Uchaguzi 2020 Spika Ndugai: Wabunge wa CHADEMA (Viti Maalum) wasipohudhuria mikutano mitatu wamejifukuzisha

Uchaguzi 2020 Spika Ndugai: Wabunge wa CHADEMA (Viti Maalum) wasipohudhuria mikutano mitatu wamejifukuzisha

Kama kweli wewe in mwanaccm kindakindaki tutajie majina ya hao wabunge wa Chadema yaliyotoka Chadema na si yaliyotoka Lumumba.
Wapi nimesema mimi CCM? jifunze kusoma na kuelewa nilichofanya nimenukuu tu maneno ya Spika.
 
Nawewe acha upashkuna. Nataka awataje hao wabunge wa viti maalum wa CHADEMA ambao hawapo bungeni. Na atasemaje ni wabunge wakati hajawaapisha? Mbona wanatubemenda akili hawa CCM? Au anadhani na sisi wananchi ambao wanatuita wanyonge tumeshikiwa akili zetu na Magufuli kama wao/yeye? Period!
Kuwa na akili hata ya kuvukia Bara bara Mimi nimenukuu maneno ya Ndugai tu.
 
Maajabu hayaishi Tanzania!

Si yeye mwenyewe Ndugai alinukuliwa na vyombo vya habari kuwa kutokana na matokeo ya uchaguzi mkuu uliopita, ambapo Chadema imeambulia mbunge mmoja pekee, hakutakuwa na kambi rasmi ya upinzani.............

Sasa tunapomsikia tena Ndugai akidai kuwa wabunge Wa Chadema wasipohudhuria mikutano mitatu mfululizo, watakuwa wamejifukuzisha ubunge, je anawaongelea wabunge wapi hapo?
Watu wa ajabu sana hawa!
 
Watajuta kumtukana Dr. Slaa
Ahh sasa hivi Afya, Elimu, Maji nchi hii chini ya utawala wa CCM linaenda kuzifutilia mbali
Mpaka 2025 Tz inakuwa kama Sydney
Wapinzani walikuwa wanatucheleweshea maendeleo
Au unasemaje kamanda

Ova
 
...huenda CDM wakabadili msimamo ili kupata uhakika wa ruzuku.
Kwenye siasa lolote linaweza kutokea, Ndio maana CCM walichofanya ni kuweka muda mrefu ili kuwachanganya CHADEMA.
 
Ahh sahvi afya,elimu,maji nchi hii chini ya utawala wa ccm linaenda kuzifutilia mbali
Mpk 2025 tz inakuwa kama Sydney
Wapinzani walikuwa wanatucheleweshea maendeleo
Au unasemaje kamanda

Ova
Hayo ni maneno tu kamanda! Kumbukua hapa tuko Afrika
Ahaaahhh
 
Kwani wabunge hao wa CHADEMA ni wapi hasa?

Wale waliochaguliwa na Magufuli na timu yake, au ni Wabunge hasa wanaowawakilisha wananchi kwa tiketi ya chama hicho?

Hapo kwa mtu mwenye fikra pevu hakuna 'mtihani' wowote kwa yeyote.

Kama ni mamluki, inajulikana hizo ndio njia kuu zinazotumiwa na watu hawa; kwani kuna jipya gani tena?

Nikiwaona watu kama Halima Mdee, Ester wawili, akina Henche na baadhi wa aina hiyo kwenye kundi hilo, nitajua miujiza inawezekana sana nchi hii. Nje ya hapo, hakuna lolote la kumshangaza yeyote.
 
Aaah hivo viti maalumu wapeni police why mnawalazimisha CDM kuwapata viti ili mpate tilioni 2 za kutoka nje kwa ajili ya ukuzaji demokrasia.

Punguzeni posho zenu, ongezeni Kodi mfano sukari iuuzwe elf 10 Sukari ni anasa sio lazima, Cement iuuzwe laki moja kwa mfuko, mafuta elf 8 lita hapa tutapata pesa nyingi Sana kuzidi hata hizo tilioni 2 wanazozitegemea
 
Wapi nimesema mimi CCM? jifunze kusoma na kuelewa nilichofanya nimenukuu tu maneno ya Spika.
Jibu swali, ng'ombe, mbuzi na kondoo hufugwa zizi moja lakini hawachanganyiki, hujitenga kulingana na asili zao; Ndivyo na wewe ulivyo hauwezi kunidanganya.
 
Kwani wabunge hao wa CHADEMA ni wapi hasa?

Wale waliochaguliwa na Magufuli na timu yake, au ni wabunge hasa wanaowawakilisha wananchi kwa tiketi ya chama hicho?

Hapo kwa mtu mwenye fikra pevu hakuna 'mtihani' wowote kwa yeyote.

Kama ni mamluki, inajulikana hizo ndio njia kuu zinazotumiwa na watu hawa; kwani kuna jipya gani tena?

Nikiwaona watu kama Halima Mdee, Ester wawili, akina Henche na baadhi wa aina hiyo kwenye kundi hilo, nitajua miujiza inawezekana sana nchi hii. Nje ya hapo, hakuna lolote la kumshangaza yeyote.
Mkuu tuwe watulivu muda ni Mwalimu mzuri Sana, kama iliwezekana kwa Lowassa sitashangaa lolote kutokea....hii ni November mpaka April tutaona mengi.
 
Magufuli atamtua:

Mbatia
Cheyo
Mrema
Lipumba
Sakaya

Kuwa wabunge wa upinzani.

Tulieni muone vituko.
 
Spika wa Bunge Job Ndugai amesema wabunge wa Chadema wasipohudhuria mikutano mitatu ya bunge watakuwa wamejifukuzisha ubunge.

Ndugai amesema mkutano wa wa kwanza ni huu wa pili January na wa tatu April.

My take.
Toka Sasa hadi April ni mbali sana, tutashudia vituko na mgawanyiko mkubwa Sana hapa katika...huu ni mtihani mwingine ndani ya Chadema.
Ndugai ana akili timamu ?
 
Jibu swali, ng'ombe, mbuzi na kondoo hufugwa zizi moja lakini hawachanganyiki, hujitenga kulingana na asili zao; Ndivyo na wewe ulivyo hauwezi kunidanganya.
Nimekuelewa Ng'ombe,Mbuzi na Kondoo hufungwa zizi moja lakini hawachanganyiki...Sasa wewe ni nani kati ya Ng'ombe,Mbuzi ama Kondoo?
 
Back
Top Bottom