TANZIA SSGT Reginald Ruta wa JWTZ amejiua kwenye Kaburi la marehemu Mkewe

Kwa ambaye anamfahamu SSGT Ruta alikuwa Msata amejiua kwenye kaburi la mke wake ambaye alifariki siku ya Jumamosi huko kilakala kaacha ujumbe kuwa alikuwa anampenda mke wake.

========

Dar es Salaam. Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Reginald Ruta amekutwa amekufa huku mwili wake ukiwa juu ya kaburi la mkewe, Godebertha aliyezikwa katika makaburi ya Mekyuri Kipawa jeshini mkoani Dar es Salaam.

Juni 7, mwaka huu mwili wa askari huyo aliyezikwa katika makaburi hayo jana, ulikutwa katika kaburi la mkewe aliyefariki dunia Alhamisi iliyopita baada ya kuugua ghafla.

Kifo cha askari huyo wa kambi ya Msata mkoani Pwani kimeacha simanzi kwa ndugu, jamaa na marafiki, kwa kuwa kilitokea siku tatu tangu mkewe afariki.

Akisoma risala kwenye ibada ya kuaga mwili wa askari huyo, iliyofanyika nyumbani kwake mtaa wa Karakata Kipawa, diwani wa Karakata, Idary Karugendo alisema marehemu ameacha watoto wanne na wajukuu watano waliokuwa wanamtegemea.

“Mzee Ruta alikuwa tegemeo kwenye familia yake kama baba, hasa baada ya kifo cha mke wake kutokea siku chache zilizopita,” alisema Karugendo.

Akizungumza katika ibada hiyo, Katekista wa Kanisa Katoliki la Bikira Maria Kipawa, Silivester Sadick alisema kifo hicho ni funzo kubwa kwa watu wote na kinaonyesha wazi hakuna binadamu mkubwa mbele ya Mungu.

“Juzi tulikuwa hapa hapa, tena nawaongoza kwenye ibada ya kumuaga mke wake, hakuna aliyekuwa anajua nani anafuata lakini leo mzee Ruta anafuata, ni funzo kubwa ndio maana nawakumbusha kuzidi kumuomba Mungu wakati wote,” alisema.

Alisema kifo kinaharibu mipango yote ambayo binadamu anakuwa amejipangia kuitekeleza na ndiyo maana watu husema kifo hakina huruma, lakini ukishakufa unakwenda kwa Mwenyezi Mungu.

“Maisha ya hapa duniani yanapita, juzi tulizungumza hatujui nani anafuata, lakini mume ameenda, kama maisha yetu yako namna hii binadamu ni nani mbele ya Mungu.

Familia ipo kwenye wakati mgumu, kama ingekuwa ni mimi leo ingekuwaje, kikubwa tujitengenezee njia ya kufika mbinguni mapema na naiomba familia kuzidi kufanya maombi na kusimama katika imani kwa Mungu kwani hawezi kuwaacha,” alisema.

Kifo kilivyotokea

Kwa mujibu wa jirani mmoja ambaye hakutaka kutaja jina lake, alidai kuwa walikuwa wote na Ruta siku ya Jumamosi ambayo yalifanyika mazishi ya mkewe aliyefariki ghafla wakati akijiandaa kwenda kazini.

Alisema baada ya mazishi Jumatatu iliyopita, vijana waliokuwa wanachunga mbuzi waliukuta mwili wake juu ya kaburi hilo.

Chanzo hicho kilieleza kwamba watoto hao baada ya kuona mwili huo wakaenda kutoa taarifa jeshini kwa sababu eneo hilo linamilikiwa na Jeshi na walipofika pale wakampekua hawakuona chochote zaidi ya kitambulisho chake.

Taarifa zaidi zinaeleza kuwa baada ya mazishi ya mkewe, Jumapili iliyopita Ruta alifanya vikao vya mara kwa mara na watoto wake wanne na kuwaeleza mali alizonazo na sehemu zilipo.

“Baada ya kufanya vikao virefu na watoto wake huku akiwachekesha muda wote, aliwaambia kuwa atakwenda kununua marumaru kwa ajili ya kujengea kaburi la mkewe na aliwaeleza kuwa akishafanya manunuzi atawaeleza,” zinaeleza taarifa hizo.

Habari zaidi zinaeleza kuwa alimuomba mwanaye mmoja ampe Sh50,000 kwa ajili ya kununua marumaru hizo na alipopewa fedha hizo aliondoka nyumbani hakurejea tena.

Polisi wanena

Kamanda wa Polisi mkoa wa Kipolisi Ilala, Janeth Magomi alikiri kupokea taarifa ya kifo na kudai ililetwa na wanajeshi wenzake kutoka kituo cha Polisi Stakishari.

“Kwamba kuna mwenzao wamemkuta amefariki juu ya kaburi la mkewe, wakati wanatoa taarifa hiyo tayari mwili ulishachukuliwa na kupelekwa hospitali ya Lugalo,” alisema Janeth.

