kirengased
JF-Expert Member
- Jan 10, 2016
- 6,348
- 7,058
Baada ya matamko kutoka viongozi mbalimbali wa Chama Cha Mapinduzi na serikali dhidi ya kauli ya Spika Job Ndugai kuhusu mikopo, leo Jumatatu saa 5:00 asubuhi, Ndugai anazungumza na waandishi wa habari, jijini Dodoma.
NDUGAI: NIMEUMIA KUOENEKANA NAPINGA MKOPO WA SERIKALI WA TSH. TRILIONI 1.3
Spika Job Ndugai amesema kauli yake aliyoitoa Desemba 26, 2021 alipoalikwa kwenye tukio la makumbusho ya wagogo kuwa imechukuliwa vibaya na kuleta mkanganyiko
Amesema alikuwa anazungumza kuhusu sababu iliyoifanya bunge kukubali na kuipitisha tozo na sio kuwa alikuwa akizungumzia taasisi nyingine yoyote
Ndugai amesema video iliyosambaa ilikatwa bila kuleta ujumbe kamili aliokuwa amekusudia. Ameumia kuonekana anapinga mkopo wa serikali
NDUGAI: TUTENGENEZE MAKUMBUSHO YA BUNGE
Spika wa Bunge Job Ndugai, amesema ni muhimu kwa Bunge kuwa na makumbusho yake ili wanaotembelea ofisi hizo wajue historia ya bunge kwa namna ilivyokuwa
Jambo hilo amesema ni muhimu hata kwa taasisi nyingine kuwa na makumbusho yake ili watu waweze kujua kuhusu historia ya taasisi husika
Amesema hayo alipokuwa anaongea na waandishi wa habari ofisi za Bunge Dodoma
NDUGAI: NAMUOMBA RADHI RAIS NA WANANCHI WOTE
Spika wa Bunge Job Ndugai amemuomba radhi Rais Samia Suluhu na wananchi wote kwa sintofahamu iliyotokana na kauli yake
Amesema yeye ni CCM ambao lengo lao ni moja hawawezi kutofautiana. Kuna watu wanaojaribu kuwafarakanisha lakini hawatafanikiwa
Ndugai amesema Rais anafanya vizuri lakini peke yake hawezi kwa hiyo ni jukumu la watu wote kumsaidia
View attachment 2066990
View attachment 2067070
Pia soma;
Job Ndugai: Ipo siku Tanzania itapigwa mnada, Watu tukishakopa tunapiga makofi kujipongeza. Deni la Taifa ni 70 Trilioni
Hata huyu atatulizwa tu sooner than you may know it
Hili la kuweka makumbusho ya bunge namuunga mkono. Tuweke kumbukumbu kwa vizazi vijavyo kwamba tuliwahi kuwa na bunge la ovyo likiongozwa na Zuzu mmoja aitwaye Ndugai.
Kiongozi wa CCM akiwa nje ya mfumo ni mwepesi kuliko karatasi laini ya chooni.
Rejea Kina Mzee Kinana,Mzee Makamba walivyohenyeshwa na Sukuma Gang,na sasa kina Polepole na Bashiru ni kama watoto yatima.
Ndungai aliliona Hilo akarudi kusujudu mapema asamehewe.Alivyokuwa anatubu ni kama vile alikuwa mbele ya baba paroko!
Nyama ya ng'ombe 9000 kutoka 7000Dawa ya meno kubwa ni sh 4000 kwa sasa kutoka sh 3000.
Hatujui tunaenda wapi wakubwa...
mtungi wa gesi mdogo 23,000 kutoka 20,000Nyama ya ng'ombe 9000 kutoka 7000
Wapi mwanaharakati huru.... hahaha anasema mm huwa situmwi na mtu yeyote ( in the voice of musiba)Haha haha
Wewe ni mpuuzi kweli kweli. Kwa taarifa yako ni kuwa kafanya kosa kubwa sana la kiufundi na hili litauchafua sana mhimili wa bunge.Nampongeza spika kwa kuomba msamaha badala ya utamaduni wa kulaumu. Hii ni hatua nzuri hasa kwa wale viongozi wenyewe upungufu wa kuwa na hasira za haraka kama spika. Badala ya kukuza hili jambo tulimalize
Spika kukosoa ni muhimu lakini huu ni mkopo mzuri sana miaka 20 bila riba!. Mkopo mbaya ni ule wa treni $1.5 B kwa miaka 6 na riba ya 8% huu sio mkopo mzuri kabisa. Muda sio mzuri lakini riba ingetakiwa isizidi 5% .
Kuna watu walikuwa wakituma meseji usiku wa manane kuomba msamaha,wengine walipiga magoti ikulu mbele ya JPM.Kuna wazee wa chama Kinana,Makamba baba na mwana,Nape hawa waulize walionja cha Moto.Tanzania ukiwa rais Ni kila kitu ht ukiwa na ukweli rais haguswi.Sasa Ni zamu ya Ndugai.Baada ya matamko kutoka viongozi mbalimbali wa Chama Cha Mapinduzi na serikali dhidi ya kauli ya Spika Job Ndugai kuhusu mikopo, leo Jumatatu saa 5:00 asubuhi, Ndugai anazungumza na waandishi wa habari, jijini Dodoma.
NDUGAI: NIMEUMIA KUOENEKANA NAPINGA MKOPO WA SERIKALI WA TSH. TRILIONI 1.3
Spika Job Ndugai amesema kauli yake aliyoitoa Desemba 26, 2021 alipoalikwa kwenye tukio la makumbusho ya wagogo kuwa imechukuliwa vibaya na kuleta mkanganyiko
Amesema alikuwa anazungumza kuhusu sababu iliyoifanya bunge kukubali na kuipitisha tozo na sio kuwa alikuwa akizungumzia taasisi nyingine yoyote
Ndugai amesema video iliyosambaa ilikatwa bila kuleta ujumbe kamili aliokuwa amekusudia. Ameumia kuonekana anapinga mkopo wa serikali
NDUGAI: TUTENGENEZE MAKUMBUSHO YA BUNGE
Spika wa Bunge Job Ndugai, amesema ni muhimu kwa Bunge kuwa na makumbusho yake ili wanaotembelea ofisi hizo wajue historia ya bunge kwa namna ilivyokuwa
Jambo hilo amesema ni muhimu hata kwa taasisi nyingine kuwa na makumbusho yake ili watu waweze kujua kuhusu historia ya taasisi husika
Amesema hayo alipokuwa anaongea na waandishi wa habari ofisi za Bunge Dodoma
NDUGAI: NAMUOMBA RADHI RAIS NA WANANCHI WOTE
Spika wa Bunge Job Ndugai amemuomba radhi Rais Samia Suluhu na wananchi wote kwa sintofahamu iliyotokana na kauli yake
Amesema yeye ni CCM ambao lengo lao ni moja hawawezi kutofautiana. Kuna watu wanaojaribu kuwafarakanisha lakini hawatafanikiwa
Ndugai amesema Rais anafanya vizuri lakini peke yake hawezi kwa hiyo ni jukumu la watu wote kumsaidia
View attachment 2066990
View attachment 2067070
Pia soma;
Job Ndugai: Ipo siku Tanzania itapigwa mnada, Watu tukishakopa tunapiga makofi kujipongeza. Deni la Taifa ni 70 Trilioni
In other words he is contrite, remorseful, ashamed, shame faced, abject.Speaker has spoken in a penitent tone!