Spika Ndugai: Rais Samia naomba unisamehe kwa sintofahamu iliyotokana na kauli yangu🙏

Aibu sana kula mata....!!! Hakuna cha kutengenezwa umeongea waaazi na ikaeleweka!!!
MTU anajidai anajua kucheza na siasa eti wamekatakata????
Watz sio malofa!
Haifai mtu waakili hii kuongoza mjengo ndomana anaruhusu mamp wasio navyama!
AIBU,AIBU,AIBUUUU KAMA TAIFA NIAIBU TAASISI KUUUBWA,MUHIMU NA NYETI KUONGOZWA NA HUYU MTU.
Nabado tunaomba Mungu uvurugikiwe na uharibu kazi yaani tunakuombea mabalaa kazini yakuandame maana ulifanyia watu hila mbaya sana!! Mizimu ya ulowaumiza ikuandame mwanzo mwisho.
 
Hivi Nduguyo ni mgogo
Baada ya matamko kutoka viongozi mbalimbali wa Chama Cha Mapinduzi na serikali dhidi ya kauli ya Spika Job Ndugai kuhusu mikopo, leo Jumatatu saa 5:00 asubuhi, Ndugai anazungumza na waandishi wa habari, jijini Dodoma.

NDUGAI: NIMEUMIA KUOENEKANA NAPINGA MKOPO WA SERIKALI WA TSH. TRILIONI 1.3

Spika Job Ndugai amesema kauli yake aliyoitoa Desemba 26, 2021 alipoalikwa kwenye tukio la makumbusho ya wagogo kuwa imechukuliwa vibaya na kuleta mkanganyiko

Amesema alikuwa anazungumza kuhusu sababu iliyoifanya bunge kukubali na kuipitisha tozo na sio kuwa alikuwa akizungumzia taasisi nyingine yoyote

Ndugai amesema video iliyosambaa ilikatwa bila kuleta ujumbe kamili aliokuwa amekusudia. Ameumia kuonekana anapinga mkopo wa serikali

NDUGAI: TUTENGENEZE MAKUMBUSHO YA BUNGE

Spika wa Bunge Job Ndugai, amesema ni muhimu kwa Bunge kuwa na makumbusho yake ili wanaotembelea ofisi hizo wajue historia ya bunge kwa namna ilivyokuwa

Jambo hilo amesema ni muhimu hata kwa taasisi nyingine kuwa na makumbusho yake ili watu waweze kujua kuhusu historia ya taasisi husika

Amesema hayo alipokuwa anaongea na waandishi wa habari ofisi za Bunge Dodoma

NDUGAI: NAMUOMBA RADHI RAIS NA WANANCHI WOTE

Spika wa Bunge Job Ndugai amemuomba radhi Rais Samia Suluhu na wananchi wote kwa sintofahamu iliyotokana na kauli yake

Amesema yeye ni CCM ambao lengo lao ni moja hawawezi kutofautiana. Kuna watu wanaojaribu kuwafarakanisha lakini hawatafanikiwa

Ndugai amesema Rais anafanya vizuri lakini peke yake hawezi kwa hiyo ni jukumu la watu wote kumsaidia
View attachment 2066990
View attachment 2067070
Pia soma;
Job Ndugai: Ipo siku Tanzania itapigwa mnada, Watu tukishakopa tunapiga makofi kujipongeza. Deni la Taifa ni 70 Trilioni
 
Siajiuzulu akajiajiri aachie wengine nao wafaidi huo mshahara au anaogopa kufa njaa!!
Profesa Assad ndio alionesha uanaume na utimamu.
Prof. Kirengased aliwahi sema mgonjwa waakili ndiyo hula matapishi yake mtu timamu hawezi!!
 
Ukishaona speaker wa Bunge ambae ni mhimili wa dola unaojitegemea ametoa msimamo wake juu ya jambo fulani halafu ghafla akamuomba msamaha Rais kwa msimamo aliotoa, jua hilo Taifa limefika mwisho na limekufa.

Kwenye hili mtu asipoona tena umuhimu wa katiba mpya basi huyo mtu ni maiti inayotembea.
 
Nampongeza spika kwa kuomba msamaha badala ya utamaduni wa kulaumu. Hii ni hatua nzuri hasa kwa wale viongozi wenyewe upungufu wa kuwa na hasira za haraka kama spika. Badala ya kukuza hili jambo tulimalize

Spika kukosoa ni muhimu lakini huu ni mkopo mzuri sana miaka 20 bila riba!. Mkopo mbaya ni ule wa treni $1.5 B kwa miaka 6 na riba ya 8% huu sio mkopo mzuri kabisa. Muda sio mzuri lakini riba ingetakiwa isizidi 5% .
 
