TANZIA SSGT Reginald Ruta wa JWTZ amejiua kwenye Kaburi la marehemu Mkewe

TANZIA SSGT Reginald Ruta wa JWTZ amejiua kwenye Kaburi la marehemu Mkewe

Mleta Uzi unaouhusiano gani na Matukio ya Vifo siku hizi?
Maana kila nikiingia nakumbana na Uzi wako juu,
Tanzia,tanzia,tanzia, unafikirisha.
 
Doh

Nimekumbuka mbali Sana. Picha kama hii hii ila mume yeye hakujiua bali alikufa ghafla siku mbili tu baada ya mkewe kufariki Kuna watu wanajua kupenda bhanaa nyie acheni, hii ndo ile, "nitakupenda hadi kufa kwangu"
Hakika kabisa yaan.
 
Kwa ambaye anamfahamu SSGT Ruta alikuwa Msata amejiua kwenye kaburi la mke wake ambaye alifariki siku ya Jumamosi huko Kilakala kaacha ujumbe kuwa alikuwa anampenda mke wake.

========

Dar es Salaam. Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Reginald Ruta amekutwa amekufa huku mwili wake ukiwa juu ya kaburi la mkewe, Godebertha aliyezikwa katika makaburi ya Mekyuri Kipawa jeshini mkoani Dar es Salaam.

Juni 7, mwaka huu mwili wa askari huyo aliyezikwa katika makaburi hayo jana, ulikutwa katika kaburi la mkewe aliyefariki dunia Alhamisi iliyopita baada ya kuugua ghafla.

Kifo cha askari huyo wa kambi ya Msata mkoani Pwani kimeacha simanzi kwa ndugu, jamaa na marafiki, kwa kuwa kilitokea siku tatu tangu mkewe afariki.

Akisoma risala kwenye ibada ya kuaga mwili wa askari huyo, iliyofanyika nyumbani kwake mtaa wa Karakata Kipawa, diwani wa Karakata, Idary Karugendo alisema marehemu ameacha watoto wanne na wajukuu watano waliokuwa wanamtegemea.

“Mzee Ruta alikuwa tegemeo kwenye familia yake kama baba, hasa baada ya kifo cha mke wake kutokea siku chache zilizopita,” alisema Karugendo.

Akizungumza katika ibada hiyo, Katekista wa Kanisa Katoliki la Bikira Maria Kipawa, Silivester Sadick alisema kifo hicho ni funzo kubwa kwa watu wote na kinaonyesha wazi hakuna binadamu mkubwa mbele ya Mungu.

“Juzi tulikuwa hapa hapa, tena nawaongoza kwenye ibada ya kumuaga mke wake, hakuna aliyekuwa anajua nani anafuata lakini leo mzee Ruta anafuata, ni funzo kubwa ndio maana nawakumbusha kuzidi kumuomba Mungu wakati wote,” alisema.

Alisema kifo kinaharibu mipango yote ambayo binadamu anakuwa amejipangia kuitekeleza na ndiyo maana watu husema kifo hakina huruma, lakini ukishakufa unakwenda kwa Mwenyezi Mungu.

“Maisha ya hapa duniani yanapita, juzi tulizungumza hatujui nani anafuata, lakini mume ameenda, kama maisha yetu yako namna hii binadamu ni nani mbele ya Mungu.

Familia ipo kwenye wakati mgumu, kama ingekuwa ni mimi leo ingekuwaje, kikubwa tujitengenezee njia ya kufika mbinguni mapema na naiomba familia kuzidi kufanya maombi na kusimama katika imani kwa Mungu kwani hawezi kuwaacha,” alisema.

Kifo kilivyotokea

Kwa mujibu wa jirani mmoja ambaye hakutaka kutaja jina lake, alidai kuwa walikuwa wote na Ruta siku ya Jumamosi ambayo yalifanyika mazishi ya mkewe aliyefariki ghafla wakati akijiandaa kwenda kazini.

Alisema baada ya mazishi Jumatatu iliyopita, vijana waliokuwa wanachunga mbuzi waliukuta mwili wake juu ya kaburi hilo.

