Benjamini Netanyahu
JF-Expert Member
- Aug 7, 2014
- 95,871
- 116,627
Haswamgojwa huyu
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Haswamgojwa huyu
ndio shida iliyopo tena, kuna maeneo ya miji utakuta masista du ndo wamejaa wanagwana hadi topic, wakati shule nyingine hakuna hata mmoja,shida halmashauri ikipewa madaraka inapanga kwa rushwa... za ngono na hela
Sure mkuuBwan' Sheikh,
Toka Lini Nyani akaona Kundule?
Nje ya Kongwa hawezi kituEe,eeee!!??
Subiri Bakora ya Bichwa
Hata mimi simkubali hata kidogo nakuombea kwa Mungu mwenyezi Mungu afanye yake huyu jamaa arudi India then akae huko kwa muda usiojulikana au akutane na watu wasiojulikana ili wamfanye yao.Sema wewe ndo humpendi lakini wengi tunamkubali kwa sana.
➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖mkuu huna hoja na mifano dhahiri kabisa. tunachozungumza hapa ni kuhodhiwa bunge na mahakama,huo mfano wa panga boi hauna mantiki hapa , kwani bunge siku hizi ndo wanatangaza tenda za serikali? nakushauri ukae kimya hauto onekana mjinga
sina muda wa kubishana na karai hata unayozungmza hujui hata ni sehemu gani uliongea uharo wako wa mtu kuhodhi bunge na mahajama. mim ndo nlikutuma udiscus mambo ambayo sio mada ya uzi. mimi nlikua nakupa taarifa tu➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖
↑
shida halmashauri ikipewa madaraka inapanga kwa rushwa... za ngono na hela
,/
Je unao ushahidi? Usiongee kwa mambo usiokuwa na ushahidi, ukipigwa pingu hapo utaanza kulalama.
➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖
Inaelekea;
Ama unachanganya hoja au hujui unachokizungumza.
Msingi na chipuko la majibizano yangu name ni hapo juu.
Sasa wewe hukai kwenye hoja unaniletea habari nyingine.
Hakuna mahala nimegusia Bunge Wala Mahakama.
Na uelewe mini nawewe hatujadili Uzi mkuu.
Unayo shida kidogo kwenye kuelewa.
Huyu Ndugu Gai kumbe anajua kile Wabunge wenzake wanacholiliaga? Yeye akiwa kwenye kiti anajua kusema: Lema Kaa chini! Askari, mtoweni huyu! Sasa yamemkuta. Akiwa kwenye kiti kuwa ANAJISAHAU kama naye ni Mbunge...Mkuki mtamu kwa nguruwe,kwa binadamu......
Hakuona halimashauri zinanyanganywa kodi za majengo,na mabango?Dodoma. Spika wa Bunge, Job Ndugai amepinga mpango wa Serikali wa kuwapangia vituo vya kazi moja kwa moja walimu wanaoajiriwa, akihoji ni kwanini inapoka madaraka ya Halmashauri.
Ndugai ametoa kauli hiyo leo Jumamosi Desemba 23, 2017 ikiwa ni siku moja baada Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Selemani Jafo kutangaza majina ya walimu 3,033 waliopangiwa vituo vya kazi.
Katika kikao cha kamati ya ushauri ya Mkoa wa Dodoma leo, Spika Ndugai amehoji TAMISEMI ni nani hata aweze kujua ikama ya walimu shuleni. Amesema wamekuwa wakijaza walimu maeneo yasiyo na mahitaji.
"Hili jambo linakera, yaani kila mahali sasa ni TAMISEMI hadi napata shaka sasa, hivi hii zana ya D by D (ugatuaji wa madaraka) ina maana haijatafsiriwa vyema au ndiyo kupoka madaraka kwa wengine," alihoji Ndugai.
Spika ametoa mfano wa Shule ya Banyibanyi wilayani Kongwa ambayo amesema ina wanafunzi wanaoingia kidato cha tatu lakini hawajawahi kusoma masomo ya sayansi hata siku moja.
"Lakini juzi hapa mmepanga walimu na nilipita tena hapo hakuna hata mwalimu. Hawajasoma hesabu, fizikia, baiolojia, kemia na jiografia; nauliza tena wanasema Tamisemi, hivi hao walisoma wapi na ninyi mmesoma shule zipi," alihoji.
Ndugai amewatupia mzigo wabunge wa Mkoa wa Dodoma amesema wanatakiwa kuupinga mpango huo bungeni wakati yeye akiongoza vikao vya Bunge.
Pia, amepinga mpango wa utoaji fedha kwa vikundi amesema umepitwa na wakati kwa kuwa zinaliwa bure.
Amesema hakuna umuhimu wa kusema watu waunde vikundi ndipo wapewe fedha au uwezeshwaji, badala yake waangaliwe mtu mmoja mmoja ambao wanakuwa na uwezo wa kuzalisha na kisha wafuatiliwe.
Mbunge wa Mtera, Livingstone Lusinde na Meya wa Manispaa ya Dodoma, Profesa Davis Mwamfupe kwa nyakati tofauti waliunga mkono hoja ya kutopeleka fedha kwa vikundi.
Lusinde amesema kumekuwa na utitiri wa vikundi baada ya kusikia kuna fedha wakati uwezo wa uzalishaji haupo.
"Namuunga mkono Spika katika hili, tunaunganisha watu hata wasiokuwa na mbinu za uzalishaji, naomba tuachane na vikundi havina tija kwa kuwa wanagawana fedha tu," amesema Lusinde.
Profesa Mwamfupe amesema Serikali inagawa vibaya rasilimali fedha kwa kauli ya kasungura kadogo tugawane lakini zinaishia kutoleta tija.
Akijibu hoja hizo, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk Binilith Mahenge amewaagiza wakurugenzi wa wilaya kuangalia ikama ya walimu na kuwatawanya mara moja.
Kuhusu fedha za vikundi kwa vijana na akina mama amesema jambo hilo liko kisheria. Amesema hakuna ubaya kuwasaidia watu mmoja mmoja ambao wanajiweza katika uzalishaji.
Ndungai akae kimya hana research yeyote ile kuhusu hili, alitakiwa kuhoji nini ki,esababisha hadi walimu kupngwa moja kwa moja kutika wizarani, walimu wamejazana mijin huku shule za vijijini zikikosa walimu kwa sababu halmashauri zilikuwa zinakula rushwa na vimemo na maafisa wengine walipata mahawala kupitia deal hilo naunga mkono tamisemi kupanga moja kwa moja kama nduga ana ndugu yake kaoangwa kijijini huko avumilie tu maana nchi hii ni yetu sote na hakuna aliye andikiwa kushi katika mazingira magumu ya kazi.Dodoma. Spika wa Bunge, Job Ndugai amepinga mpango wa Serikali wa kuwapangia vituo vya kazi moja kwa moja walimu wanaoajiriwa, akihoji ni kwanini inapoka madaraka ya Halmashauri.