Spika Tulia Ackson: Mdee na wenzake 18 wako bungeni kihalali, aeleza kuhusu kurejea kwa Bunge LIVE!

Spika Tulia Ackson: Mdee na wenzake 18 wako bungeni kihalali, aeleza kuhusu kurejea kwa Bunge LIVE!

Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson akizungumza na Wahariri wa Vyombo vya Habari. leo Februari 14, 2022 ameeleza kuwa Mdee na wenzake 18 wako bungeni kihalali:

“Uharamu haupo kwasababu hawezi kuwa haramu halafu akawepo mule ndani. Nchi yetu inaendeshwa Kidemokrasia na Kisheria. Jambo moja tu linalosubiriwa ni watu kumaliza michakato yao inayohusika.

“Jambo moja linalosubiliwa ni kumaliza michakato yao inayohusika ndani ya chama. Katiba yetu inasema mbunge lazima awe mwanachama, kwa hiyo wakimaliza wakaleta taarifa tutachukua hatua.”

Kuhusu mpango wa kurejesha Bunge live, Tulia amejibu: “Hili ni jambo ambalo linazungumzika, wacha tuone sababu zilizolifanya kuondolewa. Tutazungumza na Waziri wa habari kuona nini cha kufanya.”
Mhu! Ngoja nitasoma tena siku ingine.
 
wale walishafukuza uanachama (kwa mujibu wa katiba hawastaili kuwa bungeni ili hata spika mstaafu Mzee Msekwa alishaliongelea) suala la wao kukata rufaa ni maana yake wanataka warudishwe uanachama wao.
Hivi Sabaya alivyofunga miaka 30 ameamua kukata rufaa kwa hiyo maana yake sio mfungwa.
Jurisprudence inaelekeza kwamba unapokata rufaa ni kwamba hukumu iliyotolewa inaendelea kusimama hadi hapo rufaa yako itakaposikilizwa
Pamoja na ulioyasema, nadhani hoja ya msingi ni je utaratibu ulifuatwa hadi Spika akawatambua. Kuna barua yeyote kutoka Chadema na Tume ya Uchaguzi ikiwatambukisha kama wao ni chaguo la chama chama chao? Mnyika ameioomba hii kwa muda mrefu sasa lakini hajajibiwa.

Anachokisema Spika ni kuwa yeye ana mamlaka ya kumpa ubunge mwanachama yeyote wa chama chochote bila kujali kama chama chake kinamkubali au la. Kwa msingi huo anaweza kuamka kesho akamuapisha Catherine Ruge kuwa mbunge bila kuulizwa na mtu! Au Pambalu bila kuulizwa. Asitufanye sisi wajinga kwa kujificha kwenye suala la uanachama.

Hawa wakina mama hata wakisamehewa na Chadema na kurudishwa kwenye chama chao bado ubunge wao utakuwa haramu. Anae takiwa kuwajibika katika suala lao ni Spika na sio Chadema. Strategy ya CDM ya kuwapuuza ni nzuri sana maana kila siku inayoenda wanazidi kukosa legitimacy. Sasa hivi hakuna mtu ( isipokuwa wafuasi wa Chama kinachowakingia kifua) hawawasikilizi tena. Halima, Ester, Ester walijijengea heshima kubwa kama wapiganiaji wa haki za watanzania bila kujali gharama watakayolipa. Leo wamegeuka wagonga meza tu bungeni na watu wa kubezwa na mbunge yeyote anayejisikia. Mchango mkubwa wa Halima ninaoojua ni ule wa kutaka tiba mbadala za Covid zipewe umuhimu. Hata alipojikakamua kumuongelea Mbowe aliongea kwa uoga na ikapokelewa kwa dhihaka. Gharama wanayolipa ni kubwa mno.

Amandla...
 
Hilo Bunge live Wala hatulihitaji!Je,sababu zilizotajwa wakati wanaliondoa kuwa live zimepatiwa ufumbuzi?
 
sasa si waende huko mahakamani kwa mujibu wa katiba ya chadema wameshafukuzwa uanachama na wamekata rufaa baraza kuu,
Hawa hadi sasa sio wanachama wa chadema
Huu ni uvunjwaji wa katiba ulio zahiri
Huyu bi msumali anajifurahisha
Baraza bado halijawaita maana lilisema mwakajana lilishindwa kufanya mkutano kwa sababu ya ukata, sasa wao wafanye nini zaidi ya kuendelea kusubiri waitwe! Wao wanasubiri waitwe wakajitetee na Baraza lina ukata, sasa watatokaje bungeni na wakati hata hilo baraza likiridhiawatakimbilia mahakamani, kama ambavyo Zitto Kabwe alifanya alupofukuzwa na Chadema.

