Spika Ndugai: Wafanyabiashara wa nchi hii kila siku wanalalamika, mnahitaji kengele gani igongwe?

Spika Ndugai: Wafanyabiashara wa nchi hii kila siku wanalalamika, mnahitaji kengele gani igongwe?

Leo spika Job Ndugai amewaapisha wabunge walioteuliwa jana na Rais Samia Suluhu na kuahirisha Bunge kwa ajili ya hafla ya kuwaapisha mawaziri jioni ya leo.

Pamoja na mambo mengine, Spika Ndugai amewaambia mawaziri na mawaziri watarajiwa kwamba Bungeni ndio nyumbani na uwaziri ni matembezi ambayo muda wowote yanaweza kumaliza na kurudi nyumbani(Bungeni) hivyo wasisahauline.

Kisha akawaongelea wafanyabiashara na kuwakumbusha mawaziri wanahitaji nini kujua eneo la biashara ni kipaumbele namba moja!

"Mimi nasikia kila siku habari za wafanyabiashara wa nchi hii wakilalamika, kila siku. Hivi waziri wa uwekezaji, viwanda na biashara, fedha na waoendana na hiyo kada ya biashara, mnahitaji kengele gani igongwe kusema kwamba hili eneo ni kipaumbele namba moja"

Pia Spika Ndugai ameziongelea shida za wizara za TAMISEMI, tatizo la dawa MSD na tatizo la upimaji ardhi.


Akili zinaanza kurudi ,taratibu tutaelewana, haya maneno Ndugai sijui kayaongea KWA kupenda upepo wa mama imeanza kumpitia,
 
Lisu alijipanga kuchafua nchi .

Yani Mkenya PLO Lumumba amejipanga kuitetea Tanzania lakini mzaliwa wa Singida Tundu Lisu anajipanga kuchafua.

Ni aibu kubwa kwa taifa letu

Lakini amegaragazwa ,asante PLO
Naona TL kakuchanganya sana. Uzi huu haumhusu Lisu.
 
Duh! Siku hazigandi, leo Ndugai kawa objective kiasi hicho!!!!!
 
Alikua wapi kusema haya kipindi cha Jiwe??
Dicteta alikua kashikilia akili zake
 
Back
Top Bottom