View attachment 1815077
View attachment 1815080
Fucking coward, hivi mwanajeshi unajiuaje wakati upo uraiani? Sio kama umetekwa vitani?! How can you justfy taking ur own life?

Fucking coward, jitu lina miaka 50, linajiua! Bora ujiue kama unaumwa unahofia utawapa hasara wakikuuguza kwa muda mrefu,

This is totally shit
 
Fucking coward,hivi mwanajeshi unajiuje wakati upo uraiani?sio kama umetekwa vitani?!how can you justfy taking ur own life?
Fucking coward,jitu lina miaka 50,linajiua!Bora ujiue kama unaumwa unahofia utawapa hasara wakikuuguza kwa muda mrefu,
This is totally shit
Mapenzi hayana baunsa ndugu yangu hasa yanapogusa kwenye hisia halisi ndani ya moyo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dah alale salama
Pole kwa watoto, familia na wote walioguswa na msiba

Hakuna cha kulala salama hapo, hapo ni jahannam inamhusu.

وَلَا تَقْتُلُوا النَّفْسَ الَّتِي حَرَّمَ اللَّهُ إِلَّا بِالْحَقِّ ۗ وَمَنْ قُتِلَ مَظْلُومًا فَقَدْ جَعَلْنَا لِوَلِيِّهِ سُلْطَانًا فَلَا يُسْرِفْ فِي الْقَتْلِ ۖ إِنَّهُ كَانَ مَنْصُورًا

Wala msiuwe nafsi ambayo Mwenyezi Mungu amekataza isipo kuwa kwa haki. Na aliye uliwa kwa kudhulumiwa basi tumempa madaraka mrithi wake. Lakini asipite mpaka katika kuuwa. Kwani yeye anasaidiwa.
 
Unaona nyepesi wewe..sio nyepesi hata kidg
Hata kama ni nzito:
1. Haitoshi kujitoa uhai wako au wa mtu mwingine. Ni makosa tu kisheria, kidini na hata kimaadili.
2. Kwa kuwa mkewe keshakufa, matarajio ya kawaida ni kufikiria namna ya kulea watoto wake akiwa peke yake, na sio kuwapa watoto hasara na simanzi ya kupoteza mzazi mwingine tena. Ni mbinafsi.

Well, nakubaliana na wepesi au uzito ni relative. Lakini ni je uzito wa kujitoa uhai? Kweli?
 
Askari unakufaje kizembe hivyo aisee.!! Si bora angeomba aende Congo huko au Darfur akafie vitani huko.
Nao ni binadam. askari sio roboti. nje ya service. kuna familia pia. kuna maisha ambayo hayakuondolei ubinadam
 
Hata kama ni nzito:
1.Haitoshi kujitoa uhai wako au wa mtu mwingine. Ni makosa tu kisheria, kidini na hata kimaadili.
2. Kwa kuwa mkewe keshakufa, matarajio ya kawaida ni kufikiria namna ya kulea watoto wake akiwa peke yake, na sio kuwapa watoto hasara na simanzi ya mzazi mwingine tena.

Well, nakubaliana na wepesi au uzito ni relative. Lakini ni je uzito wa kujitoa uhai? Kweli?
Kimungu , kimaandiko ni kosa na kwa Mungu ni kosa ila kibinadamu wakati mgumu unaweza kuona dunia nzima umebaki mwenyewe tu
 
Kwa ambaye anamfahamu SSGT Ruta alikuwa Msata amejiua kwenye kaburi la mke wake ambaye alifariki siku ya Jumamosi huko kilakala kaacha ujumbe kuwa alikuwa anampenda mke wake.

========

Dar es Salaam. Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Reginald Ruta amekutwa amekufa huku mwili wake ukiwa juu ya kaburi la mkewe, Godebertha aliyezikwa katika makaburi ya Mekyuri Kipawa jeshini mkoani Dar es Salaam.

Juni 7, mwaka huu mwili wa askari huyo aliyezikwa katika makaburi hayo jana, ulikutwa katika kaburi la mkewe aliyefariki dunia Alhamisi iliyopita baada ya kuugua ghafla.

Kifo cha askari huyo wa kambi ya Msata mkoani Pwani kimeacha simanzi kwa ndugu, jamaa na marafiki, kwa kuwa kilitokea siku tatu tangu mkewe afariki.

Akisoma risala kwenye ibada ya kuaga mwili wa askari huyo, iliyofanyika nyumbani kwake mtaa wa Karakata Kipawa, diwani wa Karakata, Idary Karugendo alisema marehemu ameacha watoto wanne na wajukuu watano waliokuwa wanamtegemea.

“Mzee Ruta alikuwa tegemeo kwenye familia yake kama baba, hasa baada ya kifo cha mke wake kutokea siku chache zilizopita,” alisema Karugendo.

