Spika Ndugai: TAMISEMI inaniudhi sana; kwanini inapora Madaraka ya Halmashauri?

Spika Ndugai: TAMISEMI inaniudhi sana; kwanini inapora Madaraka ya Halmashauri?

Dodoma. Spika wa Bunge, Job Ndugai amepinga mpango wa Serikali wa kuwapangia vituo vya kazi moja kwa moja walimu wanaoajiriwa, akihoji ni kwanini inapoka madaraka ya Halmashauri.

Ndugai ametoa kauli hiyo leo Jumamosi Desemba 23, 2017 ikiwa ni siku moja baada Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Selemani Jafo kutangaza majina ya walimu 3,033 waliopangiwa vituo vya kazi.

Katika kikao cha kamati ya ushauri ya Mkoa wa Dodoma leo, Spika Ndugai amehoji TAMISEMI ni nani hata aweze kujua ikama ya walimu shuleni. Amesema wamekuwa wakijaza walimu maeneo yasiyo na mahitaji.

"Hili jambo linakera, yaani kila mahali sasa ni TAMISEMI hadi napata shaka sasa, hivi hii zana ya D by D (ugatuaji wa madaraka) ina maana haijatafsiriwa vyema au ndiyo kupoka madaraka kwa wengine," alihoji Ndugai.

Spika ametoa mfano wa Shule ya Banyibanyi wilayani Kongwa ambayo amesema ina wanafunzi wanaoingia kidato cha tatu lakini hawajawahi kusoma masomo ya sayansi hata siku moja.

"Lakini juzi hapa mmepanga walimu na nilipita tena hapo hakuna hata mwalimu. Hawajasoma hesabu, fizikia, baiolojia, kemia na jiografia; nauliza tena wanasema Tamisemi, hivi hao walisoma wapi na ninyi mmesoma shule zipi," alihoji.

Ndugai amewatupia mzigo wabunge wa Mkoa wa Dodoma amesema wanatakiwa kuupinga mpango huo bungeni wakati yeye akiongoza vikao vya Bunge.

Pia, amepinga mpango wa utoaji fedha kwa vikundi amesema umepitwa na wakati kwa kuwa zinaliwa bure.

Amesema hakuna umuhimu wa kusema watu waunde vikundi ndipo wapewe fedha au uwezeshwaji, badala yake waangaliwe mtu mmoja mmoja ambao wanakuwa na uwezo wa kuzalisha na kisha wafuatiliwe.

Mbunge wa Mtera, Livingstone Lusinde na Meya wa Manispaa ya Dodoma, Profesa Davis Mwamfupe kwa nyakati tofauti waliunga mkono hoja ya kutopeleka fedha kwa vikundi.

Lusinde amesema kumekuwa na utitiri wa vikundi baada ya kusikia kuna fedha wakati uwezo wa uzalishaji haupo.

"Namuunga mkono Spika katika hili, tunaunganisha watu hata wasiokuwa na mbinu za uzalishaji, naomba tuachane na vikundi havina tija kwa kuwa wanagawana fedha tu," amesema Lusinde.

Profesa Mwamfupe amesema Serikali inagawa vibaya rasilimali fedha kwa kauli ya kasungura kadogo tugawane lakini zinaishia kutoleta tija.

Akijibu hoja hizo, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk Binilith Mahenge amewaagiza wakurugenzi wa wilaya kuangalia ikama ya walimu na kuwatawanya mara moja.

Kuhusu fedha za vikundi kwa vijana na akina mama amesema jambo hilo liko kisheria. Amesema hakuna ubaya kuwasaidia watu mmoja mmoja ambao wanajiweza katika uzalishaji.
Yule waziri mswahili hajatulia kabisa........ mapepe mengi!
 
