TANZIA SSGT Reginald Ruta wa JWTZ amejiua kwenye Kaburi la marehemu Mkewe

TANZIA SSGT Reginald Ruta wa JWTZ amejiua kwenye Kaburi la marehemu Mkewe

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
301,577
Reaction score
754,412
Kwa ambaye anamfahamu SSGT Ruta alikuwa Msata amejiua kwenye kaburi la mke wake ambaye alifariki siku ya Jumamosi huko Kilakala kaacha ujumbe kuwa alikuwa anampenda mke wake.

========

Dar es Salaam. Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Reginald Ruta amekutwa amekufa huku mwili wake ukiwa juu ya kaburi la mkewe, Godebertha aliyezikwa katika makaburi ya Mekyuri Kipawa jeshini mkoani Dar es Salaam.

Juni 7, mwaka huu mwili wa askari huyo aliyezikwa katika makaburi hayo jana, ulikutwa katika kaburi la mkewe aliyefariki dunia Alhamisi iliyopita baada ya kuugua ghafla.

Kifo cha askari huyo wa kambi ya Msata mkoani Pwani kimeacha simanzi kwa ndugu, jamaa na marafiki, kwa kuwa kilitokea siku tatu tangu mkewe afariki.

Akisoma risala kwenye ibada ya kuaga mwili wa askari huyo, iliyofanyika nyumbani kwake mtaa wa Karakata Kipawa, diwani wa Karakata, Idary Karugendo alisema marehemu ameacha watoto wanne na wajukuu watano waliokuwa wanamtegemea.

“Mzee Ruta alikuwa tegemeo kwenye familia yake kama baba, hasa baada ya kifo cha mke wake kutokea siku chache zilizopita,” alisema Karugendo.

Akizungumza katika ibada hiyo, Katekista wa Kanisa Katoliki la Bikira Maria Kipawa, Silivester Sadick alisema kifo hicho ni funzo kubwa kwa watu wote na kinaonyesha wazi hakuna binadamu mkubwa mbele ya Mungu.

“Juzi tulikuwa hapa hapa, tena nawaongoza kwenye ibada ya kumuaga mke wake, hakuna aliyekuwa anajua nani anafuata lakini leo mzee Ruta anafuata, ni funzo kubwa ndio maana nawakumbusha kuzidi kumuomba Mungu wakati wote,” alisema.

Alisema kifo kinaharibu mipango yote ambayo binadamu anakuwa amejipangia kuitekeleza na ndiyo maana watu husema kifo hakina huruma, lakini ukishakufa unakwenda kwa Mwenyezi Mungu.

“Maisha ya hapa duniani yanapita, juzi tulizungumza hatujui nani anafuata, lakini mume ameenda, kama maisha yetu yako namna hii binadamu ni nani mbele ya Mungu.

Familia ipo kwenye wakati mgumu, kama ingekuwa ni mimi leo ingekuwaje, kikubwa tujitengenezee njia ya kufika mbinguni mapema na naiomba familia kuzidi kufanya maombi na kusimama katika imani kwa Mungu kwani hawezi kuwaacha,” alisema.

Kifo kilivyotokea

Kwa mujibu wa jirani mmoja ambaye hakutaka kutaja jina lake, alidai kuwa walikuwa wote na Ruta siku ya Jumamosi ambayo yalifanyika mazishi ya mkewe aliyefariki ghafla wakati akijiandaa kwenda kazini.

Alisema baada ya mazishi Jumatatu iliyopita, vijana waliokuwa wanachunga mbuzi waliukuta mwili wake juu ya kaburi hilo.

Chanzo hicho kilieleza kwamba watoto hao baada ya kuona mwili huo wakaenda kutoa taarifa jeshini kwa sababu eneo hilo linamilikiwa na Jeshi na walipofika pale wakampekua hawakuona chochote zaidi ya kitambulisho chake.

Taarifa zaidi zinaeleza kuwa baada ya mazishi ya mkewe, Jumapili iliyopita Ruta alifanya vikao vya mara kwa mara na watoto wake wanne na kuwaeleza mali alizonazo na sehemu zilipo.

“Baada ya kufanya vikao virefu na watoto wake huku akiwachekesha muda wote, aliwaambia kuwa atakwenda kununua marumaru kwa ajili ya kujengea kaburi la mkewe na aliwaeleza kuwa akishafanya manunuzi atawaeleza,” zinaeleza taarifa hizo.

Habari zaidi zinaeleza kuwa alimuomba mwanaye mmoja ampe Sh50,000 kwa ajili ya kununua marumaru hizo na alipopewa fedha hizo aliondoka nyumbani hakurejea tena.

Polisi wanena

Kamanda wa Polisi mkoa wa Kipolisi Ilala, Janeth Magomi alikiri kupokea taarifa ya kifo na kudai ililetwa na wanajeshi wenzake kutoka kituo cha Polisi Stakishari.

“Kwamba kuna mwenzao wamemkuta amefariki juu ya kaburi la mkewe, wakati wanatoa taarifa hiyo tayari mwili ulishachukuliwa na kupelekwa hospitali ya Lugalo,” alisema Janeth.

1623399506337.png

1623399632583.png
 
Sio tajiri ila walau alikuwa na kitu kwa ajili ya wanae.. Lakini kajimaliza kwa sababu nyepesi sana

Sent using Jamii Forums mobile app

Kwa kibongo bongo Msoja alikuwa tajiri ,ana mali nyingi tu ,kama magari manne ,nyumba 5 ,viwanja ,anaowadai pesa nyingi wa kutosha,accounts zenye pesa banks za kutosha!! Itakuwa pepo la kifo lilimdaka!
 
Kama Mkewe alifariki kisha na yeye ndio hivyo basi hajawatendea haki watoto wake.
Labda inawezekana Katoka kujipima VVU bila kupata ushauri nasaha.

Mzazi unapofanya maamuzi kama haya ni rahisi sana tukio kama hili la kujiua kuja kujirudia tena kwenye familia. Anawafanya watoto wake wakiwa kwenye Sonona nao waone njia rahisi ni kujiua.
 
Back
Top Bottom