Uchaguzi 2020 Spika Ndugai: Wabunge wa CHADEMA (Viti Maalum) wasipohudhuria mikutano mitatu wamejifukuzisha

Uchaguzi 2020 Spika Ndugai: Wabunge wa CHADEMA (Viti Maalum) wasipohudhuria mikutano mitatu wamejifukuzisha

Maajabu hayaishi Tanzania!

Si yeye mwenyewe Ndugai alinukuliwa na vyombo vya habari kuwa kutokana na matokeo ya uchaguzi mkuu uliopita, ambapo CHADEMA imeambulia mbunge mmoja pekee, hakutakuwa na kambi rasmi ya upinzani?

Sasa tunapomsikia tena Ndugai akidai kuwa wabunge Wa CHADEMA wasipohudhuria mikutano mitatu mfululizo, watakuwa wamejifukuzisha ubunge, je anawaongelea wabunge wapi hapo?
Wabunge wa viti maalum
 
Hivi hizo kanuni za kupata viti maalumu zilibadilishwa lini? Maana Zitto alikuwa mmoja bungeni na chama chake hakikupata viti maalumu iweje CDM wapate???
 
Hivi mtu anaetishia kuwafukuza watu ambao hawajawa bado wabunge atasita kweli kuwafukuza wakiwa kweli wabunge?

Amandla...
 
CHADEMA wanatuchezea akili tu.
Wanawachezea akili kivipi!? Au nyie ndiyo mnawachezea akili? Kwa nini muwatake washiriki siasa za kikora? Anyway,wanaweza wakashiriki tu maana utashi wa kisiasa wanao wao. Kwa mkhtadha uliotokea kwenye uchaguzi mpaka wakawafanya wasishiriki bungeni wanazo hoja za kuamua uamuzi huo.
 
Majina wapi! Tuwatambue!

Tusubirie tuone, Aprili siyo mbali.

Everyday is Saturday................................😎
 
Mtachukua tu hizo nafasi, aliyekuwa anazuia kesha lala mbele,
Mbowe anataka pesa kisha azire kwa lipi?
Mwenzake keshaenda kula maisha bila kazi, na mbweadanganyike aone cha mtema kuni.
Hata akina mdee kukaa nje ya bunge ndo kwa heri hiyo.

Nyie washabai humu JF ndo mmesaidia kuangusha chama baada ya kulazimisha Tundu Lisu kupeperusha bendera.
Nani angepeperusha ndiyo angeshinda? Chama kinaangushwa na hao wababe wanaotumia nguvu za dola kusalia madarakani kwa kufanya uchaguzi wenye ghiliba
 
Viongozi wa dini wamefunga ndoa na tawala dhalimu
Kuna magazeti fulani ya dini hutoka mara moja kwa wiki,haya magazeti kumbe ni ya propaganda tu wala hayafuati misingi ya dini na imani yanayojinasibu nayo.Yamekuwa yakiandika maudhui ya kisiasa tu,hasa siasa za upande wa chama tawala.

Hii inaakisi hata viongozi wa dini wapo ambao ni makada wa chama tawala,yaani ni wanasiasa typically japo wapo kwenye dini,mfano hai ni yule askofu aliyegombea ubunge akashinda kwa utatautata na ghiliba nyingi.Sasa kuna kiongozi gani wa kidini atakayejitokeza kukemea uzandiki huu wa siasa za kibabe?
 
Nani angepeperusha ndiyo angeshinda? Chama kinaangushwa na hao wababe wanaotumia nguvu za dola kusalia madarakani kwa kufanya uchaguzi wenye ghiliba
Ni bora nyarandu angepata hata wabunge 5 kuliko huyo msanii
 
Unajifukuzisha kabla hujateuliwa? Ina maana na wale wa Rais kumi kama hatateua mikutamo mitatu watakuwa wamejifukuzisha?
 
Wasipopeleka hao wabunge 19 na Chama kitakufa kweli. Maana huku nje hawana pa kusemea. Walau hao 19 wakaseme huko Bungeni.
Kikifa wewe utakuwa na hasara ngani na wakati lengo kuu la CCM ni kuiua Chadema? kwanini hamshangilii sasa?
 
Ma
Lengo lenu ni kuu upinzani na kweli umekufa, why mnataka tena kuwe na wabunge wa Chadema?
Majigambo yenu yameisha mmerudia kulalamika tena miaka mitano.
Badilisheni sera za vyama vyenu ili viwe taasisi ya kuaminika.
 
Back
Top Bottom