Spinning ni njia nzuri ya kupambana na mikutano ya hadhara ya upinzani kuliko kuikataza!

Mwl Athumani Ramadhani

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2022
Posts
1,280
Reaction score
2,522
Wakuu

Kuliko kuikataza mikutano ya hadhara kwa visingizio Mbali mbali ni bora kuifanyia spinning ili isilete madhara makubwa kwa wanaoiogopa!

CCM kama chama kikongwe bado kina vichwa vyenye uwezo wa kujenga hoja kwa kuanzisha mikutano ya ku spin hoja za wapinzani. Vichwa kama wasira, Kinana vina uwezo mkubwa wa kujenga hoja na dhana ya demokrasia ikatamalaki nchini!

Kuendelea kuikataza kwa sababu ambazo zina ukakasi zitaharibu taswira yetu ya kimataifa ambayo tumejijengea kwa miaka Mingi!

NAKUMBUKA awamu ya nne ya mzee kikwete aliweza sana kupambana kwa hoja na wapinzani na Hiyo ilisaidia sana ni wakati wetu kurudi kule amabpo ni pazuri kwa AFYA ya Taifa letu!

Kauli za kuzuia mikutano zinazotolewa ni nzito zenye kuogofya na ukakasi!

MUNGU ibariki Tanzania yetu

Mungu wabariki washauri na wafanya maamuzi wawe na maono ya Mbali!!
 
Hilo pozi tu kwa avatar linaonyesha wewe ni kilaza na cheo Mwl kwenye Id linamaanisha una njaa sana

Sent using Jamii Forums mobile app
Pozi halafu cheo!kina uhusiano gani na NJAA!!?

Pesa hazina MWENYEWE hata wasiosoma wanazo tena nyingi!!

Cheo au pozi hakina uhusiano na kumiliki au kutomiliki UTAJIRI,Bali kazi na malengo tu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…