Spika Ndugai: Vyuo vikuu vianze kufundisha Ujasiriamali kama vile vya Kenya vijana wasisubiri ajira ambazo hazipo!

Kweli tuna viongozi!! Wakilinganishwa wanasema sisi ni nchi huru na tuna namna yetu. Wakijilinganisha - wanakosea kujilinganisha!! Tatizo la ajira Kenya halina unafuu wowote kuliko Tanzania!!
 
Kandugai mwili mkubwa, akili kisoda.
 
Mbona yeye mpaka alifikia kumtandika bakora mshindani wake, tena in public, ilimradi tuu arudi bungeni kwenye pesa za bwerere?? Kama ilikuwa siyo woga wa kujiajiri ni nini hasa hicho?

Sent from my TECNO L9 Plus using JamiiForums mobile app
 
Yote sawa,ajira ni kweli hakuna,maana zitatoka wapi?wakati hakuna viwanda?na yale makelele ya Waziri Jafo kutaka kila mkoa uwe na viwanda mia!wenye akili tulijua ni porojo tu,
Sasa,Kwanza serikali inabidi ifute baadhi ya vyeo,Kuna watu wanaitwa maofisa wa maendeleo,wapo kila wilaya,futa kabisa.
Kuna wakurugenzi wa utamaduni kila wilaya,futa,
Wakuu wa mikoa wapungue,mfano mkoa wa Morogoro,Dar,Pwani,weka RC mmoja,
Wilaya zipungue,hatuna haja ya mkuu wa wilaya tuna haja na hospitari,shule,soko,usalama,mfano Dar ibaki na wilaya mbili tu,Ilala,na kinondoni,
Cha muhimu ni Miundombinu tu,na Dar ipo poa.
wizara zipungue ziwe 10 tu,majimbo ya ubunge yawe 75,Kama ilivyokuwa wakati wa Uhuru.
Tupo kipindi Cha sayansi na tekinolojia,hatuitaji Mbunge Aje aongee na sisi ana kwa ana,tutatumia mitandao tu,.
Kwa ufupi Hawa ccm wamefika mwisho hawajuhi wafanye nini kutengeneza ajira zenye kipato kizuri kuanzia laki 6,
 
Somo la ujasiriamali mbona lipo, lakini mbona yeye alikuwa ana Force ubunge Hadi alitaka kumuua mwenzake na rungu kichwani. Yeye ka mfano ajiuzulu ubunge na u speaker aanze ujasiriamali Ili kufundisha vijana kwa mfano
Weee. Nakupia miezi sita tu atakuwa amechakaa mno kama siyo kufa. Unacheza na vya bure anavyokula?
 
Ndugai,Ndugai,ndugai!!!Mungu anakuona.
 
Hii ngoma ni nzito mkuu na ni global issue..sio Tanzania pekee
Ukitaka kuamini nenda
Haiti
Algeria
Senegal
Burkina Faso
Syria
Albania bila kusahau
Afghanistan
Kila mahali tabu tupu! tusione kwamba hii ngoma ni kwa bongo pekee!
Hizo nchi ulizoorodhesha tunafanana na kwa lipi!Idadi ya watu,raslimali,utawala,aina ya siasa zao na yetu au?
Tuseme Ukweli,Magu uongozi umemshinda na ameiharibu na anaendelea kuiharibu Tanzania kwa kasi kubwa huku CCM ikiwa Hoi Taabani na haiwezi tena kumkemea wala kuisimamia serikali.
Uharibifu ni mkubwa kuliko vinavyojengwa.
Tudai Katiba ya Wananchi.
 
Kama tunataka kuondoa tatizo kila wilaya iwe na vyuo viwili vya ufundi na kila kata iwe na shule ya ufundi, tuache kufundisha watoto milima na mito mirefu Africa.
 
Vinaja kukosa kazi ndo dalili za uchumi wa kati!
 
Hivi wakinga,wapemba,wachaga wa rombo etc,
Wamefundishwa ujasiriamali?????

Ova

Sent from my SM-N920T using JamiiForums mobile app
 
Kaka usiunge hoja hapo, Kwanza mimi ninakataaaa katu katu,, kwani ujasiliamali sio paka mtu ende chuo kwani hata ukiwa darasa la Saba lazima utaujuwa ujasiliamali kwahiyo hao wanapoteza malengo tu
 
Kuna kipindi niliwaza tu ianzishwe system mtu akihudumu kwa miaka 10 aachie wengine! Wenye position zenye mishahara 6M+ wao waachie ndani ya miaka mitano tu. Kama wataungana wakafungue biashara wajiendeleze sasa maybe tungepata unafuu!
Hivi hilo wazo lako linawahusu watu wa huko mjengoni pia

Ova

Sent from my SM-N920T using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…