Spika wa Bunge Tulia Ackson anashangaa kwanini hadi leo polisi bado inamshikilia Kada wa CHADEMA Kombo Mbwana

Spika wa Bunge Tulia Ackson anashangaa kwanini hadi leo polisi bado inamshikilia Kada wa CHADEMA Kombo Mbwana

Wacha waendelee kuwapitisha kwenye TANURI,wakomae na kuongeza umaarufu wao..

Ex Mayor Bon Yai anaenda kuwa GIANT POLITICIAN hasa kwa siasa za ukanda wa Mashariki..Kombo nae akiijipanga vizuri atasumbua HANDENI..nasubiri tu muda ufike ndugu yetu GEORGE wa Njombe awe HURU awe mbunge wa Njombe..CCM endeleeni kujifunga
 
Sheria mbovu ya TISS ameipitisha mwenyewe leo anashangaa
Maadui wakubwa zaidi kwa usalama na demokrasia katika nchi hii ni:-
1. Katiba mbaya & Sheria kandamizi zilizopo.
2. Ccm
3.Polisi.
4.Tiss.

Watanzania wakifanikiwa kuwashinda maadui hao, Basi watakuwa wamepata UKOMBOZI KAMILI.
 
Akiongea na Wasafi FM leo Spika wa bunge Mh. Tulia Ackson amesema anashangaa kwanini hadi leo hii polisi bado inamshikilia Kombo Mbwana kada wa CHADEMA.

Mbwana alipotea tangu June 15 baada ya kutekwa nyumbani kwake na watu wasiojulikana huko Tanga, awali polisi ilikana kuwa naye baadae ikakiri kumshikilia.

Tulia amesema "siyo sahihi kwa polisi kumshikilia mtu bila kutoa taarifa kwa jamii kwa sababu inaweza kuzua taharuki".

Alikuwa akijibu swali aliloulizwa na Waandishi wa habari kina Kitenge, 'ni kwa nini Polisi inakamata watu na kuwaficha bila kutoa taarifa hii inapelekea jamii kuhisi kuwa polisi inahusika na utekaji'.

Tulia aliongeza kusema, hili ni changamoto na linahitaji marekebisho ya sheria.
"linahitaji marekebisho ya sheria".
Atakaporudi bungeni na kutulia kwenye kiti chake cha enzi atasema huu si wakati wa kurekebisha sheria kwani tuna jukumu la kuandaa uchaguzi mkuu.
 
"linahitaji marekebisho ya sheria".
Atakaporudi bungeni na kutulia kwenye kiti chake cha enzi atasema huu si wakati wa kurekebisha sheria kwani tuna jukumu la kuandaa uchaguzi mkuu.
Tunaweza kumpigia simu 'Jaji Mkulu' yakaisha.
 
Hii ni sawa mama mwenye nyumba kushangaa kwanini house girl haoshi vyombo?
Kama mwenye mamlaka anashangaa ,je, mwananchi muuza viazi vya mafungu buguruni atafanyeje?
 
Back
Top Bottom