Spika Ndugai: TAMISEMI inaniudhi sana; kwanini inapora Madaraka ya Halmashauri?

Spika Ndugai: TAMISEMI inaniudhi sana; kwanini inapora Madaraka ya Halmashauri?

Mbona bosi wake amepoka madaraka ya bunge na mahakama na hasemi chochote, aache unafiki kila mbuzi hula kwa urefu wa kamba yake.
Bwan' Sheikh,
Toka Lini Nyani akaona Kundule?
 
Duh, na yeye mkuu wa mhimili wa kutunga sheria analalamika? kwani sheria inasemaje? pole yake.
 
Unaishi Tanzania ipi kushindwa kujua kuwa hayo yapo?
Bila Shaka hujui kuwa kuna Mtu alipigwa Bakora ya Bichwa akazirai,
Mkosaji akiwa huyohuyo anaelalama kutaka Haki itendeke hapo.
Unajua kilichotokea baada ya tukio hilo?
Wengi hatukuwepo eneo la tukio Ila ushahidi ulisambaa na ndio hivyo mambo yalifinyangwafinyangwa.
mkuu mbona unaruka ruka nimekuuliza swali lingine, unanijibu kwa viroja. Umezungumzia juu ya mtu mmoja kuhodhi bunge na mahakama nilikuomba ushahidi unabaki unadunda dunda tuliza akili kamanda nipe huo mfano
 
Ndugai anakumbuka Condom wakati game imeisha!

Tamisemi haijaanza awamu Hii kupangia Walimu vituo Mf. Nafasi za Ualimu za Mwisho kutolewa 2016 or 2015 waliwapangia Walimu mpaka ngazi ya Shule na hata pesa hizi za Kuendesha Shule zinapelekwa Moja kwa Moja shuleni na kila Shule inapokea Mgao wake toka wizarani Moja kwa Moja hazipitii Halmashauri Kazi ya Halmshauri ni ku acknowledge pekee
 
Unaishi Tanzania ipi kushindwa kujua kuwa hayo yapo?
Bila Shaka hujui kuwa kuna Mtu alipigwa Bakora ya Bichwa akazirai,
Mkosaji akiwa huyohuyo anaelalama kutaka Haki itendeke hapo.
Unajua kilichotokea baada ya tukio hilo?
Wengi hatukuwepo eneo la tukio Ila ushahidi ulisambaa na ndio hivyo mambo yalifinyangwafinyangwa.
mkuu mbona unaruka ruka nimekuuliza swali lingine, unanijibu kwa viroja. Umezungumzia juu ya mtu mmoja kuhodhi bunge na mahakama nilikuomba ushahidi unabaki unadunda dunda tuliza akili kamanda nipe huo mfano
 
Kama ni suala la decentralization angekosoa pia ugawaji wa pesa za elimu bila malipo, sasa hivi pesa zote za Elimu bila malipo zinakwenda moja kwa moja mashuleni hazipiti idara ya elimu halmashauri then halmashauri ndio igawe
 
Siamini kama waziri kakurupuka,na siamini kama ndugai kufanya kautafiti hata kadogo tu, mpaka afikie kumpinga waziri
 
Na wewe nawe,
Si Yule Yule aliewahi kumtandikaga mshindani wake Bakora ya medula hadharani.
Na likaisha Kiana.
Umeshanza kwani?
Ohooo mekupata... em tuacheni tuwambe ngoma sie... ngozi lazma tuivutie kwetu
 
ameambiwaje kwani? press reease iko wapi mkuu. mimii naongea vitu vinavyoonekana wala am not basing on hypothesis .

baruti 1 ,
Tafuta mkuu, nimeisha kata tiketi ya ndege kwenda Wellington kuanza rikizo na kisha kwa Madiba.

Hizo clips za onyo waulize vindakindaki wanazo.
 
Siamini kama waziri kakurupuka,na siamini kama ndugai kufanya kautafiti hata kadogo tu, mpaka afikie kumpinga waziri

Haya ndiyo makosa tunayofanya ya kudhania kuwa waziri ni malaika hawezi kukosea.

Poise , tangia namfahamu spika huyo hata kabla ya kuwa spika hizo ndiyo points 2 za msingi ameziongea.. Wallah kabisa.
 
mkuu mbona unaruka ruka nimekuuliza swali lingine, unanijibu kwa viroja. Umezungumzia juu ya mtu mmoja kuhodhi bunge na mahakama nilikuomba ushahidi unabaki unadunda dunda tuliza akili kamanda nipe huo mfano
Wewe umetaka ushahidi,
Nami nakuambia;
Ushahidi ili uhukumu au ufanyeje?
Je, ukiletewa hapa utakusaidia nini wewe?

Ni kweli hujui kuwa huko Halmashuri yapo matukio ya rushwa?

Je, Hufahamu kuwa yapo yanayolalamikiwa kufanyiwa maamuzi mihimili tofauti pasi kufuata taratibu?

Nikuombe kwakuwa mwenzangu wewe ni muumini mzuri mwenyekutuhumu kwa ushahidi maridhawa;
Ni lini na wapi ilitangazwa kandarasi ya manunuzi ya 'Panga Boi'?

Wajuvi wanasema mamlaka na mamlaka yalipokwa katika hili,
Wewe unasemaje?

Toa ushahidi wewe sasa ili tusimuonee jamaa.
Na ya aina hiyo ni mengi tu.

Tukio la 'Bakora'
Nimechomeka,
Ni chagizo tu kuwa unaweza kuwa na ushahidi na ushahidi huo usikusaidie pia kutegemeana na unapambana na nani katika shauri lako.
Ama naongopa?
 
Hizi ni kauli za siasa!,sio kwamba hajui kinachoendelea.
Yaaani, siasa ni usanii tu!,wenye shida wanafikiri kiongozi kulaumu juu ya jambo fulani, kwamba yupo pamoja nao, hii yote ni danganya toto!
 
Mbona rahisi kuelewa ninacho namaanisha?
Wewe umetaka ushahidi,
Nami nakuambia;
Ushahidi ili uhukumu au ufanyeje?
Je, Ushahidi ukiletwa hapa utakusaidia nini wewe?
Na je, Ni kweli hujui kuwa huko Halmashuri Huwa kuna matukio ya rushwa?
Kweli hujui?
Je, Hufahamu kuwa yapo yanayolalamikiwa kufanyiwa maamuzi Bila kufuata taratibu?

Nakuombe nawe kwa kuwa mambo sikuhizi yapo wazi nawe Ni Mtu unaeenda na ushahidi thabiti;
Ni Lini na wapi ilitangazwa kandarasi ya manunuzi ya 'Panga Boi'?
Wajuvi wanasema wajuvi na mamlaka yalipokwa hapa,
Wewe unasemaje?

Na hilo tukio la 'Bakora' Ni chagizo tu kuwa unaweza kuwa na ushahidi na ushahidi huo usikusaidie pia kutegemeana na unapambana na nani.
Ama naongopa?
mkuu huna hoja na mifano dhahiri kabisa. tunachozungumza hapa ni kuhodhiwa bunge na mahakama,huo mfano wa panga boi hauna mantiki hapa , kwani bunge siku hizi ndo wanatangaza tenda za serikali? nakushauri ukae kimya hauto onekana mjinga
 
Back
Top Bottom