Spika Ndugai: TAMISEMI inaniudhi sana; kwanini inapora Madaraka ya Halmashauri?

Spika Ndugai: TAMISEMI inaniudhi sana; kwanini inapora Madaraka ya Halmashauri?

Aiseeeeh,
Huyu naye akili imeanza kumrudia..

Nini kimempata au ametokewa na mtume au nabii!?

Maana, tangia awe mbunge na kiongozi wa mjengoni naona hizi ndiyo points na hoja za kwanza kabisa ameiziongea.
 
Akili zake zimeanza kumrudia taratibu

popoma ,
Mkuu
Binafsi, hadi nimeogopa maana , isijekuwa ametokewa na vya kutokewa hadi akili zimemrudia kiasi hiki.

Tangia, awe madarakani hizi ndiyo points mbili (2) ameongea.

Eeeh, mola rejesha akili za wengine pia.
 
popoma ,
Mkuu
Binafsi, hadi nimeogopa maana , isijekuwa ametokewa na vya kutokewa hadi akili zimemrudia kiasi hiki.

Tangia, awe madarakani hizi ndiyo points mbili (2) ameongea.

Eeeh, mola rejesha akili za wengine pia.
CCM KUNA KANUNI ZINARUHUSU KUSEMA KWELI DAIMA, SASA SIJUI KAMA VYAMA VINGINE KUNA HILO JAMBO. Maana sijawahi wasikia nyumba ya jirani wakiongea mapungufu yao hadharani, hila utasikia tu huyu jamaa ni msaliti ,ha ha ha
 
hii sidhani kama ni sahihi kuiterm kama ajira bali ni replacement ya watumishi (walimu) ambao walitumbuliwa thus allocation ni kule kwenye magap yaliyoachwa (though minor alteration might be made)
 
Ilo la upande wa walimu kwa mm naona tamisemi hapo sawa,,mana mfumo wa kupangiwa wilayani ulikuwa na ukilitimba mkubwa jamani tena sana,,unakuta shule zingine zina wlimu kibao shule za ndani kama ya huyo sipka walimu 4 vpindi kibao,mshahara ule ule lakini mzigo mnaokula hatr,,unakutana na mwalimu anakwambia ana vipindi 6 kwa wiki harfu wee una vipindi 45 kwa wiki,,tatizo wapi kwenye upangaji wa ajila mpya,,utasikia kuna kijana wangu hapo muweke barabarani sasa makolongoni akae nani???[emoji35] [emoji35] [emoji35]
 
HALMASHAURI kwa Madiwani!?!, hapana kwa kweli bora ibaki huko huko wizarini
 
CCM KUNA KANUNI ZINARUHUSU KUSEMA KWELI DAIMA, SASA SIJUI KAMA VYAMA VINGINE KUNA HILO JAMBO. Maana sijawahi wasikia nyumba ya jirani wakiongea mapungufu yao hadharani, hila utasikia tu huyu jamaa ni msaliti ,ha ha ha

baruti 1
Mkuu,
You're making "makosa ya kimkakati" jiangalie sana uandikavyo...
Nape ameambiwaje baada ya kukosoa sana serikali yake ya CCM!?
 
Tamisemi wana mfumo wa takwimu za shule zote kutoka halmashauri unaitwa 'BEMIS' basic Education managemebt information System..ambao kila mwaka halmashauri hujaza takwimu za shule zotee nchin na kuzituma tamisemi, hivyo tamisemi wanajua kila shule Tanzania ina walimu wangapi na mahitaji kiasi gani, mfumo huo hujazwa kila kitu hadi idadi za wanafunzi walemavu, watoro, idadi ya vitabu vilivyopo na upungufu kwa kila shule nchini..hivyo tamisemi wao wanajua wapi pana upungufu katika halmashauri, ..
 
Afadhali angalau na yeye imuudhi.kidogo kama anavyotufanyia, huko kongws kuna ombwe la viongozi
Dodoma. Spika wa Bunge, Job Ndugai amepinga mpango wa Serikali wa kuwapangia vituo vya kazi moja kwa moja walimu wanaoajiriwa, akihoji ni kwanini inapoka madaraka ya Halmashauri.

