Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson ameelekeza Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kumhoji mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina kwa madai ya utovu wa nidhamu.
Akitangaza uamuzi huo bungeni jijini Dodoma leo Jumanne, Juni 18, 2024 Dk Tulia amesema kuwa Mpina amedharau mamlaka ya Spika na Bunge kwa kufanya vitendo vya utovu wa nidhamu.
Awali, Mpina alipewa wiki moja kuwasilisha ushahidi wake baada ya kulieleza Bunge kuwa Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe amelidanganya bunge katika sakata la uagizaji wa sukari.
OPEC ya kufilisi nchi, na raia tukiendelea na uzezeta wetu huenda wajukuu wetu wataikuta nchi imeisha. Hawa jamaa wanapiga nchi bila kujali kama kuna Kesho na wanalindana vibaya
Hadi sasa wabunge wako na Mpina. Taarifa ziko kama ile wabunge wako kimya mawaziri ndio wanapiga makofi kilejaleja.. nimeona Mwigulu nae akipiga makofi ..Mpina asurubiwe.
Sipika anajiliwaza tu huku kura za CCM zikiwayawaya.
Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson ameelekeza Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kumhoji mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina kwa madai ya utovu wa nidhamu...
Mbunge anawajibika kwa Bunge (spika) na wananchi ambao ndio waajiri wake, kwahiyo si kosa kupeleka ripoti bungeni halafu akaileta kwa wananchi (waajiri) wake, 🤣🤣 haya mambo ya kufanya maamuzi kwa kificho ndio yanasababisha upigaji uendelee
Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson ameelekeza Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kumhoji mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina kwa madai ya utovu wa nidhamu...
Nilidhani TAKUKURU na polisi wangechukua point 3 za ugenini chapu chapu kwenye hili sakata kwa kumuhoji mtuhumiwa kama wafanyavyo kwenye kesi zingine mtu akituhumiwa tuu wanaruka nae ushahidi unakuja baadae lakini mtoa tuhuma ndio ana wajibishwa tena 🤔🤔
Mtu anayesaidia kufichua uovu, anaambiwa mtovu wa nidhamu. Mmeona tulipofikia? Kuanzia spika and co. wanajiona miungu watu.
Mpina pekee hatoshi kupambana na hawa maharamia. Watanzania hatubebeki, ilitakiwa tumpe sapoti shujaa wetu.
Kungekuwa na mgombea binafsi wa Uraisi, Mpina ningemfanyia kampeni nchi nzima. Hivi tunashindwa nini kwenda bungeni tukampe kashikashi spika akili imkae sawa.
Mbunge anawajibika kwa Bunge (spika) na wananchi ambao ndio waajiri wake, kwahiyo si kosa kupeleka ripoti bungeni halafu akaileta kwa wananchi (waajiri) wake, 🤣🤣 haya mambo ya kufanya maamuzi kwa kificho ndio yanasababisha upigaji uendelee
Speaker huyu… yaani mbunge anampelekea ushahidi speaker Kama alivyotakiwa na yeye kufanya hivyo na pia kuwaambia wapiga kura wake ni nini alichowasilishia imekuwa utovu wa nidhamu…? Bado safari ni ndefu.