Spika Ndugai: Uingereza kuna Mbunge aliapishiwa hospitali akiwa amelazwa na "bahati" mbaya alifariki bila kwenda Bungeni

Spika Ndugai: Uingereza kuna Mbunge aliapishiwa hospitali akiwa amelazwa na "bahati" mbaya alifariki bila kwenda Bungeni

Hiyo ni exception inayotokana na dharura, but sio suala la gereji pale hapakuwa na ulazima wowote wa kuharakisha hilo jimbo, sioni ni kitu gani kinamshinda kuwela ratiba ya uapisho bungeni kwenye kikao cha bunge kitachofuata.
 
Ile siku bwana mdogo Ndugai anamuapisha Polepole lakini anaongelea mambo ya Chadema na kusema kuna "unyanyasaji wa kijinsia" akiwatumia akina Halima Mdee kama Mfano. Halima anafanya press yake na kusema Chadema hakuna mfumo dume kama inavyoelezwa, maana wao wamekuwa viongozi huko. Ndugai anajionaje?
 
Ndugai amerudisha heshima ya Bunge.

Wabunge wa vyama vya ajabu ajabu walikua wameanza kutukana watu bungeni. Na hata kutaka kurusha ngumi!!

Ndugai atakumbukwa kwa hilo. Mbunge anasimama na kuanza kumfokea spika badala ya kuzungumzia maendeleo ya jimbo lake.

Sasa Bunge limekua na hadhi na heshima . Wanastahili kuitwa waheshimiwa chini ya uongozi wa Ndugai.
 
Nitajie kifungu kinachokataza!
Soma ibara ya 68 ya katiba ya Tanzania
606881.jpg
 
Wabunge wa CHADEMA walihitaji kufungwa spare parts mpya ndo wakaapishwa gereji? Labda walikuwa hoi ndo maana hawakufika kwenye Kikao cha kujieleza!
 
Kwani hao kina Mdee walikuwa wagonjwa kiasi kwamba wasingeweza kufika bungeni kuapishwa? kuna mambo mengine speaker ni aibu hata kuyajadili, wewe ongoza bunge ujipatie mkate wako tu sio Kulazimisha mambo ambayo hayapo.
 
Kwani hao kina Mdee walikuwa wagonjwa kiasi kwamba wasingeweza kufika bungeni kuapishwa? kuna mambo mengine speaker ni aibu hata kuyajadili, wewe ongoza bunge ujipatie mkate wako tu sio Kulazimisha mambo ambayo hayapo.
Wewe ulivyowaona ni wazima wale?
 
Kikubwa nilichoona hapo nikatiba kubadilishwa ili iendane na mifumo ya kisasa.
 
Mfano, Uganda wanaruhusu mgombea binafsi. Mfano, Kenya wana tume huru. Mifano iko mingi. Tunahitaji katiba mpya, ndi jawabu.
 
Mwaka 1972 Senator Joe Biden (Rais mteule wa USA) aliapishwa akiwa hospitalini akiwauguza watoto wake wawili walionusurika kwenye ajali mbaya ya gari iliyochukua maisha ya mke wake na binti yake mdogo! Suala la wapi mtu anaapishwa linategemea na mazingira kulingana na kanuni zilizopo.
Kwani hawa Covid 19 walikuwa wanaumwa au wanadharula gani? Kwa nini asisubiri kikao kinachokuja? Any way nahisi kuna kamati walikuwa wanatakiwa kupangiwa. Lakini sio kuforce king namna hii.
 
Ni vyema kuwepo na utaratibu wa kuchagua vya kuiga na visivyoigwa kwani chadema na upinzani wakitolea mfano chochote tokea ulaya America huitwa wametumwa na mabeberu lakini ccm wakitolea mifano ya wazungu wao hujiona wapo sawa tu
 
Back
Top Bottom