Spika Ndugai: TAMISEMI inaniudhi sana; kwanini inapora Madaraka ya Halmashauri?

Spika Ndugai: TAMISEMI inaniudhi sana; kwanini inapora Madaraka ya Halmashauri?

mbona yeye mwenyewe kaporwa mamlaka yake huyu,atuachie kelele zake.katika watu ambao heshima yao imepporomoka wa kwanza ni huyu
 
Anashangaa nini?Hiyo ndiyo habari ya hivi sasa.Kwa nini hashangai bunge kupokwa madaraka?
 
Ndugai keshasahau kua,TAMISEMI ipo kwenye mikono ya mkulu, haipo kwa PM.kwahiyo anatakiwa ajue unaweza kuwaza kumkomoa mtu kumbe unajukomoa mwenyewe.
 
Supikaaaaa!! Hao wanafanya vizuri sana Kwa sababu wao hutekeleza mapendekezo us madeo wajuaye hitaji lilipo. Wanasiasa mkiletewa mwataka tumia visu vyenu kujaza wote katani kwako. Diwani asiye na nguvu hukosa kabisa
 
"Hili jambo linakera, yaani kila mahali sasa ni TAMISEMI hadi napata shaka sasa, hivi hii zana ya D by D (ugatuaji wa madaraka) ina maana haijatafsiriwa vyema au ndiyo kupoka madaraka kwa wengine," alihoji Ndugai.

Ndugai amewatupia mzigo wabunge wa Mkoa wa Dodoma amesema wanatakiwa kuupinga mpango huo bungeni wakati yeye akiongoza vikao vya Bunge.

Spika ametoa mfano wa Shule ya Banyibanyi wilayani Kongwa ambayo amesema ina wanafunzi wanaoingia kidato cha tatu lakini hawajawahi kusoma masomo ya sayansi hata siku moja.

Ukisikia "ih!! jua jiwe limempiga kichwani gizani, maumivu hayo ndiyo hupata wengine, lakini wakipaza sauti wanaitwa wachochezi


Akijibu hoja hizo, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk Binilith Mahenge amewaagiza wakurugenzi wa wilaya kuangalia ikama ya walimu na kuwatawanya mara moja.

labda kunahitajika semina elekezi kwa mawaziri, lakini pia mwandishi wa habari hii alipaswa kumhojo waziri wa TAMISEMI
 
Halmashauri zinarundika walimu mijini kwenye uhitaji wa walimu unakuta kuna walimu 3 tu shule nzima.
Ninashauri kuwa, mfumo Wa kuwapanga walimu moja kwa moja shule husika au kituo cha kazi ni mzuri sana na uendelee,Ila marekebisho yafuatayo yafanyike. Moja, shule zote ziingize kwenye mfumo ikiwepo majina ya walimu,idadi ya wanafunzi,masomo ,upungufu,na ziada ili wakati tamisemi inawapanga walimu watumie mfumo au takwimu zilizoko kwenye mfumo na mfumi huo iwe updates kila wakati. Pili maafisaelimu ni mzigo mkubwa kwa serikali hawajui wafanyalo Ila misharaha ni mikubwa na kil wilaya Ina maafisaelimu wawili ,Wa sekondari na Wa msingi, wakitumwa takwimu Leo na tamisemi wanapeleka kesho, matokeo yake takwimu haziendi kwa wakati, ushauri maafisaelimu wapangwe upya nchi nzima na kila hamashauri iwe na afisaelimu mmoja tu badala ya wawili .tatu shule za mjini walimu wamezidi wengine hata vipindi vya kufundisha hawana Ila wanalipwa wahamishwe wapelekwe vijijini,mfano manispaa ya Moshi walimu waliozidi ni zaidi ya 360 shule za sekondari,wahamishwe wapelekwe kongwa na kwingineko.nne utaratibu unaotumiwa na tamisemi ni mzuri sana unapunguza rushwa ya pesa na ngono uendelee.Ova
 
Afadhali angalau na yeye imuudhi.kidogo kama anavyotufanyia, huko kongws kuna ombwe la viongozi
Dodoma. Spika wa Bunge, Job Ndugai amepinga mpango wa Serikali wa kuwapangia vituo vya kazi moja kwa moja walimu wanaoajiriwa, akihoji ni kwanini inapoka madaraka ya Halmashauri.

Ndugai ametoa kauli hiyo leo Jumamosi Desemba 23, 2017 ikiwa ni siku moja baada Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Selemani Jafo kutangaza majina ya walimu 3,033 waliopangiwa vituo vya kazi.

Katika kikao cha kamati ya ushauri ya Mkoa wa Dodoma leo, Spika Ndugai amehoji TAMISEMI ni nani hata aweze kujua ikama ya walimu shuleni. Amesema wamekuwa wakijaza walimu maeneo yasiyo na mahitaji.

