Spika Tulia: Wapinga uwekezaji bandarini waangushiwa kitu kizito. Wanaosema watahamasisha watu wasilipe kodi, wajaribishe waone

Spika Tulia: Wapinga uwekezaji bandarini waangushiwa kitu kizito. Wanaosema watahamasisha watu wasilipe kodi, wajaribishe waone

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Joined
Dec 11, 2012
Posts
6,067
Reaction score
10,938
"Leo (jana) hukumu ya kupinga mkataba wa bandari imetoka lakini kabla haijatoka nilishafanya mikutano kadhaa nikawaambia wana-Mbeya mjini bandari haijauzwa nikawaambia nchi haijauzwa mtu akikuambia bandari imeuzwa mwambie shilingi ngapi?? Akishindwa kukuambia chaliiii!!! maana leo (jana) watu wameangushiwa kitu kizito, sasa wameelewa na wewe mwana-Mbeya mjini unielewe Mbunge wako"....

"Nilisema hivii na nina sema tena huo wanaoita mkataba yanayoitwa makubaliano sio wao pekee yao wanaosoma na sisi wengine tumesoma kama wao, na sisi pia tunaelewa, sasa kuna watu huku 'kitaa' wakajifanya wao ndio mabega makubwa nini! wakaanza kuongea ooh! spika haelewi, bunge halielewi kila mtu haelewi yeye ndio anaelewa sana! Juzi nikajifunza kumbe huyu ni 'hamnazo' yaani kuna watu ni 'hamnazo' yaani wewe unawaza umesoma sheria kuliko mimi? kama ni ile karatasi wote tumesoma sasa wewe ndio unaumiliki wauelewa, unaumiliki wa maarifa? Umeutoa wapi? Tuheshimiane...

"Kabla hujafikia kwenye uwakili unasoma kwanza uwe mwanasheria, mimi nilikuwa mwalimu wa wanasheria na baadae nikawa mwalimu wa mawakili wasomi"


"Hukumu imetoka leo (jana) sasa bado wanapita huko, na nilimuona mwingine eti anawauliza wananchi wanaokubali mkataba wa milele mimi nikawaza nikasema hawa wanaakili kweli? Kuna umilele kwenye hoja ipi ? Sasa mahakama imetoa ufafanuzi mikutano yao ya leo (jana) sijui watakuwa wanaeleza nini?

Nikasikia hao wazee 'wakupuyanga' eti wametangaza ooh tutaandamana ...embu nione mkono wa mtu anayetaka maandamano hapa ? Hakuna... Mbeya mjini tunataka maendeleo na wakija hapa kuhamasisha (maandamano) muwakatae, wakatae kwa sababu atakaye vunjwa mguu ni wewe na sio wao, wakatae kwa sababu wewe unataka Maendeleo umenituma Mbunge wako nikayapiganie na ninayapigania"....

"Wao wanasema watahamasisha watu wasilipe kodi wajaribishe waone.... Mahakama msema haki, mtoa haki kashamaliza, hii ni mahakama kuu bwana wewe nenda unakotaka kwenda, tena hii sio mahakama kuu ya kawaida hii ni mahakama ambayo ni ya kikatiba kwa hiyo ingeweza kuitwa Mahakama ya Katiba au ya Kikatiba ndio imefanya huo ufafanuzi.


Wana-Mbeya mjini niwatoe wasiwasi hizi fedha nyingi tunazozitaja tunataka Serikali ituletee"
 
Wapingaji na wateteaji wote wanahoja, kuwa wasiwasi na mali zako sio kitu mbaya, kuwa na hofu juu ya mali za UMMA sio mbaya, hii Nchi tuna mifano mingi sana ya kupigwa wala sina haja ya kuiweka hapa, Mahakama imetoa uamuzi, tuuheshimu, ila wakati utatuambia huko mbele ya safari, kama kitu kizito kimewaangukia wapingaji au kimeangukia Watanzania wote.
Ijumaa njema wadau wa JF.
 
Wapingaji na wateteaji wote wanahoja, kuwa wasiwasi na mali zako sio kitu mbaya, kuwa na hofu juu ya mali za UMMA sio mbaya, hii Nchi tuna mifano mingi sana ya kupigwa wala sina haja ya kuiweka hapa, Mahakama imetoa uamuzi, tuuheshimu, ila wakati utatuambia huko mbele ya safari, kama kitu kizito kimewaangukia wapingaji au kimeangukia Watanzania wote.
Ijumaa njema wadau wa JF.
Kwani Bandari inapelekwa wapi?
 
Duh......😂😂😂

Tanzania Assembly of God
Anatuaibisha sana.Sijui kwanini kabla hawajawa watu wakuu sana wanakuwa loyal na role model lakini kuna ngazi wakifika Uchamungu wao unakuwa kama umemezwa.Nawafahamu wa TAG kadhaa waliokuwa role model baada ya kuingia kwenye siasa na kupata nyadhifa wamekuwa watu hatari kuliko wapagani mara nyingine.Kwakweli ni aibu.

Watu waliopaswa kuwa na hofu ya Mungu,wenye hekima,wenye maneno yaliyojaa kweli tupu na dhamira njema ikiwaongoza.Mwenyehaki anatarajiwa awe kioo.Tofauti na wasiomjua Mungu.
Well hatakama mtazamo labda yuko sawa,labda lakini maneno mbona hayana ladha ya mtu anayemjua Mungu.

John siasa inaweza kukupotezea heshima yako watu waliokuwa wanakuamini wakabaki wanashangaa.
 
Hivi kwa hali hiyo inawezekanaje mtu kama huyo akawa spika wa bunge? Tumeona athari za hiyo misimamo yake kuhusu hili suala la bandari kule bungeni.

Sijui kwa nini hatupo serious kama nchi?
 
Back
Top Bottom