh, hadi adande sele😀😀😀
Inkulu dawa kana bubaa!!!Mwanachuma gani ni mdodo...
Nawewe pia zamu yako itafika ni muda tuu!Naye zamu yake itafika ni muda tu!
Yani kajisema mwenyewe kua yeye nyani ndio mana wahindi walimpunguza vidole,akirudi india wanapunguza zaga na kengele zake,mungu fundiHii kauli ya Spika wa bunge mh Ndugai inafikirisha sana.
Hao nyani wanaofurahia kifo cha hayati Magufuli ni akina nani?
Je, ni Ufipa?
Na kwanini mwakani watakosa chakula?
Hata hivyo Ndugai amesema wanaoshangilia wanajidanganya Tanzania haitarejea kuwa shamba la bibi kamwe.
Maendeleo hayana vyama!
========================
SPIKA wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai, amewashukia watu wanaofurahia kifo cha aliyekuwa Rais wa Tanzania, Hayati John Magufuli (61), kilichotokea Jumatano ya tarehe 17 Machi 2021.
Kiongozi huyo wa mhimili wa bunge, amewashukia watu hao leo Jumatatu tarehe 22 Machi 2021, wakati mwili wa Hayati Rais Magufuli ukiagwa na wabunge kwenye viwanja vya bunge jijini Dodoma.
Hayati Magufuli amefariki dunia katika Hospitali ya Mzena, mkoani Dar es Salaam, alikokuwa anapatiwa matibabu ya matatizo ya mfumo wa umeme wa moyo.
Akizungumzia kifo hicho, Spika Ndugai amewafananisha watu hao na nyani waliofurahia kifo cha mwenye shamba la mahindi, ambaye alikuwa anawazuia kula mahindi yake.
“Sasa iko hadithi ya wale nyani walioshambulia shamba la mkulima kwenye mahindi, wakifurahi sana mahindi yanapokuwa yanaiva wanavuna wanakula, walipopata habari mwenye shamba amefariki wale nyani walifurahi sana.”
“Naamini katika nchi yetu manyani wa namna hii hawakosekani, lakini wakasahau mwaka uliofika wakati mahindi kuiva wakarudi shambani kula mahindi wakasahau mwenye shamba alifariki mwaka jana wakawa wanasikitika,” amesimulia Spika Ndugai.
Spika Ndugai ameshauri Watanzania, wasiwe kama ngedere hao kwa kutofanya mambo mabaya ambayo hayati Rais Magufuli aliyakataza.