Spika Ndugai: Rais Samia ametuandalia futari Wabunge na Wafanyakazi wote wa Bunge siku ya Alhamisi 22/04/2021

19 March 2021

TLS Yatoa Mwongozo Uundwaji wa Serikali Mpya, Baada ya Kuapishwa Rais Samia Suluhu​

Source : Wakili TV
 
Sasa mkubwa unanitafuta ugomvi, hivi mimi nafaa kukaa meza moja na hao waheshimiwa hapo chini!! ha ha ha h

Kama kuna ushahidi wa jinsi gani Mwendazake alivuruga utamaduni , mila na desturi zetu ni hili la hotuba.

Ilikuwa kama taboo kwa viongozi wa nchi kutoa hotuba zao katika nyumba za ibada.

Mwendazake alitumia makanisa kueleza mambo ya kitaifa. Hili tu lilitosha kuligawa Taifa

Ukizingatia teuzi zake ziliwatupa hazikujali uwiano wa dini kuna kila sababu ya kuamini alikuwa mdini sana

Namshauri sana Mh Rais Samia akemee viongozi kutumia nyumba za dini kama alivyoanza VP
 
Vunja bunge, tuone nani atarudi. Na sis tutafutarishwa lini?
 
Angalieni futari hiyo isijegeuka vilio bungeni, si mnajua mama ni mtaalamu wa lugha?
 
Kutumia nyumba za ibada kwa mambo ya kisiasa hakuepukiki ustaadh!
 
Hivi maana ya huu msemo ni nini?
Msemo huu ni zao la unyumbuaji wa neno Dema - yaani tembea taratibu kama mtoto anaejifunza kutembea au chopeachopea - pepesuka hivi... Kwenye uchezaji ngoma kunahali ya kucheza kwa madaha unadem.eka nadhani umeelewa.
 
Mmh
 
Gharama za hizi futari huwa analipa kwa mshahara wake au kwa salio Ikulu?
Kama kwa mshahara wake anapata thawabu.
Kama kwa tozo za serikali basi I we inasomeka Ikulu/Serikali imeandaa futari.
 
Gharama za hizi futari huwa analipa kwa mshahara wake au kwa salio Ikulu?
Kama kwa mshahara wake anapata thawabu.
Kama kwa tozo za serikali basi I we inasomeka Ikulu/Serikali imeandaa futari.
Absolutely true
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…