Spika Tulia amburuza Luhaga Mpina Kamati ya Maadili

Spika Tulia amburuza Luhaga Mpina Kamati ya Maadili

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610
Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson ameelekeza Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kumhoji mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina kwa madai ya utovu wa nidhamu.

Akitangaza uamuzi huo bungeni jijini Dodoma leo Jumanne, Juni 18, 2024 Dk Tulia amesema kuwa Mpina amedharau mamlaka ya Spika na Bunge kwa kufanya vitendo vya utovu wa nidhamu.

Awali, Mpina alipewa wiki moja kuwasilisha ushahidi wake baada ya kulieleza Bunge kuwa Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe amelidanganya bunge katika sakata la uagizaji wa sukari.

PIA SOMA
- Luhanga Mpina apewa siku 10 na Spika kuleta ushahidi wa Bashe kulidanganya Bunge

- Luhaga Mpina: Usambazaji wa sukari haukuwa ukifanywa na mfanyabiashara mmoja wa Mwanza pekee, Waziri Bashe alidanganya

- Luhaga Mpina amshukia Waziri Bashe, adai amelidanganya Bunge, awataja Magufuli, Rais Samia

- LIVE - Bunge lajadili juu ya adhabu ya Mbunge Luhaga Mpina

- Mpina afunguka, asema Kifungu kilichotumiwa na Spika Tulia kumtuhumu na kumhukumu hakipo!

- Mpina kuwapelea Mahakamani Waziri Bashe na Bodi ya Sukari kwa kutoa idhini ya vibali vya kuagiza sukari kinyume cha Sheria
 
Tulia anataka kunasa kwenye mtego mbovu.

Alitakiwa alimilize hili jambo kwa waziri kuachia ngazi na maisha yaendelee.
Sasa chupika alimtaka Mpinga alete majibu Kwa Bunge na raia tukasikia, sasa majibu ya Mpinga mbona yenyewe anataka yawe Siri. Na raia tusijue.
 
Speaker anaanza kutumia madaraka yake vibaya, halafu trick yao moja wote kujaribu kuwapa hekaheka watu wanaojaribu kufichua uovu.

Kazi ya mbunge ni kuisimamia serikali yeye speaker anadhani wabunge wapo pale kufanya maigizo.

Nyaraka za Mpina zinakuwaje taarifa zilizotayarishwa na bunge, huyu nae mtu hovyo kweli.
 
Speaker anaanza kutumia madaraka yake vibaya, halafu trick yao moja wote kujaribu kuwapa hekaheka watu wanaojaribu kufichua uovu.

Kazi ya mmbunge ni kuisimamia serikali yeye speaker anadhani wabunge wapo pale kufanya maigizo.

Nyaraka za Mpina zinakuwaje taarifa zilizotayarishwa na bunge, huyu Betina nae mtu hovyo kweli.
Hadi sasa wabunge wako na Mpina. Taarifa ziko kama ile wabunge wako kimya mawaziri ndio wanapiga makofi kilejaleja.. nimeona Mwigulu nae akipiga makofi ..Mpina asurubiwe.

Sipika anajiliwaza tu huku kura za CCM zikiwayawaya.
 
Hadi sasa wabunge wako na Mpina.

Sipika anajiliwaza tu huku kura za CCM zikiwayawaya.
Wabunge wa CCM awaaminiki wanaendeshwa kwa utamaduni wa ‘carrot on the stick’ hao sio watu wakuwategemea kabisa katika kupinga ufisadi.

Wananchi wako na Mpina, speaker anataka kuanza vitisho. Badala ya waziri kujibu tuhuma, speaker analeta hadithi za kamati ya maadili na haki.

Na ushahidi wa Mpina anadai ni taarifa za bunge zimęachiwa public kabla ya kusikilizwa, eti amemvunjia heshima yeye kama speaker,

Huyu speaker ameanza kulewa madaraka, anataka wabunge wengine waogope kuisimamia serikali. Taarifa za Mpina ni mali yake sio za bunge.
 
Mbunge anawajibika kwa Bunge (spika) na wananchi ambao ndio waajiri wake, kwahiyo si kosa kupeleka ripoti bungeni halafu akaileta kwa wananchi (waajiri) wake, 🤣🤣 haya mambo ya kufanya maamuzi kwa kificho ndio yanasababisha upigaji uendelee
 
Nilidhani TAKUKURU na polisi wangechukua point 3 za ugenini chapu chapu kwenye hili sakata kwa kumuhoji mtuhumiwa kama wafanyavyo kwenye kesi zingine mtu akituhumiwa tuu wanaruka nae ushahidi unakuja baadae lakini mtoa tuhuma ndio ana wajibishwa tena 🤔🤔
 
Mtu anayesaidia kufichua uovu, anaambiwa mtovu wa nidhamu. Mmeona tulipofikia? Kuanzia spika and co. wanajiona miungu watu.

Mpina pekee hatoshi kupambana na hawa maharamia. Watanzania hatubebeki, ilitakiwa tumpe sapoti shujaa wetu.

Kungekuwa na mgombea binafsi wa Uraisi, Mpina ningemfanyia kampeni nchi nzima. Hivi tunashindwa nini kwenda bungeni tukampe kashikashi spika akili imkae sawa.
 
Mbunge anawajibika kwa Bunge (spika) na wananchi ambao ndio waajiri wake, kwahiyo si kosa kupeleka ripoti bungeni halafu akaileta kwa wananchi (waajiri) wake, 🤣🤣 haya mambo ya kufanya maamuzi kwa kificho ndio yanasababisha upigaji uendelee
Hata akitumia hiyo kanuni aliyoisoma, kuna kitu ame overlook na hapo watu walitarajia lazima atanasa, na amenasa kweli.

Vita ya 2025 watu wameshaanza kufanya usafi.
 
Back
Top Bottom