Na aliebdelea kuwa Mbunge hadi mahakama ilipotoa hukumu, na itoa hukumu katika mkutano wa mwisho wa bunge hivyo kupelekea Zitto kupewa haki zake za miaka mitano kama wabunge wengine licha ya hukumu kumuona ana hatia.

Na hawa watakwenda kwa mchezo huo huo, usione wako kimya wanajua hatua za kufuata! Huu ni wakati wa masika jamani, twende mashambanii!!!
 
Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson akizungumza na Wahariri wa Vyombo vya Habari. leo Februari 14, 2022 ameeleza kuwa Mdee na wenzake 18 wako bungeni kihalali:

“Uharamu haupo kwasababu hawezi kuwa haramu halafu akawepo mule ndani. Nchi yetu inaendeshwa Kidemokrasia na Kisheria. Jambo moja tu linalosubiriwa ni watu kumaliza michakato yao inayohusika.

“Jambo moja linalosubiliwa ni kumaliza michakato yao inayohusika ndani ya chama. Katiba yetu inasema mbunge lazima awe mwanachama, kwa hiyo wakimaliza wakaleta taarifa tutachukua hatua.”

Kuhusu mpango wa kurejesha Bunge live, Tulia amejibu: “Hili ni jambo ambalo linazungumzika, wacha tuone sababu zilizolifanya kuondolewa. Tutazungumza na Waziri wa habari kuona nini cha kufanya.”
Huyu na naye hanatofauti na ndugai hilo mbona linajulikana mapema walibariki wote na dikteta mwendazake huo uharamia, labda anataka michakato toka ndani ya ccm maana ndyo wanaoamua maisha ya walalahoi
 
Waachwe tu, muda wenyewe upo ukingoni kumalizika!

Huo sio mjadala tena.

Wenye Akili zao timamu tayari waliisha iona fulsa,zingine ni kelele tu.
 
Moja ya sababu kuliondoa Bunge kuwa live ni watu kutofanya kazi na kuangalia Bunge!
Suala lingine ni gharama kubwa kwenda live!
Je,hayo yamepatiwa ufumbuzi?Labda Hilo la kwanza,Kwa Bunge hili sioni mtu akiacha shughuli zake na kuangalia Bunge!
 
Binafsi naona waachwe waendelee, nao wale mema ya nchi. Maana tukitafuta uhalali wa wabunge mule ndani wanaweza wasifike 50. Wengi ni kazi haramu ya mwendazake! Huu ulimwengu wa tatu ni changamoto sana.


YESU NI BWANA.
Duh !!?
 
Tumeelewa
Naomba Mungu afanye muujiza tuamke kesho iwe 2024 tuanze kampeni ya kufa mtu
Hizi ngonjera za bunge bungulele zifikie kikomo tuheshimiane
 
Nchi ya hovyoo sana hii, yaani huyu ndio alikuwa pale shule ya Sheria udsm??.

Etiii wanasubiri michakato yao ndani ya chama kipi?, Cdm walikataa hawa sio wanachama wao. Mambo mengine sio hata yakusema mbele za watu.
 
Baraza bado halijawaita maana lilisema mwakajana lilishindwa kufanya mkutano kwa sababu ya ukata, sasa wao wafanye nini zaidi ya kuendelea kusubiri waitwe! Wao wanasubiri waitwe wakajitetee na Baraza lina ukata, sasa watatokaje bungeni na wakati hata hilo baraza likiridhiawatakimbilia mahakamani, kama ambavyo Zitto Kabwe alifanya alupofukuzwa na Chadema. Na aliebdelea kuwa Mbunge hadi mahakama ilipotoa hukumu, na itoa hukumu katika mkutano wa mwisho wa bunge hivyo kupelekea Zitto kupewa haki zake za miaka mitano kama wabunge wengine licha ya hukumu kumuona ana hatia. Na hawa watakwenda kwa mchezo huo huo, usione wako kimya wanajua hatua za kufuata! Huu ni wakati wa masika jamani, twende mashambanii!!!
Suala hapa si uanachama wao. Suala ni taratibu zilizopelekea wao kuwa wabunge. Hata kama Baraza litawasema wao ni wanachama bado hawatakuwa na haki ya kukaa bungeni kwa sababu taratibu hazikufuatwa.

Ila kwa Spika wetu suala la uanachama halina maana. Kuna mbunge alijivua uanachama, akajiunga chama kingine lakini Spika akamuita aende bungeni kuwakilisha chama ambacho aliishajitoa. Jamaa akawa bungeni akiwakilisha Chadema akiwa mwanachama wa CCM!

Suala la uanachama wa wakina Halima lisipewe uzito wowote. Spika abanwe kwa kukiuka taratibu za utambuzi wa wabunge wa viti maalum.

Amandla...
 
Back
Top Bottom