Spika Ndugai: Uingereza kuna Mbunge aliapishiwa hospitali akiwa amelazwa na "bahati" mbaya alifariki bila kwenda Bungeni

Spika Ndugai: Uingereza kuna Mbunge aliapishiwa hospitali akiwa amelazwa na "bahati" mbaya alifariki bila kwenda Bungeni

Ni vyema kuwepo na utaratibu wa kuchagua vya kuiga na visivyoigwa kwani chadema na upinzani wakitolea mfano chochote tokea ulaya America huitwa wametumwa na mabeberu lakini ccm wakitolea mifano ya wazungu wao hujiona wapo sawa tu
Tupo kwenye jumuiya ya madola!
 
Kama ni kweli sawa... mgonjwa kuapishiwa sipitali makes a load of sense.

Sasa.... hawa COVID-19 walivyoapishiwa gereji ina maana wao ni magari mikangafu?
 
Sasa katazo liko wapi?

Bunge ni pamoja na eneo lake lote!
Unauliza katazo liko wapi?!Kwani sheria inaposema kuwa mbunge aapishwe kwenye bunge haijakataza kuapisha mbunge katika sehemu nyingine kama vile misikitini,makanisani,masokoni,e.t.c?

Bunge siyo pomaja na eneo lake lote.Bunge maana yake ni ule mkusanyiko rasmi wa wabunge wote wakiwa katika shughuli zao za vikao rasmi vya bunge pamoja na kanuni zote zinazoendesha mkusanyiko huo ndani ya jengo la bunge.

Note:Nimetaja vitu vinne katika definition yangu ya bunge:

1.Mkusanyikao rasmi wa wabunge(Assumption hapa ni kwamba wahudhurie wabunge wote japo haiwezekani kutokana na wengine kuwa na udhuru)

2.Shughuli rasmi za vikao vya bunge

3.Kanuni za uendeshaji wa bunge zizingatiwe

4.Ndani ya jengo rasmi la bunge

Hiyo ndiyo definition sahihi ya bunge.Lakini ukiangalia wale wabunge walioapishwa pale garage kuna sifa za "bunge" zilikosekana pale kama vile mkusanyiko/kikao rasmi cha bunge pamoja na shughuli rasmi ya bunge.
 
Mfano, Uganda wanaruhusu mgombea binafsi. Mfano, Kenya wana tume huru. Mifano iko mingi. Tunahitaji katiba mpya, ndi jawabu.
Hata kenya wanaruhusu kupinga matokeo ya Urais mahakamani kama malawi na hata Afrika kusini wanaruhusu Rais aliyepo madaraka kuhojiwa na Bunge na hata kushitakiwa, katiba ya namna hii ikija Tanzania ndipo kutakuwa na Haki pasipo uonevu mkubwa uliopo sasa kwenye utawala wa akina Ndungai waliojiwekea kinga za kutoshitakiwa
 
Kama ni kweli sawa... mgonjwa kuapishiwa sipitali makes a load of sense.

Sasa.... hawa COVID-19 walivyoapishiwa gereji ina maana wao ni magari mikangafu?
ipo siku wataapishwa hata Guest house
 
Mfano wake ni nzuri CCM iulinde kwa nguvu zote na iutekeleze bila aibu, Malawi ilirudia uchaguzi baada ya kuonekana haukuenda vizuri hivyo CCM ikubali kuurudia uchaguzi chini ya NEC mpya kama ilivyofanya Malawi, wote ni wanachama wa Jumuia ya Madola pamoja na Uingereza.
 
Covid 19 wamejipeleka kihuni ndiyo maana na yeye Ndungai kawaapisha kienyeji kama wapo kwenye jando la ukeketaji
 
Spika wa bunge anaapishiwa wapi?
Kwa nini unatoka nje ya mada?Sisi mada yetu inahusu speaker kuapisha wabunge na wala siyo speaker kuapishwa.Ishu ya speaker kuapishwa ni tofauti kabisa wala haina uhusiano wowote na wabunge kuapishwa na inasimamiwa na sheria nyingine tofauti kabisa.
 
Kwani Tanzania na uingereza tunatumia katiba moja?!...linapokuja swala la utawala wa sheria tunaangalia uingereza wanafanyaje ili tuige au tunaangalia katiba yetu inasemaje?!...viongozi uchwara wanatusumbua sana
 
Hiyo ni exception inayotokana na dharura, but sio suala la gereji pale hapakuwa na ulazima wowote wa kuharakisha hilo jimbo, sioni ni kitu gani kinamshinda kuwela ratiba ya uapisho bungeni kwenye kikao cha bunge kitachofuata.
Mungu hapendi uonevu wao ndiyo maana kawaumbua kwa style hiyo, mungu huwa na njiani nyingi za kuwaumbua maadui wa haki za watu
 
Kwa nini unatoka nje ya mada?Sisi mada yetu inahusu speaker kuapisha wabunge na wala siyo speaker kuapishwa.Ishu ya speaker kuapishwa ni tofauti kabisa wala haina uhusiano wowote na wabunge kuapishwa na inasimamiwa na sheria nyingine tofauti kabisa.
Tuko kwenye definition ya bunge bwashee.
 
Ndugai hao wenzetu Waingereza Katiba yao haisemi take oath before the parliament. Tatizo wewe umetunga kanuni inayokinzana na sheria mama ( katiba). Chutama.
 
Kwani Tanzania na uingereza tunatumia katiba moja?!...linapokuja swala la utawala wa sheria tunaangalia uingereza wanafanyaje ili tuige au tunaangalia katiba yetu inasemaje?!...viongozi uchwara wanatusumbua sana
Huo ni mfano tu bwashee usilie lie!
 
Kwani Tanzania na uingereza tunatumia katiba moja?!...linapokuja swala la utawala wa sheria tunaangalia uingereza wanafanyaje ili tuige au tunaangalia katiba yetu inasemaje?!...viongozi uchwara wanatusumbua sana
Kama suala ni kuiga Uingereza mbona hawaigi kuwa na mfalume na Serikali kuongozwa na waziri mkuu kisha Bunge kuwa na nguvu ya maamuzi sahihi Spika anayeheshimu taratibu na Sheria siyo kama Tanzania Spika anatumia mawazo yake binafsi na ushauri wa mkewe kuongoza Bunge.
 
Umeeleweka vizuri sana mkuu. "Kuapishwa ni jambo moja, na kuingia Bungeni ni jambo la pili"

Nimejaribu kufuatilia threads/comments zako kwenye hili sakata la "wabunge" wa viti maalumu "kutoka CHADEMA" nimegundua umeujua mchezo mchafu uliofanywa na wanaotaka hawa wamama wawe "WABUNGE"

Tusubiri tuone kama watakua wabunge/wataingia Bungeni, pamoja na kwamba wameapishwa.
 
Back
Top Bottom