"Hili jambo linakera, yaani kila mahali sasa ni TAMISEMI hadi napata shaka sasa, hivi hii zana ya D by D (ugatuaji wa madaraka) ina maana haijatafsiriwa vyema au ndiyo kupoka madaraka kwa wengine," alihoji Ndugai.

Spika ametoa mfano wa Shule ya Banyibanyi wilayani Kongwa ambayo amesema ina wanafunzi wanaoingia kidato cha tatu lakini hawajawahi kusoma masomo ya sayansi hata siku moja.

"Lakini juzi hapa mmepanga walimu na nilipita tena hapo hakuna hata mwalimu. Hawajasoma hesabu, fizikia, baiolojia, kemia na jiografia; nauliza tena wanasema Tamisemi, hivi hao walisoma wapi na ninyi mmesoma shule zipi," alihoji.

Ndugai amewatupia mzigo wabunge wa Mkoa wa Dodoma amesema wanatakiwa kuupinga mpango huo bungeni wakati yeye akiongoza vikao vya Bunge.

Pia, amepinga mpango wa utoaji fedha kwa vikundi amesema umepitwa na wakati kwa kuwa zinaliwa bure.

Amesema hakuna umuhimu wa kusema watu waunde vikundi ndipo wapewe fedha au uwezeshwaji, badala yake waangaliwe mtu mmoja mmoja ambao wanakuwa na uwezo wa kuzalisha na kisha wafuatiliwe.

Mbunge wa Mtera, Livingstone Lusinde na Meya wa Manispaa ya Dodoma, Profesa Davis Mwamfupe kwa nyakati tofauti waliunga mkono hoja ya kutopeleka fedha kwa vikundi.

Lusinde amesema kumekuwa na utitiri wa vikundi baada ya kusikia kuna fedha wakati uwezo wa uzalishaji haupo.

"Namuunga mkono Spika katika hili, tunaunganisha watu hata wasiokuwa na mbinu za uzalishaji, naomba tuachane na vikundi havina tija kwa kuwa wanagawana fedha tu," amesema Lusinde.

Profesa Mwamfupe amesema Serikali inagawa vibaya rasilimali fedha kwa kauli ya kasungura kadogo tugawane lakini zinaishia kutoleta tija.

Akijibu hoja hizo, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk Binilith Mahenge amewaagiza wakurugenzi wa wilaya kuangalia ikama ya walimu na kuwatawanya mara moja.

Kuhusu fedha za vikundi kwa vijana na akina mama amesema jambo hilo liko kisheria. Amesema hakuna ubaya kuwasaidia watu mmoja mmoja ambao wanajiweza katika uzalishaji.
 
Nimependa alivoponda ulazima wa kuunda Vikundi, Vikundi ndio mpate kukopeshwa fedha za kuwezeshwa, kuungana interest za kufanana kwa Leo ni kazi sana, ubepari hauwezi hayo, kuhusu Walimu, halmashauri za utawala za chini ziruhusiwe kutafuta walimu bora kwa kutumia uzalendo wa eneo, kuna watu kibao wa naweza kufundisha ila hawaruhusiwi kwa kuwa hawatambuliwi, sasa serikali itafute namna ya kuwathibitisha ubora wao iwatumie
 
Tamisemi inapokea taarifa kutoka katika Halmashauri kupitia, ofisi ya Ras, ambayo kuna afisa elimu mkoa
 
Huu mfumo ni mzuri sana. Waziri aendelee nao. Mfumo wa zamani ndio ulirundika walimu mijini kwa rushwa na kujuana. Spika atulie, shule yake itapangiwa walimu endapo shule nyingne zenye hali mbaya zaidi ya yake zitapata walimu.
 
LOcal government (halmashauri)zimeanza kupoteza umaana kwa sababu ya utendaji kazi wake.majukumu mengi wananyang'anywa , wameondoa barabara wamepeleka tarura, na mwakani wataondoa maji wataundiwa chombo cha usimamizi, wataondoa kilimo wataunda tena hii ni kwa sababu halmashauri zetu zinafanya kazi kwa mazoea na kazi zao hazina tija na wala hazionekani.kumejaa majungu,malumbano,ushirikina na migogoro isiyoisha na madiwani
 
Vp jamaa wa Tamisem walikuwa karibu yke nn? Nafikiri ile BAKORA INAWAHUSU WATU KAM hao na kule bungeni unachokifanya Ndugai bakora ile inabid ikuhusu tu
 
Mbona na wewe madaraka yako yamepokwa hufanyi kitu.
 
Back
Top Bottom