No. Maendeleo yana chama. Kwa miaka kadhaa Uturuki ilikuwa ikichukuliwa kama 'mtu mgonjwa wa Ulaya' kutokana na ubovu wa uchumi wake. Vyama kadhaa vimekuja vikaondoka lakini havikuweza kuuguza gonjwa gumu la kufanya uchumi wa Uturuki angalau ufanane hata na ule wa nchi maskini zaidi Ulaya (kabla ya Umoja wa Ulaya) Ureno.
Fast Forward, kimekuja chama cha Adala (Justice) cha Prime Minister Rajab Orduwan....hivi sasa Uturuki ndiyo yenye uchumi imara zaidi Ulaya, kiasi Wazungu (kama kawaida yao) wanaanza kuiweka mizengwe na kuipiga vita.
Uturuki ndiyo yenye fleet kubwa zaidi ya ndege duniani, ina uwanja mkuu zaidi wa ndege duniani, inazalisha vitu viwandani zaidi kuliko nchi zote za Ulaya ukitoa Ujerumani! Nani anasema maendeleo hayana chama? Kitoeni hicho chama chenu kizee muone kama nchi haitapaa!