Chadema kisipobadilika kimtizamo na kiharakati basi itakua ni hatari sana kuwa na Chama Tawala chenye hulka hiyo. Ni nafuu kidogo Kwa CCM mana ni vyama vingi ndani ya Chama kimoja Cha Kijamaa feki .
CCM ina upinzani wa ndani Kwa ndani Tangu kilipoundwa,na kinafanya mabadiliko ya kiini macho mara Kwa mara. CCM inatawala na itaendelea kutawala mana inajua kucheza na akili ndogo za watanzania wengi na pia akili kubwa za wachache Kwa kuwapa fursa za kula nchi mpaka kuvimbiwa.
CCM inacheza na ukabila,CCM inacheza na Udini ,CCM inacheza na ujana ,CCM inacheza na jinsia ,CCM inacheza na Matajiri ,CCM inacheza na maskini. Ni ngumu sana Kwa siasa za upinzani kuiangusha CCM.
Kwa mfano suala la Kina Mdee lilikua ni suala dogo sana. Walipaswa kulishughulikia Kwa misingi yote ya Utawala Bora na Demokrasia.
Chadema ni Chama chenye udikteta mbaya kuliko ule wa Magufuli.
Wale akina mama walitoa udhuru kuwa Wapewe muda wa kujitetea na kusikilizwa . Kwani palikua na tatizo Gani kuwasikiliza ?
Mpaka Sasa wale ni washindi kwenye Misheni yao. Wamefanikiwa kuihadaa Serikali na wanapata mapesa Mengi kuliko hiyo misaada waliyotegemea kuipata Kutoka na bunge la vyama vingi.
Hili ni tatizo kubwa Kwa Watawala kufanya matumizi makubwa kuliko pato halisi la nchi. Chadema mpaka Sasa wameshindwa kusikiliza rufaa yao na kuitolea majibu na kupeleka Taarifa rasmi bungeni Tena mbele ya vyombo vya habari na kuonyesha barua hiyo Kwa wazi.
Chadema ni Chama kibaya kinachopendwa kama ilivyo CCM. Ni hulka ya Watanzania wanapenda kitu kishabiki. Chadema hakijajua kuwa kinafanya makosa Mengi sana ya kiufundi wakitegemea kutumia timua timua kuendesha Chama.
Waarabu walifanikiwa kuingia Afrika ya Kaskazini na kuifanya kuwa kama sehemu yao Kwa kuoa Wanawake wa Kiafrika na kubadili kizazi Cha waafrika na mwishowe waarabu kuwa wengi.
Kuna wakati unaweza kupambana na adui yake Kwa akili TU na ukamshinda bila kutumia nguvu. Chadema muda wote wanatumia ubabe kupambana na wababe wenye Dola , CCM.
Fungueni Kesi ya Kikatiba kupinga Hao Wabunge feki kukaa bungeni! Hukumu ikitoka hata 2030 ipo siku waliohusika watafikishwa mahakamani Kwa uhujumu uchumi mana wametumia mabilioni ya walipa tozo huku mafuta,sukari, Kodi , vifaa vya ujenzi n.k. Vikizidi kupanda bei. Watu wameoneana Muhali na kuruhusu mabilioni ya fedha za umma kupotea bila sababu wakati ambapo Vijana wengi wapo mitaani bila ajira.
Hukumu ikitoka kwamba katiba ilikiukwa Iko siku watu watakimbia kimbia na kujificha. Vinginevyo Chadema hawana uhakika Wala matumaini ya kushika Dola siku Moja.
Vinginevyo Chama kiwasamehe ili wafanye siasa kama kawaida na Sauti ya upinzani isikike bungeni Kwa uchache wake na vurugu zao zianze upya. 2025 wawapige cheni kwenye kura za maoni ndani ya Chama. Wawaache waendelee na Ubunge wao kihalali lakini wawavue uongozi ndani ya Chama.
CCM hua hakipotezagi muda mrefu kushambulia mtu lakini chadema miaka nenda Rudi kinaweza kuendeleza malumbano tu hata kama hayana tija yoyote. Kuna watu walikimbilia CCM Kwa tamaa ya madaraka na uteuzi kutokana na ugumu wa maisha. Mbowe alitakiwa awaambie Vijana wake wasipoteze muda kuwatukana na kuwadhalilisha kwenye mitandao.
Hao hao Huko ndani ya CCM ndio wangetumika kuibamoa CCM na kutoa Siri za ndani lakini badala yake ni matusi na kejeli mpaka wanageuka na kuwa wabaya zaidi.
Bunge linataka kujua kuwa utaratibu wa kufukuzwa kwao umefuatwa Kwa misingi ya Katiba ya Chama kinachojiita Cha kidemokrasia.
Hivi vyama vyote vya Kiafrika ni vya ajabu sana kwenye Demokrasia ya ndani matokeo yake vikiingia madarakani vinakuwa vya hovyo kabisa. Demokrasia hua haidanganyi ,mtu anayefaa hata iweje atashinda TU hata Kwa kura Moja. Uongozi ni karama. mfano hata kama pangekua na kampeni na uwazi kiasi Gani Sumaye asingemshinda Mbowe. Lakini figisu figisu na hofu vikasababisha uchaguzi kuwa wa kisanii usio na uhuru Wala usawa na haki.