Spika Tulia Ackson: Mdee na wenzake 18 wako bungeni kihalali, aeleza kuhusu kurejea kwa Bunge LIVE!

Spika Tulia Ackson: Mdee na wenzake 18 wako bungeni kihalali, aeleza kuhusu kurejea kwa Bunge LIVE!

Total rubbish, wewe ukihukumia kifungo miaka 4 jela ukakata rufaa hutatumikia kifungo chako mpaka rufaa yako isikilizwe?
Wewe ndio hamnazo kabisa. Kisheria si kila rufaa hufanya maamuzi ya awali yabaki. Nikupe mfano: mtu akikushtaki umechukua shamba lake, akashinda, halafu wewe ukakata rufaa, Je anaweza kuja kulima kwenye shamba kwa sababu tu alishinda kesi ya awali? Kijana, husiwe mbumbumbu wa sheria
 
Binafsi naona waachwe waendelee, nao wale mema ya nchi. Maana tukitafuta uhalali wa wabunge mule ndani wanaweza wasifike 50. Wengi ni kazi haramu ya mwendazake! Huu ulimwengu wa tatu ni changamoto sana.

YESU NI BWANA.
Comment yako nimeipenda Sana. Unachosema ni kwamba hata spika mwenyewe ubunge wake una uharamu, hakupita kihalali. Kwahiyo wabunge wengi ni haramu. Why uharamu wa Mdee uwe issue???
 
Bunge zima sidhani kama kuna mbunge halali hata mmoja akiwepo supika mwenyewe
 
Binafsi naona waachwe waendelee, nao wale mema ya nchi. Maana tukitafuta uhalali wa wabunge mule ndani wanaweza wasifike 50. Wengi ni kazi haramu ya mwendazake! Huu ulimwengu wa tatu ni changamoto sana.

YESU NI BWANA.
Amiina baba[emoji120][emoji120][emoji120]
 
Wewe ndio hamnazo kabisa. Kisheria si kila rufaa hufanya maamuzi ya awali yabaki. Nikupe mfano: mtu akikushtaki umechukua shamba lake, akashinda, halafu wewe ukakata rufaa, Je anaweza kuja kulima kwenye shamba kwa sababu tu alishinda kesi ya awali? Kijana, husiwe mbumbumbu wa sheria
Utakuwa mpuuzi sn, kesi ya shamba ina mazingira yake
 
..Mnyika alishaandika barua kwa Spika kwamba Chadema imewafuta uanachama Halima na wenzake.

..Sheria inaelekeza kwamba mbunge aliyetokana na chama akifukuzwa ktk chama chake anapoteza sifa ya ubunge.

..Kwa hiyo anayetakiwa kutoa maelezo ya uhalali wa ubunge wa kina Halima ni Spika, na sio Mnyika.

..Spika anatakiwa aeleze sheria inayompa mamlaka ya kuendelea kuwakubali watu wasio na chama bungeni.

..Zaidi, vyombo vya DOLA vilitakiwa kuchunguza Halima na wenzake wamefika vipi bungeni kwani Chadema wanadai hawajawahi kufanya kikao cha kuteua wabunge wa viti maalum.
Hata yeye anajua vizuri sn kuwa Halima na genge lake siyo wabunge
 
Wabunge hawa feki ni matokeo ya matumizi mabaya ya madaraka yaliyofanywa na Mwendazake. That man was evil!
Lakini licha ya mtu mmoja kufanya mambo kinyume na sheria,mbona watu wale waliokuwa vigogo katika serikali yake na chama chake Bungeni hata Chief Justice hawakuikosoa au kulaani kitendo hicho.
Mimi nadhani katika miaka 60 ya uhuru tumeshindwa kujitambua kama Taifa.
Hata hii katiba mpya wapo watu wazito wanaodai katiba mpya sio muhimu.Lakini leo Mama SSH akiamua twende na katiba mpya watu hao hao wataweka korasi kubwa bila aibu wakiunga mkono.
Adui no.1 Tanzania ni uwogo uliozaa unafiki.
 
Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson akizungumza na Wahariri wa Vyombo vya Habari. leo Februari 14, 2022 ameeleza kuwa Mdee na wenzake 18 wako bungeni kihalali:

“Uharamu haupo kwasababu hawezi kuwa haramu halafu akawepo mule ndani. Nchi yetu inaendeshwa Kidemokrasia na Kisheria. Jambo moja tu linalosubiriwa ni watu kumaliza michakato yao inayohusika.

“Jambo moja linalosubiliwa ni kumaliza michakato yao inayohusika ndani ya chama. Katiba yetu inasema mbunge lazima awe mwanachama, kwa hiyo wakimaliza wakaleta taarifa tutachukua hatua.”

Kuhusu mpango wa kurejesha Bunge live, Tulia amejibu: “Hili ni jambo ambalo linazungumzika, wacha tuone sababu zilizolifanya kuondolewa. Tutazungumza na Waziri wa habari kuona nini cha kufanya.”
 
Back
Top Bottom