Bila kuwataja kwa majina au chama, Spika Ndugai amesema wabunge wengi waliojitenga wana madeni makubwa hivyo hawaoni tija ya kuendelea kuhudhuria bungeni.
Spika anasema kwa uchunguzi mdogo alioufanya amegundua wabunge hao wana madeni ya ujanja ujanja na wanadhani wanaweza kuyakimbia hivyo ameshaitaarifu serikali iwachukulie hatua.
Ndugai amewataka wabunge wanaohudhuria vikao kutoshtushwa na mahesabu ya madeni waliyopewa na idara ya uhasibu kwani mahesabu hayo yatafanyiwa marekebisho ili wasiondoke Dodoma mikono mitupu.
Source Star tv!
My take; Chadema wanapitia kipindi kigumu makamanda mjiandae kuwachangia
Maendeleo hayana vyama!