Ndugai ametoa kauli hiyo leo Jumamosi Desemba 23, 2017 ikiwa ni siku moja baada Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Selemani Jafo kutangaza majina ya walimu 3,033 waliopangiwa vituo vya kazi.

Katika kikao cha kamati ya ushauri ya Mkoa wa Dodoma leo, Spika Ndugai amehoji TAMISEMI ni nani hata aweze kujua ikama ya walimu shuleni. Amesema wamekuwa wakijaza walimu maeneo yasiyo na mahitaji.

"Hili jambo linakera, yaani kila mahali sasa ni TAMISEMI hadi napata shaka sasa, hivi hii zana ya D by D (ugatuaji wa madaraka) ina maana haijatafsiriwa vyema au ndiyo kupoka madaraka kwa wengine," alihoji Ndugai.

Spika ametoa mfano wa Shule ya Banyibanyi wilayani Kongwa ambayo amesema ina wanafunzi wanaoingia kidato cha tatu lakini hawajawahi kusoma masomo ya sayansi hata siku moja.

"Lakini juzi hapa mmepanga walimu na nilipita tena hapo hakuna hata mwalimu. Hawajasoma hesabu, fizikia, baiolojia, kemia na jiografia; nauliza tena wanasema Tamisemi, hivi hao walisoma wapi na ninyi mmesoma shule zipi," alihoji.

Ndugai amewatupia mzigo wabunge wa Mkoa wa Dodoma amesema wanatakiwa kuupinga mpango huo bungeni wakati yeye akiongoza vikao vya Bunge.

Pia, amepinga mpango wa utoaji fedha kwa vikundi amesema umepitwa na wakati kwa kuwa zinaliwa bure.

Amesema hakuna umuhimu wa kusema watu waunde vikundi ndipo wapewe fedha au uwezeshwaji, badala yake waangaliwe mtu mmoja mmoja ambao wanakuwa na uwezo wa kuzalisha na kisha wafuatiliwe.

Mbunge wa Mtera, Livingstone Lusinde na Meya wa Manispaa ya Dodoma, Profesa Davis Mwamfupe kwa nyakati tofauti waliunga mkono hoja ya kutopeleka fedha kwa vikundi.

Lusinde amesema kumekuwa na utitiri wa vikundi baada ya kusikia kuna fedha wakati uwezo wa uzalishaji haupo.

"Namuunga mkono Spika katika hili, tunaunganisha watu hata wasiokuwa na mbinu za uzalishaji, naomba tuachane na vikundi havina tija kwa kuwa wanagawana fedha tu," amesema Lusinde.

Profesa Mwamfupe amesema Serikali inagawa vibaya rasilimali fedha kwa kauli ya kasungura kadogo tugawane lakini zinaishia kutoleta tija.

Akijibu hoja hizo, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk Binilith Mahenge amewaagiza wakurugenzi wa wilaya kuangalia ikama ya walimu na kuwatawanya mara moja.

Kuhusu fedha za vikundi kwa vijana na akina mama amesema jambo hilo liko kisheria. Amesema hakuna ubaya kuwasaidia watu mmoja mmoja ambao wanajiweza katika uzalishaji.
 
Je unao ushahidi? Usiongee kwa mambo usiokuwa na ushahidi, ukipigwa pingu hapo utaanza kulalama.
Unaishi Tanzania ipi kushindwa kujua kuwa hayo yapo?
Bila Shaka hujui kuwa kuna Mtu alipigwa Bakora ya Bichwa akazirai,
Mkosaji akiwa huyohuyo anaelalama kutaka Haki itendeke hapo.
Unajua kilichotokea baada ya tukio hilo?
Wengi hatukuwepo eneo la tukio Ila ushahidi ulisambaa na ndio hivyo mambo yalifinyangwafinyangwa.
 
baruti 1
Mkuu,
You're making "makosa ya kimkakati" jiangalie sana uandikavyo...
Nape ameambiwaje baada ya kukosoa sana serikali yake ya CCM!?
ameambiwaje kwani? press reease iko wapi mkuu. mimii naongea vitu vinavyoonekana wala am not basing on hypothesis .
 
Back
Top Bottom