Spika Ndugai: Nyani wanashangilia kifo cha mkulima wa mahindi wanasahau mwakani hawana pa kula

Nyani atakuwa Tundu Lissu na genge lake la wapigaji
 
Kauli kama hizi hazijengi, wala hazitakiwi kutoka kwenye kinywa cha mtu kama Spika wa Bunge. Binafsi sipendi watanzania wengi ambavyo wameonesha hisia chanya juu ya msiba wa Raisi Magufuli, japo ukitazama kwa undani utafahamu kweli wengi waliumizwa sana (Japo kiuungwana hili halihalalishi watu kushangilia).

Katika mtazamo wa uhalisia, ndani ya miaka mitano iliyopita watu walinyamazishwa kwa nguvu ya dola, sasa huu ndiyo wakati muafaka wanatumia kuyatoa ya moyoni (Venting out anger and frustrations). Hivyo ni heri uwaache waongee wee mwishoni yataisha na watanyamaza na kujirudi. Ukitaka kuwazuia watu wasiseme huku mwenyewe Spika ulikuwa ni sehemu ya tatizo nadhani mtajenga chuki kubwa sana na kumponza hata Raisi mpya.

Tanzania ni yetu sote, hili nalo japo linaumiza lakini litapita na mambo yatakaa sana.
Tuache propaganda za kipumbavu zinazoligawa taifa na tusonge mbele.
 
Bahati mbaya hayo yaliweza fanya kazi, under 1 man show, tuulizane ametuachia mfumo dhabiti wa kuendeleza haya??

Miaka 5-10 ijayo, hii generation hapa inakuwa imedhulumika, wengi wamesoma kwa mikopo ambayo HESLB haijali wana vipato au hawana inawapiga penalty.
Unahalalishaje hawa kupoteza gap la maisha, in the meantime ndugu, rafiki, watoto wa vigogo hawajawahi kukosa kazi!

Nazidi kusema ku-terrorize the mass, kuwa demoralize kama hawa graduates wasio na ajira wala vipato huku wakiambiwa wajiajiri na vigogo walio kwenye maviete kama wabunge wanaojilipa milumbesa, na kuhakikisha wamatumbi they remain poor, na waaamini wao ni wanyonge ili kazi ya kuwatawala na siyo kuwaongoza iwe rahisi.
Ndiyo maana nasema wale waliozaliwa kwenye asali na maziwa hawawezi kuelewa kilio chetu wanyonge wa kweli siyo wale waliokuwa wanasimama kwenye majukwaa. Wakati wa ziara na kupewa mil5 wakilalamika nyungo zao zimebebwa na mgambo wa jiji.

Demoralize, terrorize and make sure they are poor enough to believe u their savior not their ruler.
Psychological!

Everyday is Saturday............................... 😎
 
Huyu jamaa akili yake ina walakini sana.....

Moja, je leo ni siku muafaka ya kuanza kuzebezana na kuvutana na kuleta kebehi ?

Mbili, Yaani Nchi na Taasisi zote zinamtegemea mtu mmoja, kwamba yeye akiondoka kila kitu kinasimama ? (kama ndivyo wote watoke huko pamoja na yeye tutafute mtu mmoja / mkulima sababu inaonyesha hao wengine wote waliopo hawawezi kazi...

Haya ya watu wengine kufurahia ni kazi nzuri / mbaya iliyofanywa na Awamu ya Tano ya Kuwatenga watu badala ya kuwaunganisha (hakuna sababu ya kuendelea kuonyesha utofauti hususan wakati huu ambapo nchi imeingia kwenye tafrani ambayo haijawahi kuingia) Huyu mtu asiye na busara anaendelea kuongeza ufa wa mshikamano... (Bure Kabisa...)
 
Ni imani tu mkuu. Wakristo wana amini kuwa kila nafsi ni huru, ndiyo maana wanabatiza ili unapofanya dhambi, wakiamini kuwa kila nafsi ina dhambi, unatubu mwenyewe. Na unatubu ukiwa hai. Kwa hiyo hayati rais alitakiwa awe ameshatubu dhambi zake alipokuwa hai wakristo wengine wanamuombea tu raha ya milele.
 
Kwenye kuendeleza kusimamia haki mwenye macho aambiwi tazama, viongozi wote wameona vilio vya wananchi wanyonge nani atawatetea tena.

Kwenye uchumi nadhani umeshakutana na msemo ‘Rome wasn’t built in a day’.

Sometimes sacrifices za leo ni lazima kwa faida ya kizazi kijacho. Watu waliojenga canals nchi za wenzetu, njia za train za juu na underground; na infrastructure zingine engineers walioshiriki kwenye main designing kwa umri wao wengi waliona mwanzo tu wa projects zenyewe.

Hii miradi ya leo ndio itamfanya mtu alie Arusha miaka ijayo badala kufikiria uwekezaji ni kwenye sector ya utalii tu; kuna opportunity ya kuleta alizeti kutoka Shinyanga mpaka Arusha na train na kukamua mafuta huku aki target soko la kaskazini na nchi jirani.

Watu wanafikiria kutokana na fursa zilizopo, uwezi kufikiria kujenga kiwanda cha kuongeza thamani ya maharage (tin packaging) Tanga wakati hujui utayotoa vipi kutoka mbeya. Lakini ukishawawekea wanatanga access ya barabara au train wanaweza kufikiria hizo possibilities ndio uchumi unavyokua.

Serikali aiwezi kusema iache kutoa elimu kisa inazalisha wasomi kushinda uwezo wa soko kuajiri, hiyo itakuwa ni kuwanyima raia wengine haki zao za msingi. Kwa sasa ni jukumu la wahitimu kuwa wabunifu.

Kupata kwao ajira baada ya kumaliza masomo sio jukumu la serikali, kazi ya serikali ni kuweka mazingira ya kuvutia uwekezaji zaidi ili ajira zizalishwe ndio alichokuwa anajaribu kuwafanyia Magufuli.

Umeshawai kuisikia hii hadithi ya ‘Walt Disney’, alifariki miezi michache kabla ya theme park yake ya kwanza kufunguliwa.

Siku ya uzinduzi mdogo wake akaulizwa “it’s a shame, Walt isn’t here to witness the opening” jibu lake lilikuwa lifuatalo “not at all, he saw all of this first in his head before any of us”. Ndio baadae mtakavyokuja kumuelewa Magufuli investment zikianza kuleta faida.
 
..
..shamba siyo la mtu, ni la "manyani wote" mwakani hakuna shaka ya chakula kwani haliko wazi hadi sasa. Yupo nyani mteule na tayari kaanza kutia mbegu shambani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…