Dawa ya meno kubwa ni sh 4000 kwa sasa kutoka sh 3000.

Hatujui tunaenda wapi wakubwa...
 
Hahaaaa !!!hapana chezea mhimili uliojichimbia chin zaid.
Huwa nikiona mihimili ya Kenya ikifanya kazi mpaka raha
Kiongozi wa CCM akiwa nje ya mfumo ni mwepesi kuliko karatasi laini ya chooni.
Rejea Kina Mzee Kinana,Mzee Makamba walivyohenyeshwa na Sukuma Gang,na sasa kina Polepole na Bashiru ni kama watoto yatima.
Ndungai aliliona Hilo akarudi kusujudu mapema asamehewe.Alivyokuwa anatubu ni kama vile alikuwa mbele ya baba paroko!
 
ndugai wala hajaomba msamaha bali kacheza na akili za watu tu, muda ni mwalimu mzuri utajibu.
 
Nampongeza spika kwa kuomba msamaha badala ya utamaduni wa kulaumu. Hii ni hatua nzuri hasa kwa wale viongozi wenyewe upungufu wa kuwa na hasira za haraka kama spika. Badala ya kukuza hili jambo tulimalize

Spika kukosoa ni muhimu lakini huu ni mkopo mzuri sana miaka 20 bila riba!. Mkopo mbaya ni ule wa treni $1.5 B kwa miaka 6 na riba ya 8% huu sio mkopo mzuri kabisa. Muda sio mzuri lakini riba ingetakiwa isizidi 5% .
Wewe ni mpuuzi kweli kweli. Kwa taarifa yako ni kuwa kafanya kosa kubwa sana la kiufundi na hili litauchafua sana mhimili wa bunge.
 
Baada ya matamko kutoka viongozi mbalimbali wa Chama Cha Mapinduzi na serikali dhidi ya kauli ya Spika Job Ndugai kuhusu mikopo, leo Jumatatu saa 5:00 asubuhi, Ndugai anazungumza na waandishi wa habari, jijini Dodoma.

NDUGAI: NIMEUMIA KUOENEKANA NAPINGA MKOPO WA SERIKALI WA TSH. TRILIONI 1.3

Spika Job Ndugai amesema kauli yake aliyoitoa Desemba 26, 2021 alipoalikwa kwenye tukio la makumbusho ya wagogo kuwa imechukuliwa vibaya na kuleta mkanganyiko

Amesema alikuwa anazungumza kuhusu sababu iliyoifanya bunge kukubali na kuipitisha tozo na sio kuwa alikuwa akizungumzia taasisi nyingine yoyote

Ndugai amesema video iliyosambaa ilikatwa bila kuleta ujumbe kamili aliokuwa amekusudia. Ameumia kuonekana anapinga mkopo wa serikali

NDUGAI: TUTENGENEZE MAKUMBUSHO YA BUNGE

Spika wa Bunge Job Ndugai, amesema ni muhimu kwa Bunge kuwa na makumbusho yake ili wanaotembelea ofisi hizo wajue historia ya bunge kwa namna ilivyokuwa

Jambo hilo amesema ni muhimu hata kwa taasisi nyingine kuwa na makumbusho yake ili watu waweze kujua kuhusu historia ya taasisi husika

Amesema hayo alipokuwa anaongea na waandishi wa habari ofisi za Bunge Dodoma

NDUGAI: NAMUOMBA RADHI RAIS NA WANANCHI WOTE

Spika wa Bunge Job Ndugai amemuomba radhi Rais Samia Suluhu na wananchi wote kwa sintofahamu iliyotokana na kauli yake

Amesema yeye ni CCM ambao lengo lao ni moja hawawezi kutofautiana. Kuna watu wanaojaribu kuwafarakanisha lakini hawatafanikiwa

Ndugai amesema Rais anafanya vizuri lakini peke yake hawezi kwa hiyo ni jukumu la watu wote kumsaidia
View attachment 2066990
View attachment 2067070
Pia soma;
Job Ndugai: Ipo siku Tanzania itapigwa mnada, Watu tukishakopa tunapiga makofi kujipongeza. Deni la Taifa ni 70 Trilioni
Kuna watu walikuwa wakituma meseji usiku wa manane kuomba msamaha,wengine walipiga magoti ikulu mbele ya JPM.Kuna wazee wa chama Kinana,Makamba baba na mwana,Nape hawa waulize walionja cha Moto.Tanzania ukiwa rais Ni kila kitu ht ukiwa na ukweli rais haguswi.Sasa Ni zamu ya Ndugai.
 
Back
Top Bottom