Akizungumza katika ibada hiyo, Katekista wa Kanisa Katoliki la Bikira Maria Kipawa, Silivester Sadick alisema kifo hicho ni funzo kubwa kwa watu wote na kinaonyesha wazi hakuna binadamu mkubwa mbele ya Mungu.

“Juzi tulikuwa hapa hapa, tena nawaongoza kwenye ibada ya kumuaga mke wake, hakuna aliyekuwa anajua nani anafuata lakini leo mzee Ruta anafuata, ni funzo kubwa ndio maana nawakumbusha kuzidi kumuomba Mungu wakati wote,” alisema.

Alisema kifo kinaharibu mipango yote ambayo binadamu anakuwa amejipangia kuitekeleza na ndiyo maana watu husema kifo hakina huruma, lakini ukishakufa unakwenda kwa Mwenyezi Mungu.

“Maisha ya hapa duniani yanapita, juzi tulizungumza hatujui nani anafuata, lakini mume ameenda, kama maisha yetu yako namna hii binadamu ni nani mbele ya Mungu.

Familia ipo kwenye wakati mgumu, kama ingekuwa ni mimi leo ingekuwaje, kikubwa tujitengenezee njia ya kufika mbinguni mapema na naiomba familia kuzidi kufanya maombi na kusimama katika imani kwa Mungu kwani hawezi kuwaacha,” alisema.

Kifo kilivyotokea

Kwa mujibu wa jirani mmoja ambaye hakutaka kutaja jina lake, alidai kuwa walikuwa wote na Ruta siku ya Jumamosi ambayo yalifanyika mazishi ya mkewe aliyefariki ghafla wakati akijiandaa kwenda kazini.

Alisema baada ya mazishi Jumatatu iliyopita, vijana waliokuwa wanachunga mbuzi waliukuta mwili wake juu ya kaburi hilo.

Chanzo hicho kilieleza kwamba watoto hao baada ya kuona mwili huo wakaenda kutoa taarifa jeshini kwa sababu eneo hilo linamilikiwa na Jeshi na walipofika pale wakampekua hawakuona chochote zaidi ya kitambulisho chake.

Taarifa zaidi zinaeleza kuwa baada ya mazishi ya mkewe, Jumapili iliyopita Ruta alifanya vikao vya mara kwa mara na watoto wake wanne na kuwaeleza mali alizonazo na sehemu zilipo.

“Baada ya kufanya vikao virefu na watoto wake huku akiwachekesha muda wote, aliwaambia kuwa atakwenda kununua marumaru kwa ajili ya kujengea kaburi la mkewe na aliwaeleza kuwa akishafanya manunuzi atawaeleza,” zinaeleza taarifa hizo.

Habari zaidi zinaeleza kuwa alimuomba mwanaye mmoja ampe Sh50,000 kwa ajili ya kununua marumaru hizo na alipopewa fedha hizo aliondoka nyumbani hakurejea tena.

Polisi wanena

Kamanda wa Polisi mkoa wa Kipolisi Ilala, Janeth Magomi alikiri kupokea taarifa ya kifo na kudai ililetwa na wanajeshi wenzake kutoka kituo cha Polisi Stakishari.

“Kwamba kuna mwenzao wamemkuta amefariki juu ya kaburi la mkewe, wakati wanatoa taarifa hiyo tayari mwili ulishachukuliwa na kupelekwa hospitali ya Lugalo,” alisema Janeth.

View attachment 1815077
View attachment 1815080
Sex inamuunganiko wa kiroho legacy ya mkewe imemualika kuzimu

R I P bro
 
Kimungu , kimaandiko ni kosa na kwa Mungu ni kosa ila kibinadamu wakati mgumu unaweza kuona dunia nzima umebaki mwenyewe tu
...labda kwa kuwa hatujui vitu vingi vinavyozunguka maamuzi yake.
 
Doh

Nimekumbuka mbali Sana. Picha kama hii hii ila mume yeye hakujiua bali alikufa ghafla siku mbili tu baada ya mkewe kufariki Kuna watu wanajua kupenda bhanaa nyie acheni, hii ndo ile, "nitakupenda hadi kufa kwangu"
 
Hata kama ni nzito:
1. Haitoshi kujitoa uhai wako au wa mtu mwingine. Ni makosa tu kisheria, kidini na hata kimaadili.
2. Kwa kuwa mkewe keshakufa, matarajio ya kawaida ni kufikiria namna ya kulea watoto wake akiwa peke yake, na sio kuwapa watoto hasara na simanzi ya kupoteza mzazi mwingine tena. Ni mbinafsi.

Well, nakubaliana na wepesi au uzito ni relative. Lakini ni je uzito wa kujitoa uhai? Kweli?
Hujapenda wewe...hata mimi naweza jitoa uhai kwaajili ya mapenzi...wee acha kbs!ndo maana kasema wanaye wamsamehe
 
Back
Top Bottom