SportsPesa Cup: Bandari 2 vs 1 Simba

SportsPesa Cup: Bandari 2 vs 1 Simba

TANGU LINI SIMBA AKAMUDU KAZI ZA BANDARI? HAHAHAH WAUEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEE
 
Ifike wakati tuwe wakweli,Tanzania mpira inabidi tujipange,kwa ndani tunaweza kuona tunajiweza lakini kwa hakika tukitoka nje hamna kitu. Ukweli mchungu huo. Na hilo ni kwa Simba,Yanga,Azam na team yoyote. Kwa hakika tumepoteza dira. Tubaki tu kujisifia mechi za ndani lakini huko nje ni shida tupu,inatia sana simanzi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na hapo kuna international players km 8,kocha wa kigeni na msaidizi wake, na fedha zipo
Mkuu umeandika kwa kumaanisha au kwa Sababu Simba imetolewa? Kwanini wasitumie michuano kama hii kama njia ya kujiimarisha na kurekebisha makosa yao? Ina maana kweli mkuu huyaoni mapungufu makubwa ya hichi kikosi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu umeandika kwa kumaanisha au kwa Sababu Simba imetolewa? Kwanini wasitumie michuano kama hii kama njia ya kujiimarisha na kurekebisha makosa yao? Ina maana kweli mkuu huyaoni mapungufu makubwa ya hichi kikosi?
Nasema nikimaanisha maana naonaga kama ni upumbavu kabisa unaoendelea hapa Tanzania katika medani ya soka.

Haiwezekani eti Simba leo inacheza Klabu Bingwa Afrika alafu kesho Simba hiyo hiyo inacheza Mapinduzi Cup.

Alafu Simba hiyo hiyo inashiriki Ligi Kuu ambayo tayari kuna team zimeshacheza mechi saba zaidi yake.


Hivi hawa viongozi wa soka wa hii nchi ni machizi au wamelogwa.
 
Simba tumedharau game, mechi ilikua nyeupe kabisa hii
Sio kudharau mkuu,uwezo wetu bado sana asee. Nilichotegemea ni kuona kuna 'Improvement' katika baadhi ya idara ili kusahihisha makosa yaliyofanyika Congo.
Ila ninachokishuhudia ni madudu tu kila siku,inapiga hatua 10 nyuma kwasasa. Huoni mnyumbuliko wa wachezaji kabisa.
Hili nakiri kabisa Simba ni Underdog kwenye kundi lake.
 
Mkuu umesema vema kabisa, Simba hamna dira kilichopo Ni kelele na ngonjera tu, hatuna kocha kabisa hapo, hatuna kampuni imara kabisa, wanaleta wachezaji hovyo kabisa, Simba Simba Simba nimekuita Mara tatu....Simba wanatudhalilisha sisi mashabiki
Kila kitu tunachukulia rahisi tu hatueleweki tunataka nini.Hii ni aibu kubwa kwa klabu inayoshiriki klabu bingwa.

Daima toa bila kukumbuka na Pokea bila kusahau
 
Back
Top Bottom