Ukimsikiliza hadi mwisho, ni kama ameuruka huo mtego na kuwarushia Kamati ya Bunge wachafuke mikono wentewe.
Muda wote aliokuwa akifanya uwasilishaji sauti yake ilitawaliwa na kitetemeshi, kitetemeshi hicho kilianza kwa kujificha, lakini kila alipoendelea kilisikika dhahiri.
Hapo kuna pande mbili, upande mmoja Serikali na upande mwingine ni Mpina.
Cha kushangaza Spika akijua hili swala lipo mezani na bunge linashughulikia anasikika kwa sauti yenye kitetemeshi kikali akiishukuru serikali. Hapo tayari Mpina ameshanyingwa.