Unajua sana budget zinapitishwa Magogoni(uwanja wa ndege, hospitali ya rufaa, ofisi za TRA Mkoa Chattle, n.k)
Vipi unaweza kuleta vifungu vinavyomzuia kufanya hivo?
 
sina muda wa kubishana na karai hata unayozungmza hujui hata ni sehemu gani uliongea uharo wako wa mtu kuhodhi bunge na mahajama. mim ndo nlikutuma udiscus mambo ambayo sio mada ya uzi. mimi nlikua nakupa taarifa tu
Hoja kwa hoja.
Na Mimi nilikujibu pale tulipoanzia Ila kwakuwa yaelekea huna majibu ya hoja zangu tumalize majadiliano bila matusi la kama unadhani nitakurudishia matusi sitafanya hivyo,
Mwenzako nimelelewa,
Pole yako kwakukosa malezi,
Sikufunzwa kutusi watu kwakuwa tu tunapishana hoja,kauli au misimamo.
Hapinyuyia!
 
Wamefanya vizuri sana TAMISEMI maana ukiritimba ulikuwa mkubwa sana watu kubadili vituo hovyo hovyo mlundikano wa watumishi wengibshule moja hususani mijini au barabarani sasa naona wamelenga [HASHTAG]#Ngarenayuki[/HASHTAG] na peripheral of the peripheral
 
Waziri wa TAMISEMI yuko sahihi;Halmashauri nyingi zinawapangia walimu vituo kwa misingi ya rushwa hasa dada zetu rushwa ya ngono.Waziri akiwapangia kituo siyo rahisi kukwepa kituo na itakomesha rushwa hongera sana Waziri wa TAMISEMI.Huwa inashangaza sana Mwalimu kapangiwa kituo chake Morogoro kisha muda mfupi unamkuta Dar es salam
 
Asante
 
Tamisemi ilishahamishiwa chini ya ofisi ya raisi sio?Basi ajiandae huyo anayepingana na ofisi kuu.
 
Leo mida ya jioni Nilikuwa naongea na Afisa Utumish mmoja wa halmashaur
Flani

Nikajaribu kumuuliza hili Swala LA Spika na tamisemi ikoje

Kwanin wanapanga Watumishi Vituo badala ya ninyi wakati ikama mnayo nyie

Majibu yake ni kwamba wao tamisemi wanapata taarifa ya uhitaji kupitia wao na akatoa mfano halmashaur yetu imepokea Walimu 12 tu idara msingi na kiukweli wamepangwa vituo ambavyo kweli vinaupungufu na ni vya vijinini Sana ndani hukooo

Tamisemi IPO sahihi
 
Hivi hizo fedha za vikundi zinatolewa wapi wadau?
 
Saturday, December 23, 2017
Ndugai akosoa upangaji vituo vya kazi kwa walimu

spika+pic.jpg

Kwa ufupi
Amesema Tamisemi imekuwa ikiwajaza walimu maeneo yasiyo na mahitaji.

By Habel Chidawali, Mwananchi hchidawali@mwananchi.co.tz

Dodoma. Spika wa Bunge, Job Ndugai amepinga mpango wa Serikali wa kuwapangia vituo vya kazi moja kwa moja walimu wanaoajiriwa, akihoji ni kwa nini inapoka madaraka ya halmashauri.

Ndugai ametoa kauli hiyo leo Jumamosi Desemba 23,2017 ikiwa ni siku moja baada Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tamisemi Selemani Jafo kutangaza majina ya walimu 3,033 waliopangiwa vituo vya kazi.

Katika kikao cha kamati ya ushauri ya Mkoa wa Dodoma leo, Spika Ndugai amehoji Tamisemi ni nani hata aweze kujua ikama ya walimu shuleni. Amesema wamekuwa wakijaza walimu maeneo yasiyo na mahitaji.

"Hili jambo linakera, yaani kila mahali sasa ni Tamisemi hadi napata shaka sasa, hivi hii zana ya D by D (ugatuaji wa madaraka) ina maana haijatafsiriwa vyema au ndiyo kupoka madaraka kwa wengine," alihoji Ndugai.

