Huyu ni Spika wa Bunge la Gabon alipokuwa anataka kutoroka leo hii asubuhi, Agosti 31, 2023.
Ukiona viongozi tuliowaamini wanasaini mkataba mbovu kama DPW ujue nyuma yake kuna mambo kama haya!
Video inayodaiwa kumuonesha Spika wa Bunge akiwa amekamatwa na Mabegi ya fedha akitoroka
Ukiona viongozi tuliowaamini wanasaini mkataba mbovu kama DPW ujue nyuma yake kuna mambo kama haya!
Video inayodaiwa kumuonesha Spika wa Bunge akiwa amekamatwa na Mabegi ya fedha akitoroka
- Tunachokijua
- Agosti 30, 2023, Rais Ali Bongo aliyekaa madarakani kwa miaka 14 nchini Gabon aliwekwa kizuizini na Jeshi la Nchi hiyo muda mfupi baada ya Jeshi kutangaza kuwa halikubaliani na matokeo ya Urais na hivyo linayafuta pamoja na kuwaondoa kazini Viongozi wa Taasisi zote za Umma.
Wengine waliokamatwa ni Mtoto wa Rais, ambaye ni Mshauri wake wa karibu, Noureddin Bongo Valentin, Katibu Mkuu Kiongozi, Makamu wa Rais, Washauri wengine wa Rais na Maafisa Wakuu wa Chama Tawala cha PDG.
Kwa mujibu wa Jeshi, Viongozi hao wanatuhumiwa kwa Uhaini, Ubadhirifu, Rushwa na Kughushi Saini ya Rais na tuhuma nyingine. Mapinduzi haya yatakuwa yanamaliza Utawala wa familia ya Bongo iliyotawala Nchi hiyo kwa zaidi ya miaka 55.
Madai ya viongozi wa Serikali kuanza kutoroka Gabon baada ya Mapinduzi
Baada ya kutokea kwa mapinduzi haya, taarifa nyingi zinazohusu viongozi wa Gabon kutoroka Nchi hiyo zilianza kusambaa kwa kasi kwenye mitandao ya kijamii.
Miongoni mwa taaarifa hizo ni ile inayohusisha madai ya Spika wa Bunge la Gabon akiwa na mabegi yaliyojaa fedha akitaka kutoroka.
Mtumiaji mmoja wa mtandao wa X (Zamani Twitter) anayefahamika kwa jina la JoeSelasini ameiweka ikiambatana na ujumbe huu;
"Leo Spika wa Gabon aipotaka kutoroka. Africa tunaongozwa na majizi. Kwa miaka mingapi wamekuwa wakiibia hii nchi. Kwa hali hii mapinduzi yalihitajika maana kila uchaguzi walikuwa wakipita kwa kishindo."
Agosti 31, 2023, mtumiaji mwingine wa mtandao wa X, Sia Da Vinci aliweka pia video inayoonesha tukio hilo ikiwa na maneno haya;
"Kiongozi mwingine wa serikal ya Gabon iliyopinduliwa akamatwa na mabegi yenye fedha wakati akijaribu kutoroka nchi baada ya mapinduzi ya kijeshi."
Ukweli wa Madai haya upoje?
JamiiForums imefuatilia madai haya na kubaini mambo yafuatayo;
- Video hiyo sio ya Spika wa sasa wa Bunge la Gabon
- Ni video ya kweli, lakini sio ya sasa. Ilionekana mtandaoni siku za nyuma na haina uhusiano na kile kinachodaiwa kuwa ni kutoroka nchi kufuatia mapinduzi yaliyofanyika
Utafutaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiForums umebaini kuwa video hii imekuwepo mtandaoni tangu mwaka 2022. Mathalani, Septemba 18, 2022, akaunti ya Mtandao wa YouTube ya TV5 Monde iliweka video hii ikiwa na maelezo tofauti na yale yanayosambaa sasa.
JamiiForums imebaini kuwa anayeonekana kwenye video hii ni Guy Nzouba-Ndama, Rais wa zamani wa Bunge la Kitaifa la Gabon aliyekamatwa Septemba 17, 2022 akiwa na masanduku yaliyojaa zaidi ya faranga za CFA bilioni 11. Nzouba-Ndama alijiunga na upinzani mwaka 2016 baada ya kukihama chama tawala.
Aliteuliwa kwa mara ya kwanza serikalini Machi 1983 kwenye Wizara ya Nchi, Biashara na Viwanda. Kisha akateuliwa kuwa mjumbe kwenye Wizara ya Ardhi, Nyumba na Makazi mnamo Januari 1986 kabla ya kupandishwa cheo hadi nafasi ya Waziri wa Elimu ya Kitaifa Novemba 18 Novemba, 1987.
Guy Nzouba-Ndama kwenye screenshot ya video
Picha halisi ya Guy Nzouba-Ndama kutoka Mtandaoni
Katikati ya mgomo uliohusisha walimu, Rais Omar Bongo alimfukuza kutoka wadhifa wake kama Waziri wa Elimu Februari 26, 1990. Baadae alikuwa Mshauri wa Kisiasa wa Rais Bongo kuanzia Februari hadi Novemba 1990.
Katika uchaguzi wa ubunge wa 1990, alichaguliwa kuingia Bungeni na alikuwa Rais wa Kundi la Wabunge wa PDG kuanzia 1990 hadi 1996. Alichaguliwa tena kuwa mbunge katika uchaguzi wa wabunge wa Desemba 1996. Kufuatia uchaguzi wa mwisho, Nzouba-Ndama alichaguliwa kuwa Rais wa Bunge Januari 27, 1997.
Uthibitisho mwingine unaopingana na madai haya ni kuwa Rais wa sasa wa Bunge la Gabon ni Faustin Boukoubi aliyeingia kwenye nafasi hiyo Septemba 2019 na sio Guy Nzouba-Ndama anayeonekana kwenye video.
Taarifa za Guy Nzouba kukamatwa na mabegi yenye fedha zilichapishwa pia na majarida ya Les Pays, The North African Post, All Africa, La Libreville na Africa Intelligence.
Faustin Boukoubi, Rais wa sasa wa Bunge la Gabon
Hivyo, taarifa zinazosambaa zikimhusisha Rais wa sasa wa Bunge kukamatwa na Mabegi ya fedha akitoroka nchi sio za kweli.