Spika Ndugai: Wafanyabiashara wa nchi hii kila siku wanalalamika, mnahitaji kengele gani igongwe?

Spika Ndugai: Wafanyabiashara wa nchi hii kila siku wanalalamika, mnahitaji kengele gani igongwe?

Replica

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2017
Posts
1,681
Reaction score
8,887
Leo spika Job Ndugai amewaapisha wabunge walioteuliwa jana na Rais Samia Suluhu na kuahirisha Bunge kwa ajili ya hafla ya kuwaapisha mawaziri jioni ya leo.

Pamoja na mambo mengine, Spika Ndugai amewaambia mawaziri na mawaziri watarajiwa kwamba Bungeni ndio nyumbani na uwaziri ni matembezi ambayo muda wowote yanaweza kumalizaka na kurudi nyumbani(Bungeni) hivyo wasisahauliane.

Kisha akawaongelea wafanyabiashara na kuwakumbusha mawaziri wanahitaji nini kujua eneo la biashara ni kipaumbele namba moja!

"Mimi nasikia kila siku habari za wafanyabiashara wa nchi hii wakilalamika, kila siku. Hivi waziri wa uwekezaji, viwanda na biashara, fedha na waoendana na hiyo kada ya biashara, mnahitaji kengele gani igongwe kusema kwamba hili eneo ni kipaumbele namba moja" Alihoji spika Ndugai

Pia Spika Ndugai ameziongelea shida za wizara za TAMISEMI, tatizo la dawa MSD na tatizo la upimaji ardhi.

 
Lisu alijipanga kuchafua nchi .

Yani Mkenya PLO Lumumba amejipanga kuitetea Tanzania lakini mzaliwa wa Singida Tundu Lisu anajipanga kuchafua.

Ni aibu kubwa kwa taifa letu

Lakini amegaragazwa ,asante PLO
 
Back
Top Bottom