Spika ametoa mfano wa Shule ya Banyibanyi wilayani Kongwa ambayo amesema ina wanafunzi wanaoingia kidato cha tatu lakini hawajawahi kusoma masomo ya sayansi hata siku moja.

"Lakini juzi hapa mmepanga walimu na nilipita tena hapo hakuna hata mwalimu. Hawajasoma hesabu, fizikia, baiolojia, kemia na jiografia; nauliza tena wanasema Tamisemi, hivi hao walisoma wapi na ninyi mmesoma shule zipi," alihoji.

Ndugai amewatupia mzigo wabunge wa Mkoa wa Dodoma amesema wanatakiwa kuupinga mpango huo bungeni wakati yeye akiongoza vikao vya Bunge.

Pia, amepinga mpango wa utoaji fedha kwa vikundi amesema umepitwa na wakati kwa kuwa zinaliwa bure.

Amesema hakuna umuhimu wa kusema watu waunde vikundi ndipo wapewe fedha au uwezeshwaji, badala yake waangaliwe mtu mmoja mmoja ambao wanakuwa na uwezo wa kuzalisha na kisha wafuatiliwe.

Mbunge wa Mtera, Livingstone Lusinde na Meya wa Manispaa ya Dodoma, Profesa Davis Mwamfupe kwa nyakati tofauti waliunga mkono hoja ya kutopeleka fedha kwa vikundi.

Lusinde amesema kumekuwa na utitiri wa vikundi baada ya kusikia kuna fedha wakati uwezo wa uzalishaji haupo.

"Namuunga mkono Spika katika hili, tunaunganisha watu hata wasiokuwa na mbinu za uzalishaji, naomba tuachane na vikundi havina tija kwa kuwa wanagawana fedha tu," amesema Lusinde.

Profesa Mwamfupe amesema Serikali inagawa vibaya rasilimali fedha kwa kauli ya kasungura kadogo tugawane lakini zinaishia kutoleta tija.

Akijibu hoja hizo, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk Binilith Mahenge amewaagiza wakurugenzi wa wilaya kuangalia ikama ya walimu na kuwatawanya mara moja.

Kuhusu fedha za vikundi kwa vijana na akina mama amesema jambo hilo liko kisheria. Amesema hakuna ubaya kuwasaidia watu mmoja mmoja ambao wanajiweza katika uzalishaji.
 
Hakuna hoja yenye akili inayoweza kutoka kwenye ubongo wa Ndugai. Anapapasa tu.
 
Wanalialia tu lakini wakifika bungeni kazi yao ni kugonga meza na kuunga mkono kila kitu!
 
[emoji730] [emoji729] [emoji728] [emoji727] [emoji726] [emoji725] [emoji731] [emoji732] [emoji723] [emoji722] [emoji773] [emoji774] [emoji775] [emoji777] [emoji778] [emoji783] [emoji784] [emoji666] [emoji665] [emoji658] [emoji651] [emoji651] [emoji651] [emoji660] [emoji657] [emoji648] [emoji655] ukiingia deep, watu wengi tumevurugwa [emoji16] [emoji15] [emoji16] [emoji15] [emoji16] [emoji15] [emoji16] [emoji15] [emoji16] [emoji15] [emoji16] [emoji15] [emoji16] [emoji15] [emoji16] [emoji15]
 
Tatizo la walimu wa masomo ya sayansi ni kubwa na lipo maeneo mengi wasomi wa masomo hayo ni wachache na Kati ya hao 3000 walimu wa secondary ni 700 tu,sasa Kuna wilaya ngapi nchi hi? Na Kila wilaya ina takriban shule zisizo pungua 20 Kila shule huenda inaukosefu au upungufu wa walimu, sasa analaumu nini na kutusi wengine angeonekana wa maana saana endapo angehoji kwanini 700 tu na sio 7000 waajiriwe?
 
Back
Top Bottom