Chanzo hicho kilieleza kwamba watoto hao baada ya kuona mwili huo wakaenda kutoa taarifa jeshini kwa sababu eneo hilo linamilikiwa na Jeshi na walipofika pale wakampekua hawakuona chochote zaidi ya kitambulisho chake.

Taarifa zaidi zinaeleza kuwa baada ya mazishi ya mkewe, Jumapili iliyopita Ruta alifanya vikao vya mara kwa mara na watoto wake wanne na kuwaeleza mali alizonazo na sehemu zilipo.

“Baada ya kufanya vikao virefu na watoto wake huku akiwachekesha muda wote, aliwaambia kuwa atakwenda kununua marumaru kwa ajili ya kujengea kaburi la mkewe na aliwaeleza kuwa akishafanya manunuzi atawaeleza,” zinaeleza taarifa hizo.

Habari zaidi zinaeleza kuwa alimuomba mwanaye mmoja ampe Sh50,000 kwa ajili ya kununua marumaru hizo na alipopewa fedha hizo aliondoka nyumbani hakurejea tena.

Polisi wanena

Kamanda wa Polisi mkoa wa Kipolisi Ilala, Janeth Magomi alikiri kupokea taarifa ya kifo na kudai ililetwa na wanajeshi wenzake kutoka kituo cha Polisi Stakishari.

“Kwamba kuna mwenzao wamemkuta amefariki juu ya kaburi la mkewe, wakati wanatoa taarifa hiyo tayari mwili ulishachukuliwa na kupelekwa hospitali ya Lugalo,” alisema Janeth.

View attachment 1815077
View attachment 1815080
With due respect naomba kuuliza, Kanisa Katoliki lilianza lini kuendesha Ibada ya Mazishi kwa mtu aliyejinyonga (kujiua)?
 
Sasa watoto wake kamwachia nani? hivi wahaya nao wana akili za hovyo namna hii.......nyegera waitu.
 
Wengi humu mtamlaumu lakini depression is real and inatisha sana ...Apumzike kwa amani MUNGU pekee ndo ajuae kipi alipitia mpaka kufikia maamuz ayo may his soul rest in peace
 
Kipo alichokikosa kwa mkewe huku akiamini hawezi kuishi bila yeye, na mbaya zaidi akakosa hata faraja ya walimwengu
Na si ajabu hata yeye ndio chanzo cha kifo cha mkewe akawa anafeel guilty.Who knows?
 
Sio tajiri ila walau alikuwa na kitu kwa ajili ya wanae.. Lakini kajimaliza kwa sababu nyepesi sana

Sent using Jamii Forums mobile app
Kazingua .
Yeye kaondokewa na make wengine wameondokewa na mama na wengine Bibi .kaona haitoshi kaamua kujimuvu,Isha nayeye ilinkiongeza pugo kwa wanawe na wajukuu
 
NAAM NAMI NATAFUTA MKE MPENZI NITAKAYE MPENDA KULIKO UHAI WANGU.
YEYOTE MWENYE NIA NJOO PM,

KIKUBWA UMRI 30+
KABILA LOLOTE
DINI YOYOTE
 
Na si ajabu hata yeye ndio chanzo cha kifo cha mkewe akawa anafeel guilty.Who knows?

Au ndugu wa karibu wanataka kuchukua na kumiliki mali zao, au kuna mtu wanamdai kaamua afanye yake.... yote yanawezekani
 
Huyu jamaa amekufa kifo cha kijinga sana na cha kujitakia. Wanawake wote warembo waliojaa hapa nchini ameshindwa kukamata mmoja amuoe azibe pengo la mkewe badala yake amejitoa roho? Mpuuzi mkubwa. Rest In Hell (RIH). Tazama sasa hili jinga limewaacha watoto yatima kwa 100% halafu eti linawapa wosia wawe wanasali!!! Lenyewe limeshindwa kusali limejitoa uhai kiumbwa linawaambia watoto wasali? Ni hasara kubwa sana kuwa na baba la aina hii. Bora hata limekuga!! Afu eti lianajeshi!!! Hili linaweza kuhimili vita kweli ikiwa akifa mkewe tu linajitoa roho? Pumbavu sana!!!
 
Back
Top Bottom