SPORTPESA SUPER CUP SPECIAL THREAD: Taarifa za Mechi zote na matokeo yote mpaka Ubingwa

SPORTPESA SUPER CUP SPECIAL THREAD: Taarifa za Mechi zote na matokeo yote mpaka Ubingwa

Roma haikujengwa kwa Siku Moja.

Naamini kama ipo dhamira njema ya kujiboresha basi watabadilika, muhimu wapokee maoni ya Walaji/watazamaji na kuyafanyia kazi.
Independent Television
 
Katika hili Sportpesa wamechemka sana..Wangewapa hata Star TV au TBC...

Hawaoneshi dakika, hawaoneshi mfungaji anayeingia/anayetoka..Hawaoneshi hata penati zilizofungwa ama kupotezwa
mkuu hata ubora wa picha ni mbovu mbovu ,picha inagiza sana ,kweli Azam wapo mbali
 
wanatia aibu, ukijumlisha na hizi aibu tunazotiwa na uongozi wa awamu ya tano, kwa kweli wakenya mnayoyaona yaacheni hapa hapa bongo. huko radio one kina wanatangaza goli kukoswa-koswa wakati mpira upo nje ya kumi na nane

Bongo bahati mbaya tu
 
Hata uchambuzi leo mchambuzi anamtaja Dida wakati hakucheza ITV yao Malumbano ya Hoya tu live ndio wanaweza
 
Yaani nilikereka hatari, kheri AzamTV japo wana dosari ila kwa bongo wanajitahidi...

ITV mtu wenu wa graphics mmemtoa wapi eti, maana juzi niliona mkijitapa kuwa nyie ndio waanzilishi wa kurusha michezo live. Maana kuna wakati hata mchukuaji alisahau kuelekeza camera kwenyr mpira ulipo.

Pia sauti, sauti ilikuwa hovyo mara tusikie sauti ya mtangazaji wa radio mara arudi wa tv.

Camera hazikuwa na mwanga mmoja, hii giza hii inaonyesha jua kali la saa saba.

Replay! Dah! Replay basi wekeni deferent angle nyie mnatuwekea ile ila ya wide tunawezaje sasa kuona tukio lilitokea kwa mbali.

Rekebisheni hiyo!
 
Asikuambie mtu radha kamili ya soka huwa sionagi michezo ikichezwaga kwenye uwanja wa Uhuru!
Si wangeenda hata kuomba dimba la Azam basi maana Uhuru ni kama wanacheza kibarazani... Hakuna radha
 
Wengine sisi hatuna vifurushi vya azam hiyo ITV na kamera zake tumeridhika
 
Azam naona kagoma kurusha mashindano ya kamari, bora ungewapa hata clouds TV ila IPP hakuna kabisa
Azam hata kuripoti hayo mashindano hajaripoti chochote, sijajua kususa au Vp
 
Back
Top Bottom