Spika Ndugai: Vijana wa Tanzania hawaaminiki, wakiachiwa biashara bila kuiba wanajiona wajinga

Spika Ndugai: Vijana wa Tanzania hawaaminiki, wakiachiwa biashara bila kuiba wanajiona wajinga

Mkuu unajisikiaje nafsini kwako kwa hiki ulichokiandika?
Haijalishi upo nyuma ya key board kwa Id feki ila ndani kwako wewe ni binadamu tu na una dhamira(consciousness)
Hivi ulishajiuliza kwanini kuna watu ni wagonjwa ila madaktari kwa vipimo vyao hawaoni anaumwa mini? Roho mbaya, kuhukumu, visasi na chuki vinaongoza kuwalaza watu kama wewe kitandani!Ifike hatua Kazi ya kuhukumu tumuachie Mungu!
Nisamehe Sana kama nimekukwaza!
Hujielewi. Tafakari tena. Kuna ujumbe mzito kwenye post yangu usiyoifahafahamu.
 
Hujielewi. Tafakari tena. Kuna ujumbe mzito kwenye post yangu usiyoifahafahamu.
Panya lenyewe pia ni gonjwa la HIV/AIDS. Limevimba mashavu sababu ya ARVs. Ni suala la muda, atamfuata aliyetangulia kwa corona.
Kwamba mkuu wewe una uhakika 100% na afya yako kuwa ni mardhawa, na una uhakika mheshimiwa atakufa kabla wewe hujafa au ujumbe gani mwingine?
 
Wakati Waziri Mkuu akiahirisha Bunge baada ya hotuba ya Waziri Mkuu, Spika Ndugai ameongelea suala la uaminifu wa watanzania hasa kwa vijana na kudai wawekezaji wengi wamekuwa wakilalamika. Ndugai amesema mtu anaeanzisha mradi atajikuta tu amefilisika asipokuwa makini.

'' Mtu akianzisha labda tuseme 'super market' nisikilizie kama bado utamkuta barabarani miaka mitatu ijayo. Ataibiwa pale si kawaida, hata wewe wekeza halafu njoo bungeni hapa umewaachia miezi sita hujawatembelea, subiri siku utakayoenda upige mahesabu, utakuta umepigwa'' Alisema spika Ndugai.



Aliendelea '' Mswahili humuachii shughuli mkakubaliana usipigwe kwa sababu ya uaminifu, sijui namna gani tutafanyia kazi?''

''Kijana akiwa na fursa kama hiyo akaachiwa asimamie biashara asikuibie, wenzake mtaani wanasema mjinga sana yule, alipewa goli liko wazi kaliacha, mjinga kweli! Jamaa mwaka mzima yuko bungeni kule, yeye kakaa tu lakini uaminifu unalipa sana katika maisha'' Alimalizia Spika Ndugai.

Maskini ni maskini tu.
Madini hamuibiwi?
Makato ya Riba ya nchi ni hela ya juu ya misaada mnayopewa na world bank na mikopo fake ya nchi siyo wizi??
Tena wa wazi kabisa.
Ila umeona vijana wa kitanzani??

Ok! Labda umeenda bungeni umewaachaje hao wanao kuuzia??
Anae jua strategies za biashara ni wewe au ni wao??
Lazima waibe sababu hauko serious!!

Km ni wezi.wenzako mbona mabilionea wako mbali kwa kutumia hao hao watanzania mfano
Gula mali
shubash
Mengi
wewe ndo unaibiwa tu unadhani wote!sababu kimeo tu! Unalinda wanyama.
 
Back
Top Bottom