Spika Ndugai usijilinganishe na Jenerali Ulimwengu

Spika Ndugai usijilinganishe na Jenerali Ulimwengu

Sina imani na wote wawili, Ndugai na Jenerali Ulimwengu.

Sina imani na Jenerali Ulimwengu hata kidogo tokea gazeti lake la Rai kwenye kampeni ya 2005 limchafue Salim Ahmed Salim na kumpamba JK na wengi walioshiriki walibarikiwa kupewa vyeo!!

BW Mkapa ile kampeni timu yake ya 1995 wale wengi wa karibu aliwatema live na hapo ndo bifu kuubwa mkapa alilopata toka kwa hao akina Jenerali na wenzie.

Kwa hiyo Jenerali hakutegemea kabisa kutoswa kivile mpaka akaanzisha makala kali za kuukosoa sana utawala wa BWM.

JK kuingia mwanzoni akaanza kumpamba, nanukuu ''Kwa mara ya kwanza tumepata kiongozi anayekemea rushwa kwa uwazi kabisa''. (maneno ya Jenerali hayo kwa JK)

Ghafla akagundua jamaa wala sio kama anavyofikiri. Hapo alitambua nguvu za akina Rostam Aziz dhidi ya JK na mtandao kwa ujumla ambao Jenerali hawakumu hitaji yeye, Salva, Shoo wakaparaganyika na RA kiulaini akainunua HCL na kuiweka chini yake huku Salva akielekea Ikulu, Shoo mtaani lakini akipata chapuo za kazi toka kwa RA kupitia Salva.

Wakati wa Mwendazake huyu Jenerali alikuwa baridi kama maji ya kwenye mtungi. Hakuthubutu kumkosoa wala kimsema kwani alijuwa kuwa anaweza kumpoteza kama walivyopotea akina Ben Saanane.

Tunaposhabikia hii vuta nikuvute ya Jenerali tujuwe tuna deal na mtu anayependa kujifanya ana akili sana na ni mjuwaji wa kuweza kumuamrisha hata Rais afanye anavyotaka yeye
Sisi tunaangalia nguvu ya hoja zake ya sasa hivi. Historia ya nyuma SI hoja. Jaribu kuchambua alichoongea kwa sasa. Hata kwa speaker tukiangalia ya nyuma yanatisha.
 
Kupiga picha na viongozi mbalimbali haikupi mamlaka ya kuropoka hivyo,ndio maana mkapa alimnyang'anya uraia amshukuru jaji waryoba kumsaidia,na wakati wa magu,alimpigia simu kumuonya asiropoke,jamaa kafikisika kabisa anategemea mkewe kwa kika kitu, sasa ndio anaropoka hovyo

Sent from my SM-N960F using JamiiForums mobile app
Mnataka taifa la wakaa kimya ama siyo????
Kuropoka manake ni kuongea hovyo ( kurocha) karopoka nn ???
Huyo magufuli alikuwa hajawani tyuuu
 
Jenerali ulimwengu sio mtanzania , Mimi simkubali Bora kina lissu na mbowe wakosoe maana ni wenzetu, jenerali anatumika na kagame
 
Jenerali ulimwengu sio mtanzania , Mimi simkubali Bora kina lissu na mbowe wakosoe maana ni wenzetu, jenerali anatumika na kagame
Si raia kwa kigezo kipi?
IMG_20211112_192010.jpg
 
Kwa hiyo kwa hizi picha Ulimwengu amefanya kipi cha ziada katika kuitumikia nchi yetu?
Ameiwakilisha nchi katika/ameifanyia nchi mambo mengi ambayo ukiwa serious kuperuzi utayafahamu kwani inaonekana enzi yuko active serikalini haukuwa na ufahamu.
IMG_20211113_112116.jpg
 
Tuna kazi kubwa ya kuwaondoa akina Ndugai na mifumo yao la sivyo nchi hii hali itakuwa mbaya zaidi.
Wanatamani taifa liwe tu na watu wa kusifia kila kitu na kuimba mapambio kwa watawala, hawataki kabisa kukosolewa au watu kutoa mawazo yao kama yatakuwa yanakinzana na mitazamo watakayo watawala.
 
Kupiga picha na viongozi mbalimbali haikupi mamlaka ya kuropoka hivyo,ndio maana mkapa alimnyang'anya uraia amshukuru jaji waryoba kumsaidia,na wakati wa magu,alimpigia simu kumuonya asiropoke,jamaa kafikisika kabisa anategemea mkewe kwa kika kitu, sasa ndio anaropoka hovyo

Sent from my SM-N960F using JamiiForums mobile app
Alinyanganywa uraia baada ya kufichua uwizi WA rafiki yake MKAPA. ULIMWENGU NI MTU MAKINI.mwweedi na anajitanbua KULIKO Ndungai. Ndungai anajimwambafai kwenye kiti cha kuchaguliwa,HAJUI kesho kwenye kiti hicho atakuwa hayupo. Amuulize Polepole,Leo sio mwenezi tena WA CCM. Amuulize Makonda sio mkuu WA mkoa tena. Amuulize huyo uliye SEMA alimpora URAIYA,Yuko wapi na yako wapi aliyojitapia. Kuwa MAKINI.
 
Kwa yoyote mwenye elimu na ufahamu wa mambo ya dunia, hasa siasa za Kimataifa, atajua Tanzania ina Spika wa Bunge ovyo kabisa kutokea katika historia ya nchi. Yeye ni matokeo halisi ya siasa za kulindana, kumegeana na uchama, na wala si uwakilishi wa akili na weledi wa Watanzania.
Bunge limekuwa linaburuzwa tu na executive hadi katiba kuvunjwa na kupondwapondwa yeye akiona, bali akisaidia. Kazi yake kubwa ni kushambulia upinzani, kukamia watu walio huru na wenye elimu mara sabini kuliko yeye. Kwa akili yake, bado yuko katika utawala wa Hayati!
 
Kumlinganisha Komredi Jenerali Ulimwengu (the great wall) na ndugai ni sawa na kulinganisha mlima Kilimanjaro na kichuguu.
Mmoja amejenga legacy njema na kubwa sana kwa kizazi kijacho, mwingine ataacha legacy ya hovyo kabisa ktk nchi hii 🤣
 
Mwanaccm ccm mm siwezi kumfananisha huyu Babu wetu mzalendo yaani Mzee Ulimwengu na Ndugai kwani Ndugai bado kabisa kwa sababu bado anajifunza kuishi.

Mzee Ulimwengu Mwenyenzi Mungu azidi kukulinda na kukupa hekima zaidi
 
Kupiga picha na viongozi mbalimbali haikupi mamlaka ya kuropoka hivyo,ndio maana mkapa alimnyang'anya uraia amshukuru jaji waryoba kumsaidia,na wakati wa magu,alimpigia simu kumuonya asiropoke,jamaa kafikisika kabisa anategemea mkewe kwa kika kitu, sasa ndio anaropoka hovyo

Sent from my SM-N960F using JamiiForums mobile app
Unaweza kutuambia kuwa ameropoka nini?
 
Back
Top Bottom